Wameshaamua kusimamia wanachokiamini, kufa kwao sio issue tena, kifupi wamechagua kufa.
Uwepo wao hao wanaoitwa magaidi tafsiri yake amani kwa Israeli haiwezi kuwepo maana magaidi Kila leo wanatafuta mbinu yakusurvive na kutimiza azma zao.
Duniani sio kila mtu ni mjinga kama sisi wengine tulivyoamua kuwa wajinga, Dunia zipo jamii au watu wasiokubali kunyanyaswa, inapofika suala la kunyanyaswa basi wao huchagua kifo.
Nyuma ya Israel kuna USA, UK na allies wengine wenye nguvu lakini nyuma ya masikini wa Palestina wamesimama wanyonge wasio na nguvu Iran, Hamas na Hizbollah lakini pamoja na unyonge wao wameamua kutochagua kupiga magoti au kuinama bali wamechagua kufia wanachokiamini.
Siku tukitaka balance of power, basi tuhakikishe Palestina wanakuwa na utawala wao, jeshi lao, na uhuru wakununua silaha, technolojia nk Kwa wakati wowote watakao kama Israeli, Iran pia asiwekewe vikwazo aachwe afanye anavyoona inafaa kama adui yake Israeli ili kuwe na balance of power halafu tuseme sasa Israeli kidume na sio style ya kuwafunga mikono wengine mikono na kumuacha Israeli atambe.