Uchaguzi 2020 Hata CHADEMA wasiposhirikiana na ACT-Wazalendo, bado CCM itapigwa chini. Membe na Lissu “watakula vichwa vingi” vya wanachama wa CCM

Uchaguzi 2020 Hata CHADEMA wasiposhirikiana na ACT-Wazalendo, bado CCM itapigwa chini. Membe na Lissu “watakula vichwa vingi” vya wanachama wa CCM

Ndio muungane sasa ili mpate kula nyingi zaidi ili hata wakiiba ishindikane kufikia lengo
Hili nalo ni la muhimu. Unajuwa wanaweza kuwa na ushirikiano mzuri tu kama kweli wana nia ya kuiondoa ccm madarakani siasa za Taifa hili zibadilike moja kwa moja kwa uzuri lakini.
 
Hili nalo ni la muhimu. Unajuwa wanaweza kuwa na ushirikiano mzuri tu kama kweli wana nia ya kuiondoa ccm madarakani siasa za Taifa hili zibadilike moja kwa moja kwa uzuri lakini.
Ndio hivyo mkuu ila cha ajabu vyama vyote vya upinzani vimesha onyesha tamaa ya kuweka mgombea kutoka kwenye chama chao. Hii haitawasaidia
 
Ndio hivyo mkuu ila cha ajabu vyama vyote vya upinzani vimesha onyesha tamaa ya kuweka mgombea kutoka kwenye chama chao. Hii haitawasaidia
Hata wakiweka, lakini wakubaliane kushirikiana siyo mbaya. Kwasababu mimi ninaamini kabisa kuwa kura za upinzani zote kwa ujumla, zinazidi zile za ccm. Kwanza mwaka 2015, chadema walioata kura milioni 6 za mgombea wa urais.
 
Mkuu nilikaa kimya kuhusu haya mambo, naona umeamua 'kunichokoza''
Mkuu, kwanza, sina taarifa za Joka na ni muda sasa sijamuona jamvini, natumai yu bukheri aliko.

Pili, nianze na Zanzibar. Kama kuna fyongo iliyochezwa na CCM ni hii ya Hussein. Huyu bwana hakubaliki na kwamba aligombea ''nyumbani'' mkurunga kunamuondolea sifa ya ''uzanzibar'' hata kwa wana CCM a.k.a mapinduzi daima

Hii ilikuwa fursa ya Shamsa Vuai, lakini kamati maalumu Znz ilichezewa akili kwa kuaminishwa ni Mbarawa.
Hussein akaiangizwa katika kundi la Shamsi, Khalidi akisindikiza bila kujua huku bara ilikuwa Bw Hussein.

Kura za CCM 35 kutoka Znz zilikwenda kwa machaguo yao, huku mwana mpendwa akikomba 129 za Bara

Hili limepeleka ganzi visiwani, kwamba, CCM hawana uthubutu wa kunyanyua nyuso, wameuza ''ghala la silaha''. Zanzibar hakuna raha kwa CCM.

Wale wa Maalimu Seif alipo wapo, wakipata CCM kidogo tu hata mbinu ya kupunguza majimbo haifanyi kazi

Tegemeo la CCM Zanzibar ni moja , kupitia sera za 'Jecharism'' .
Tatizo la sera hiyo ni moja, umma ukiamua basi maji yatazidi unga kama si tui kuingia maji.
Shah wa Iran na Nicole Ceuasescu wa Romani wanatambua somo la nguvu ya umma vizuri.

Kuhusu Bara, kuna tatizo kubwa sana. Baada ya Lowassa na Sumaye wengi wanawaangalia wahamiaji kwa jicho la shaka sana.

Ni kwa msingi huo Chadema hawafikirii kurudia makosa yaliyowagharimu muda mwingi sana.
Mwaka 2015 CDM walitumia muda mwingi kwa mtu, kitu ambacho kingewapa wabunge wengi.

Kwa upande wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amekomaa na nia yake si uongozi kama yeye bali uongozi wa kuiondoa CCM kwanza. Mtazamo huu umemfanya awe 'muumini' mzuri wa ushirika kwa Wapinzani.

