Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HASSAN NASRALLAH (1964 – 2024)
Hassan Nasrallah alipokuwa mtoto mdogo sana alikuwa akiwachekesha watu wazima nyumbani kwao.
Ilikuwa pakiadhiniwa na kisha pakakimiwa yeye atatoka mbio kukimbilia jikoni kwa bibi yake na akifika anamvua mtandio aliojitanda bibi yake kichwani na atakuja mbio ukumbini amepiga kilemba mtandio wa bibi yake na atasimama mbele ya safu anataka kusalisha.
Top
Wote watacheka.
Kumbe hii ilikuwa bishara kuwa mtoto Hassan Nasrallah atakapokuwa mkubwa atakuwa kiongozi shujaa na atapendwa sana watu wake na kuogopewa na maadui zake.
Mimi nilichelewa sana kumfahamu Hassan Nasrallah.
Nimekuja kumfahamu Hassan Nasralla kiasi cha miongo miwili iliyopita akiwa na miaka 39.
Kuanzia hapo nikawa nasoma kila kitu kuhusu yeye hadi leo nilipopokea taarifa ya kifo chake.
Hassan Nasrallah mwanae alikufa akiwa katika mapigano na Wayahudi.
Watu walifika nyumbani kwake kumpa pole kwa kifo cha mwanae.
Ilipofika zamu yake kuzungumza alisema maneno haya:
‘’Siku zote mimi nilipokuwa pamoja na nyie niliinamisha chini kichwa changu kwa kuwa nyie wote milikuwa mmetoa mashahidi watoto wenu waliokuwa wamekufa katika vita na Wayahudi.
Mimi sikuwa na mtoto aliyekufa shahidi.
Leo mimi nimetoa shahidi kwa hiyo na mimi kuanzia leo nitanyanyua kichwa changu juu kwa fahari sitojiinamia tena.‘’
Kulikuwa na dhana kuwa Wayahudi hawawezi kushindwa vita.
Vita iliyokuja kumaliza dhana hii ni vita vya mwaka wa 2006 kati ya Hizbullah wakiongozwa na Hassan Nasrallah na Wayahudi.
Vita vilipoanza fikra za wengi katika nchi za Kiarabu zilirejea katika Vita Vya Siku Sita vya mwaka wa 1967 na wengi waliamini kuwa Hizbullah watamalizwa kwa muda mfupi kwa kusagwasagwa na Israel.
Hili halikutokea.
Vita vilipiganwa kwa siku 34 katika mwezi wa Julai na Agosti hadi pale Umoja wa Mataifa ilipoingia kati na kuweka makubaliano ya kuweka silaha chini na kumaliza vita.
Wayahudi kwa mara ya kwanza katika historia ya mapambano yao na Waarabu walionekana katika stesheni nyingi kubwa za televisheni duniani wakirudi Israel kutoka uwanja wa mapambano wameinamisha chini vichwa vyao.
Israel ilikuwa kwa mara ya kwanza imeonja kipigo katika vita na Waarabu.
Hapakuwa na shamrashamra ziliyozoeleka za ushindi dhidi ya majeshi ya Kiarabu.
Hizbullah ilikuwa imevunja, ‘’myth,’’ ile fikra ya kuwa Wayahudi hawawezekani.
Hassan Nasrallah kiongozi wa Hizbullah alikuwa akiuliza wakati wa vita:
‘’Wako wapi askari wa Kiyahudi mbona hatuwaoni katika uwanja wa vita?
Tunachoshuhudia ni ndege za Kiyahudi wakipiga mabomu nyumba za raia.’’
Baada ya vita, ilipofika wakati wa kubadilishana mateka Wayahudi walipata fadhaa zaidi pale walipokuwa wao wanapokea majeneza ya askari wao waliouliwa vitani na Hizbullah na Israel ikiwaachia huru askari hai wa Hizbullah.
Kwa kifupi sana huyu ndiye Hassan Nasrallah kwa wale ambao hawakuwa wanamfahamu.