Nimekudharau sana bwana mdogo kwa kurubuniwa kizembe sana na kukubali kuingia mkenge wa kutua ndani ya bunge la Tanzania , umebugi sana !
Bunge la Tanzania halijawahi kusaidia mwanamichezo yeyote yule mahali popote nchini Tanzania , Matumla , Cheka walipigwa laana baada ya kukubali kuingia kwenye bunge lisilopenda michezo , labda nikunong'oneze hata huyu mkimbiaji Simbu kwa kuingia kwake bungeni kishajitia mkosi ambao hatakuja tena kunyakua medali hata ya kifuu cha nazi , jaribu kutafakari kabla ya kuamua , hivi ni nani aliyewahi kukujua kutoka ndani ya bunge la Tanzania , kwani ngumi umeanza jana ? hivi mnakuwa mmepofushwa vipi hadi kujipendekeza kwa watu wasiowajali hata chembe ?
Majuto ni mjukuu .