Zitto amegundua tatizo si yeye kuwa kiongozi bali yeye na wenzake kuongoza kuiondoa CCM.
Hii ni ''maturity'' nzuri sana na nampa big up

Pamoja na hayo, kumpokea Membe kuna maswali kama yale tuliyouliza wakati wa Lowassa.
Je, uwekezaji kwa Membe kuna manufaa? Je, kwanini ajiunge dakika za mwisho?
Lengo ni kugombea au kuamini katika demokrasia?

Je, akiwa Kachero anaweza kuleta mabadiliko gani tofauti na yale ya Waziri mkuu Lowassa?
Membe ana dhima ya kuwahahikishia Wapinzani, ana kitu tofauti vinginevyo itakuwa hadithi ile ile.

Kwa upande mwingine najiuliza sana, nini mkakati wa Wapinzani? Suala hapa si kushinda, wana uwezo huo.

Tatizo ni mfumo uliosukwa ambao sasa unahusisha vyombo vingi. Chaguzi zote za marudio zinathibitisha

Hivi Mkurugenzi anakimbia vipi ofisini kupokea fomu na hakuna kinachotokea kwa kosa hilo?

Hivi hatuoni Polisi wakikamata Wapinzani wakati CCM wakisaidiwa na Magereza kupandisha bendera.

Msajili yupo kimya kama vile ofisi yake ipo likizo, huku tume ya uchaguzi na nakala za matokeo ikifanya yake.

Wengi wanadhani Takukuru kuwakamata CCM ni kupambana na rushwa.

Siku kibao kitakapogeuka Wapinzani ''watakamatwa siku moja kabla ya kurudisha fomu''.

Wakurugenzi wataugua masaa machache kabla ya kurudisha fomu.

Mwaka huu CCM itashinda majimbo zaidi ya 50 bila kupingwa kwa namna. Haya hayajulikani?

Kukokesekana kwa tume huru na kushindwa kuidai ni kosa kubwa sana kwa wapinzani

Uchaguzi wa Afrika hauamuliwi na namba bali namna, na ni kwa wale tu wanaoweza kama Malawi , matokeo mengine hayatakuwa tofauti na zama zile
Mkuu ahsante kwa nondo ya moto.
Huu ni uchambuzi mahiri ambao unazungumzia hali halisi ya uchaguzi ujao na madhaifu yake kwa pande zote, pia tutegemee nini kama mapungufu hayo yataachwa kama yalivyo bila kurekebishwa.

Mchango wako umenikumbusha enzi za JF ya GT waliobobea. Big up!
 
Lazima mkuu! Kama kukiwepo na dalili kidogo tu za uchaguzi huru, siyo siri ccm itameguka kabla hata ya uchaguzi mkuu. Wait and see!
Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa,umeifanya Jumuiya ya Kimataifa iitolee macho TZ,
Madhila aliyofanyiwa TL ya kupigwa risasi, bila uchunguzi Wala kuwatafuta waliotaka kumuua yameifanya Jumuiya ya kimataifa yatamani kuja kushuhudia Uchaguzi na hasa TL ikigombea,
Mateso ya wapinzani ya Mara kwa Mara yanaifanya Jumuiya ya Kimataifa kutaka kuja kushuhudia uchaguzi,
Utekaji,upigaji na kupotezwa kwa baadhi ya wananchi,waandishi na wanasiasa Ni mambo mageni yanayowavutia jumiya ya Kimataifa kuona Hali ikitendeka katika Uchaguzi wa mwaka huu.
Wafanyakazi,wakulima na wafanyakazi wa nchi hii wamepitia wakati mgumu kuliko wakati wowote ule tangu nchi hii ipate uhuru.
WanaCCM hawana Raha,wapinzani hawana raha,wawekezaji hawana Raha,wanasiasa hawana Raha na hata VIONGOZi wa Dini hawana Raha.
Mabalozi wa nchi wahisani ambao kwa Sasa wanaitwa Mabebebru wameshatoa matamko juu ya Uchaguzi huru.
Uchaguzi wa mwaka huu utakua wa kipekee zaidi.
Tutegemee CNN,BBC, ALJAZEERA,nk. kuweka kambi hapa.
 
