PreGE2025 Hasheem Rungwe asema sasa analindwa, kila kitu kimebadilika na usafiri mpya amepewa. Asema mshenga alikuwa John Mrema

PreGE2025 Hasheem Rungwe asema sasa analindwa, kila kitu kimebadilika na usafiri mpya amepewa. Asema mshenga alikuwa John Mrema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu ndo mpinzani wa kweli, siyo Wewe na Mbowe wenu mmepewa rushwa mmekauka kimya, kisa mnajua kutunza Siri. Acha sisi tuende na wakili msomi mzee Hashimu Spunda. Ukimhonga umeyakanyaga ndo maana CCM wakaishia kuwahonga chadema mnaojua kutunza Siri.
Huyo unayemjibu ni mbogamboga mwenzako ujue.
 
Tukiweka siasa pembeni. Mzee Rungwe yupo fresh sana. Vijana tulikuwa tukihitaji milioni 5 au 10 ya chap chap unaenda ofisi yake anaithaminisha ndinga yako unaipaki uani mnakubaliana anakupa mpunga ukifanya mambo yako unarudisha pesa kutokana na makubaliano unachukua ndinga yako.
Kwa hili nampa maua yake
 
Mzee Spunda. Viongozi wako huku chini wanatuzungusha kutupa kadi za chama, hatupo wengi na hatuathiri bajeti ya ubwabwa. Tafadhali nipokee na mimi natokea Chama Kubwa huku
 
Hahaha ndio uzuri wake huwa hataki dhambi ya uongo na unafiki iko siku atasema kweli ni nani aliratibu waingie na alilipwa kiasi gani.

Njaa haina bouncer.

G-55, madalali na chawa ulikuwa mzigo kwenye safari isiyo na matumaini. Ama hakika ilikuwa Bora mno wakwendree!
imhotep, Fortilo, Drifter, binti kiziwi na wale wengine au nasema uongo?
 
Kwa umri wake hana cha kupoteza anafunguka tuu😂😂😂
Inakuwa vigumu sana kumshushia shoka la lawama mtu kama huyu, kuwa sehemu ya kizingiti cha kutafuta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi hii!

Sasa sijui tusemeje kwa mtu kama huyu!

Kwa upande mmoja kasaidia kuondoa uchafu ndani ya chama kinacho onekana kupigania HAKI ya waTanzania kujinusuru toka kwa hawa majangiri ya Genge la wauaji; na kwa upande wa pili, ni kama anawapa nafasi majangili hawa kumtumia katika kufifisha juhudi za kuwadhibiti Genge la wauaji, kwa kumtumia yeye na chama chake.
 
Back
Top Bottom