Hasira za Gen Z ya Kenya; Chanzo Chake ni Umaskini Uliotopea

Hivi Manzese na Mbagala unazionaje? Zile siyo slums kama za Nairobi
 
Naunga mkono hoja yako.
Angalau Tanzania kuna fursa kwa kada mbalimbali kutajirika tofauti na ilivyo Kenya.
Kenya ardhi yote imetwaliwa na watu wachache wenye uwezo, ni ngumu kwa jamii nyingine kupata chochote kupitia ardhi hiyo.
Tanzania ni jitihada zako ndizo zitakufanya uwe lofa milele au usogee hatua kadhaa mbele.
Kuna ardhi ipo ipo tu kuanzia Lindi mpaka Ruvuma, Itigi mpaka Tabora.
Kariua mpaka Uvinza.
Sikonge mpaka Mlele.
Hata kabla hatujafikiria kilichomo chini ya ardhi hiyo, kilimo tu kinaweza kubadilisha maisha ya watu wetu.
 
Usichukue slum kama kigezo tuu cha kutathmini umaskini, je Watanzania wengapi hapa Dar hawana hata pa kulala wanalala barabarani na kwenye vituo vya mabus.
Slam kwenye jiji kama Nairobi ni kielelezo cha kwanza kutambua umasikini wa nchi hiyo.
Nairobi au Dar ni kioo cha nchi.
Mji unapokuwa na makazi machafu wanayoishi masikini wa mji kama Kibera huwezi kukwepa ukweli wa umasikini wake.
Tuonyeshe eneo kama Kibera jijini Dar.

Suala la watu kulala vituo vya basi au sokoni ni hali ya kawaida kwenye miji mingi Duniani.
 
Wangapi wametajirika kupitia hizo fursa, mbona kila awamu watu wanarudi nyuma kua masikini acheni propaganda watanzania sie nimasikini wakutupwa gusa hizo aridhi kama utafungwa kwa kuvamia hifidhi za kiba za taifa........
 
Wangapi wametajirika kupitia hizo fursa, mbona kila awamu watu wanarudi nyuma kua masikini acheni propaganda watanzania sie nimasikini wakutupwa gusa hizo aridhi kama utafungwa kwa kuvamia hifidhi za kiba za taifa........
Nenda Njombe, Mafinga, Madibira, Makete, Wanging'ombe, Kapunga, ukaone vijana walivyowekeza kwenye kilimo cha parachichi, mpunga, Vitunguu nk.
Nenda Namtumbo, Madaba, Mbinga, Ukaone vijana wanavypiga pesa kwenye kilimo cha Nafaka kama Mahindi na Maharage.
Nenda Ifakara, Kisaki, Mbingu, Mang'ula, Mbigili nk ukajionee vijana waliojitoa wanavyopiga pesa kwenye kilimo cha mpunga.
Wewe kazi yako kuzurula na bahasha yako ya kaki mjini kutafuta ajira huwezi kuziona fursa hizo.
Endelea kulala, miaka 10 ijayo utaenda Njombe kuomba kazi kwa mkulima wa Parachichi
 
Umeliweka vizuri sana Mkuu. Watu wanasubiri kuwekewa hela mfukoni na Serikali. Hapo ndipo wanapotea
 
Hii ni kweli , Tz vijana wadogo wanapiga pesa kuliko huko kenya kumiliki ardhi ni ishu ....Kenya pesa ipo ila inatajirisha wanasiasa na wageni .
 
#Mama Samia mitano tena
Tanzania maisha ni mazuri sana
 
Umeliweka vizuri sana Mkuu. Watu wanasubiri kuwekewa hela mfukoni na Serikali. Hapo ndipo wanapotea
Wanaota ndoto, hakuna serikali itakuwekea pesa mfukoni kirahisi hivyo
Serikali inawezesha vijana wenye nia na malengo ya kuzalisha Mali.
Mwaka jana serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetoa fungu la pesa kwa vijana furani wa Makete ili walime ngano.
Hivi sasa vijana wapo kazini wanazalisha.
Hawa wengine wanataka kwanza waone shamba, trekta, nyumba nzuri na wapewe pesa mkononi ndiyo waende shamba.
Watasubiri sana.
 
Kama ni umasikini Tanzania ndo ingekua ya kwanza kuandamana, wewe angalia wadamanaji vijana wameva vizuri hata kupita waalimu wa Tanzania,
Hapana mkuu umasikini unakwenda mbali zaidi.

Wewe unafikiri maandamano ya CDM au vijana wa chuo kuna mtu huwa amevaa matambala ya deki??

Ukitafiti ni wasomi wangapi kila mwaka wanazaliwa kenya bila tumaini la maisha bora ndio ungejua kwanini juzi kiliwaka,tz bado bado wengi tuna katumaini dhaifu kamebakia.
Tunaendelea kuchochea kuni tutafika tu sehemu ambayo mtu akiongeza bei ya sukari kwa shiliki 100,moto unawaka,kwa saa hizi bado.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…