Tusubiri tuone hicho "kipigo kitakatifu" kamanda. Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo.
Wewe si unafurahia tume hii iliyopo? That is what you’re banking on, not a free and fair election.
 
Wanajamvi,

Kama heading ya uzi huu inavyojieleza, ni kwamba hakuna haja ya upinzani ku panic kabisa! Hayo ni ya wana ccm kuyafanya, na kamwe siyo upinzani. Wao ccm, kwani wamezuiwa kufanya siasa? Wamekuwa wakifanya kampeni toka awamu hii iingie madarakani. Wakati vyama vingine vikizuiwa kufanya hata vikao vya ndani! Sasahivi, wananchi kama ni kuona na kusikia, basi wameshasikia na kuona vya kutosha kupitia kwa wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, mameneja wa miradi, makatibu uenezi na katibu mkuu wa ccm, ndo wamekuwa wakitamba siyo tu kwenye vyombo vya habari vya binafsi ambavyo viliingiwa na hofu na woga, haswa baada ya tukio ka clouds media pale studio walipovamiwa na kikosi kazi maalum na kunaswa kwenye camera live! Lakini hata Tv yetu ya Taifa TBC, ambayo inaendeshwa kwa kodi zetu wote bila kujali vyama vyetu, wala itikadi zetu, imekuwa ni kama chombo cha propaganda cha ccm. Kwahiyo wao ccm ndo wanaotakiwa kupanic maana wanarudia yale yale ambayo wananchi wamelazimika baada ya kulazimishwa, wameshayaona na kuyasikia kwa miaka minne mfululizo!

Ni wazi sauti nyingine zikija na kumwaga sera zao na kuonyesha madhaifu yaliyopo kwa utawala huu wa ccm, basi watakuwa na shauku kubwa ya kuwasikia bila chembe ya shaka! Hiyo ni kawaida kwa hulka ya mwanadamu. Ni kiumbe mwenye kutafuta habari kila uchao! It is a human psychology. Tunataka tusikie pande zote, kisha tuchague!

Sasa nimeona watu wanasumbuka sana kuhusiana na suala la nani atakuwa mgombea kwa upande wa upinzani. Vyama vya ACT-Wazalendo, pamoja na kile chama kikuu cha upinzani nchini, yani CHADEMA vikizungumziwa na kuhusishwa na wagombea wawili maarufu sana, yani Tundu Antipas Lissu, sambamba na Bernard Membe, ambaye inasemekana yumo ACT-Wazalendo.

yangu rahisi ya ki “layman”, inaonyesha wazi kabisa kuwa ACT-Wazalendo, ni chama mbadala cha CUF. Na ndiyo kinategemewa kumsimamisha mgombea kule Zanzibar. Na kama sikosei, mgombea huyo ni Maalim Seif Sharif Hamad. Kwahiyo kwa upande huo wa kushirikiana inapokuja kwa upande wa Zanzibar, ni suala la kawaida tu na ni utamaduni ulio kuwepo wa kushirikiana. Na ndiyo maana halitabadilika, kwasababu ACT-Wazalendo wameisha wafuta CUF.

Na kwa upande wa bara, mambo yalikuwa ni kati ya Lipumba, na mgombea wa CHADEMA, ambapo CHADEMA walikuwa ndo wanaotoa mgombea wa urais kwa upande wa bara. Last time Lowassa, kabla ya hapo Slaa nk.

