KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA KOSA LA UBAKAJI NA UDHALILISHAJI
ACP Debora Magiligimba RPC Ilala
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linamshikilia Said Hassan Said, 26, Askari Magereza, Mkazi wa Ukonga kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 29 (jina linahifadhiwa).
Mnamo tarehe 01/09/2021 majira ya saa tano nusu usiku katika barabara ya madafu Ukonga mtuhumiwa huyo ambaye ni askari wa Jeshi la Magereza mwenye namba B 9780 WDR Said Hassan akiwa na mwenzake ambaye bado hajakamatwa walimkamata kwa nguvu msichana huyo na kumuingiza kwenye gari dogo kisha kuondoka naye hadi kwenye nyumba moja iliyopo karibu na kambi ya KMKM Ukonga Magereza na kuanza kumbaka na kumlawiti kwa zamu.
Baada ya kumaliza kumbaka na kumlawiti watuhumiwa hao waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kumsababishia majeraha makubwa na maumivu makali katika sehehmu zake za siri.
Aidha, baada ya mtuhumiwa kugundua kuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tukio baya alilolifanya na mwenzake, mnamo tarehe 02/09/2021 alijaribu kujiua kwa kujinyonga na kuacha ujumbe wa maandishi kwa mkuu wake wa kazi na askari wenzake kuwa “mnisamehe bure kwa uamuzi wangu niliochukua kwa tukio nililolifanya nitaonekana nimekufa kizembe” lakini kabla hajafanikisha azma yake ya kujitoa uhai alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linaendelea na msako mkali kwa mtuhumiwa mwenzake aliyekimbia baada ya tukio hilo baya na linamtaka ajisalimishe haraka iwezekanavyo katika kituo chochote cha Polisi.
Imetolewa na:-
DEBORA D. MAGILIGIMBA-ACP
KAMANDA WA POLISI,
MKOA WA ILALA DAR ES SALAAM.
03/09/2021
Hapa huyu Dada akibeba SMG na kuwasaka askari magereza litaibuka libaba kubwajinga na kubwatuka 'huyu dada alikuwa ni gaidi alijifunzia kwenye danguro'
Achunguzwe kwanza alikuwa na mke, je alikuwa domo zege au masharti ya mganga..
Km alikuwa na mke na kabaka, akatwe kikojoleo chake. Kama ni domo zege, wamfunge mashine ya kukamulia maziwa iwe automatic haizimi mpaka ifikishe lita moja kudadadeki.
KAMA ni masharti ya mganga, akamatwe yeye na mganga wake, wakatwe vikojoleo vitengenezewe soseji, wale vikojoleo vyao, kisha wafungwe mawe wakatupwe mto kagera