Punguza jazba mjomba, ndivyo dunia ilivyo.
Huyo singo maza nikimuoa anakua mke wangu, wa ubani, mbavu yangu ya kushoto, msiri wangu na mengine mengi.
Sasa niache kumsaidia huyu ati kisa mtoto wa binamu yake mjomba ana shida fulani?
Imagine huyo single maza kanizalia wana, niache kumpiga tafu kwa dogo lake moja ilhali wote ni watoto tu.
Kama nilivyokwisha kuandika awali, kama uwezo wako ni wa ngama kama wangu huwezi toa chochote na ni kheri uache, lakini kama uwezo unao toa tu.
Usimp haupimwi kwa maandishi bali vitendo, ukatili na roho mbaya ya kibandidu sio ishara ya kua wewe ndio mwanaume bora, matendo ya huruma, misaada na upendo sio ishara ya usimp, usichanganye hayo.