Lakini tofauti iliyoko kwa sasa, ni Bernard Kamilius Membe. Huyu yeye ndiye anayeleta mjadala mkali. Ni mjadala ambao unachochewa sana na wana ccm wenyewe! Nadhani kisaikolojia, ni umbea kwasababu yao wenyewe, yamewashinda! Wanatafuta wa kujifananisha nao nje ya chama, na wakati wenzao bado wako kwenye utaratibu wa kupata wagombea urais. Lakini kwasababu ccm wao wameshamaliza upande wao, na watu kunyimwa hata nafasi ya kuchukuwa fomu za kugombea kwenye nafasi ya urais, yani fomu zikafichwa na katibu mkuu akasema wazi kabisa kuwa hawatatoa fomu kwa mtia nia mwingine yoyote yule zaidi ya mwenyekiti aliyeko! Na ndiyo matokeo yake Bernard Membe kujitoa. Huyu tayari ana watu wengi tu ndani ya ccm wanaoona ameonewa na ccm. Jambo lilokuwa ni kinyume hata na katiba yao ya chama. Pia woga unaonyesha udhaifu mkubwa! Hata JK mwenyewe tuliyemuita “dhaifu”, yeye alikubali kina Shibuda wakajitosa na kuchukuwa fomu! Woga wa sasa, unaonyesha kutokukubalika ndani ya chama!

Kwa maoni yangu, hata kama vyama hivi vikiamuwa kuwasimamisha wagombea wao, bado idadi ya kura watakazozipata, zitawazidi ccm. Huu ni ukweli mchungu kwa ccm na ndiyo maana wanahaha sana kuleta mijadala ya kuwachanganya na kutaka kuleta migawanyiko! Lakini hili halitafanya kazi wala kufanikiwa, maana siku ya kufa nyani, miti yote huteleza! Kwanza kuna kura nyingi sana za wana ccm ambao hawakuona umuhimu wa Lissu kutaka kuuwawa! Kura za huruma, ama “sympathy”, na sisi waafrika, siyo tu kwamba tuna sifa hizo, bali pia wengi wana sifa ya “empathy”, ambapo ni “uwezo wa kujiweka kwenye nafasi ya mtu mwingine”.

Na hata matendo ya serikali na bunge kupitia kwa spika Ndugai, yameonyesha wazi kabisa, wananchi wanajuwa kwasababu kwa miaka hiyo minne, wamekuwa wakilishwa propaganda za upande mmoja!, na sasa mahakama nayo inaweza kutupiwa macho pamoja na polisi. Bunge lilishafanya kazi yake kwa wale “wasumbufu”, mara baada ya kusitishwa kurushwa mubashara! Na kweli wengi wameshighulikiwa nje ya bunge! Wengine kutishwa na wengine inasemekana “kununuliwa”

Kule Kenya, hili liliwahi kutokea pia, na ndipo hapo chama cha KANU kilipoanguka chali! Kama sikosei, mara ya pili, ilibidi upinzani wafanye muungano, kwasababu mara ya kwanza, kura zao zote, ziliwashinda KANU, lakini wao walikuwa hawajaungana, na hivyo KANU kubakia madarakani. Sisi hapo tunaweza kurekebisha.

Kwa upande wa Tanzania, siasa zetu ni za tofauti kidogo na zile za Taifa la Kenya. Sisi kwanza siasa za ukabila siyo kivile hata kidogo! Pamoja na kwamba ccm wamejitahidi sana kuzitumia dhidi ya upinzani, Lakini hazijafanikiwa, na ndiyo maana upinzani ulipata nguvu na kuongeza wabunge wengi, pamoja na madiwani!, na umaarufu mkubwa, sana hadi ccm kutishika! Na hata wengine wakisema uchaguzi uliopita, kama siyo kwa “goli la mkono”, ambalo Nape, January pamoja na Kinana, walifanya kazi ya ziada, basi leo hii ccm ingekuwa ndo upinzani.

