Miongoni mwa dhambi kubwa sana CCM wameitenda na Mungu atawaadhibu kwa hili ni kitendo chao cha kutomuambia ukweli Hayati Magufuli.
CCM ni kundi la watu wa motoni kabisa, wakiwa wanajua Mwenzao anapuyanga, na haki za watu kuishi zinadhurumiwa hadharani, wao waliamua kumsifia kwa kila jambo. Miongoni mwa watu wanaostahili adhabu ni Wazir wa viwanda katika utawala wa Hayati, akiwa anajua bado hakuna viwanda, huyu mtu aliamua kusimama hadharani na kuutangazia ulimwengu kuwa tuna viwanda zaid ya 100 kila wilaya...kibaya zaid akashangiliwa ndani ya Bunge tukufu.
Lala salama Magufuli, ulipata bahati mbaya sana ya kuishi na kundi la wanafiki na wewe ukashindwa kugundua mapema.
Mim siwezi kumlaumu Hayati hata kwa bahati mbaya kwakuwa hawezi kunijibu, ila hawa wahuni walioko hai Mungu aingilie kati tu kama aliyofanya kwa wale wa kabla yetu.