Sasa miaka mitano ndo hiyo imeshakata, Kinana ni juzi tu kaomba msamaha, ni baada ya Nape na January kufanya hivyo! Lakini nao walifanya kwa shingo upande tu. Kwasababu, nguvu za mwenyekiti ni kubwa mnoo, na pia mara baada ya kuingia, alifanya mabadiliko ambayo wengi waliyaona ni kama dalili za kuji “dhatiti” zaidi ndani ya chama! Na ukizingatia yeye ndo mkuu wa serikali, wengi wanasikilizia kupata nafasi, huku wengine wa “jalalani”, nao wakipiga jaramba! Lakini pia, ni wazi kuwa hao kina Nape na January, wamekulia humo ccm, hivyo hawana ujanja, siasa ndo maisha yao! Na hivyo wamekuwa kama “mateka” wa kifikra na hata kimwili! Wakitoka ccm, wanajuwa hawana lao tena! Kwasababu wanafahamu raha za kubakia humo! Wanafahamu kwa mfumo uliopo, mathalan tume ya uchaguzi, ni vigumu kuwatoa ccm madarakani! Hao nao sura zao halisi zingeonekana kama wengine wangeruhusiwa kuchukuwa fomu ya kugombea urais ndani ya ccm. Hata mzee Makamba naye ni hivyo hivyo tu, wengi tulimsikia kwenye zile tape walizodukuliwa wakati wakimsema mwenyekiti wao! Mzee Mkapa yeye hata kama alidukuliwa, hawakutuhubutu kuweka wazi kama hao wengine, lakini naye alizungumzia umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi nchini! Hilo tu, linaonyesha wazi kabisa kuwa wenye busara, wanatambuwa hitaji kuu la wananchi na Taifa kwa sasa! Siyo kauli ya bahati mbaya tu.

Kura za ccm ndizo zitakazogawanywa, cha msingi, kuwepo na makubaliano baina ya wapinzani mapema iwezekanavyo! Ninayo imani kwamba, uchaguzi huu, kama haki na ushauri na maoni yakizingatiwa, walau kwa kuanzia na mabadiliko kwenye uchaguzi, kuelekea kwenye katiba mpya na tume huru, basi utatuletea viongozi wanaowakilisha kada zote za wananchi pamoja na masilahi yao! Yale ya moja kwa moja kwenye jamii, na pia yale ya watanzania wote kwa ujumla! Hili amelizungumzia vyema sana Sheick Ponda kwenye ule waraka wa “Shura ya Maimamu”, ambapo walizungumzia kuhusu upatikanaji wa katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu! Lakini pia umuhimu wa kuweka kanuni za kipindi cha mpito, ili tupate serikali itakayotuongoza kuelekea kwenye katiba mpya ya wananchi kutoka kwa wananchi.

Hapa ina maana kwamba kuna mengi yanayowaunganisha watanzania dhidi ya ccm kuliko yale yanayowatenganisha! Hayo ya kututenganisha, ni machache sana ambayo siyo lazima kupewa kipaumbele! Maana yenyewe ni ya kuwagawanya wapinzani ili kuwadhibiti! Kuwagawanya watanzania, ili kuwaondolea sauti na umoja wa kudai haki, uhuru na maendeleo ya nchi! Yani “devide and rule”. Kwetu ni tofauti kabisa na kule Kenya ambapo siasa za ukabila ndizo zinawaumbuwa na zimekuwa zikifanya hivyo kwa muda mrefu.

“Coalitions”, ama miungano yao, ni ya misingi ya kikabila. Mfano Kaleinjin na Wakikuyu, Vs Waluo na makabila mengine madogo nk. Na Kwahiyo sisi tuna nafasi nzuri zaidi kwa wapinzani kuiangusha ccm, na bado tukapata serikali iliyopatikana kutokana na ridhaa ya wananchi...serikali itakayowatumikia wananchi vyema, na kwa mujibu wa katiba ya nchi! Na hao wakifanya uzembe, tuwe na nafasi na uwezo wa kuwandoa madarakani kwa kupitia sanduku la kura kwa mujibu wa katiba.

Siyo siri, chama cha CUF, kilikuwa na wanachama wengi wa maeneo ya mwambao wa Pwani! Na hivyo wengi kuwa waislam. Majimbo mengi ya waislam, ni hao CUF waliyabeba, lakini mengine machache, ccm wamekuwa wakitumia ujinga na umasikini kuendelea ku watawala. Mifano mingi ipo hai! Ni tofauti na baadhi ya sehemu na mikoa ambako wameshaifuta kabisa ccm kwenye misamiati yao. Hata hivyo, kama nilivyosema hapo awali, ACT-Wazalendo ndiyo ambao sasa wameichukuwa nafasi hiyo ya chama cha CUF. “CUF has simply been replaced”, haswa baada ya Maalim Seif kuondoka huko, na Zitto kuitumia nafasi hiyo kumsajili.

Sasa endapo ACT-Wazalendo watamsimamisha Membe, nadhani siyo mbaya hata kidogo kwa upande wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla!Kwanza kuna malalamiko mengi sana ya uwepo wa udini. Malalamiko ambayo yanaelekezwa kwa utawa wa ccm! Na wala siyo mara ya kwanza! Na ndiyo maana hata CUF ilipata nguvu sana! Malalamiko yao hayajaanza leo chini ya utawala wa ccm! Hawa watu sauti zao lazima zitakuwa zinataka mwakilishi. Hata waislam wale ambao walikuwa hawaipigii CUF kura, na wakawa wanaipigia ccm, basi sasa wataipigia kura ACT-Wazalendo.

Hata wale ccm wasioipenda CHADEMA baada ya kulishwa sumu mbaya na chama chao, wataipigia kura ACT-Wazalendo kumfuata Membe...Maana tunafahamu propaganda za ccm inapokuja kwenye udini na ukabila! Na kujidai kwamba wao siyo mafisadi! Tuhuma zao wenyewe, lakini wamekuwa wakiwasingizia upinzani. Sasa ccm mmetawala toka uhuru, upinzani ndo umeleta shida za waislam toka lini? Ufisadi umeanza wapi? Kauli ya “kujivua gamba”, ilikuwaje? Hili huwa najiuliza sana wakati ccm inapokuja na mgombea wao huku wakitutajia maendeleo waliyoyaleta, na kujifananisha na upinzani ambao hawajawahi kuongoza nchi. Mbona hawakubaliani na ukweli pia hata umasikini na unyonge ni wao waliowasababishia watanzania? Hili lenyewe, lilitakiwa liwe kama nguzo ya sababu nzuri kabisa ya kuwa na uchaguzi huru tuone kama hawajaondolewa madarajani! Maana nani mwingine ambaye ameshafanya “mazuri” zaidi yao tokea December 31st 1961? Nani mwingine ameshawahi kufanya “mabaya” zaidi ya ccm kwenye taifa letu?

Hivyo kwa maoni yangu, ni kweli kabisa kuwa uchaguzi wa huru na haki, utawaondoa ccm madarakani, upinzani uungane, ama usiungane, moto ni ule ule! Membe atakula vichwa vya wana ccm, chadema nao watakula vichwa vya wana ccm. Hata yule Sipunda anaweza kula vichwa!

Cha msingi, ni makubaliano yafanyike mapema! Makubaliano ambayo yatahusisha nia ya dhati kabisa ya pande zote mbili! Nia za kuwa na tume huru ya uchaguzi pamoja na katiba mpya ya wananchi kutoka kwa wananchi! Na siyo hii ya mkoloni yenye viraka vya ccm, ambayo inaendelea kutushikia chini kiasi cha kwamba uhuru wetu ukawa mashakani! Waliotufanya wanyonge, ndo hao hao wanaoendelea kuutetea unyonge wetu ili tubakie nao eti na kuendelea kuwachaguwa na kukatazwa kuhoji lolote kuhusu raslimali zao! Unyonge wa watanzania ndiyo sababu kubwa ya wao ccm kuendelea kuwepo madarakani pamoja na umasikini wetu.

Sababu ziko nyingi sana, ila nimeamuwa kuanzia na hizi!

cc Nguruvi3
****Maoni ya Nguruvi3

“Mkuu nilikaa kimya kuhusu haya mambo, naona umeamua 'kunichokoza''
Mkuu, kwanza, sina taarifa za Joka na ni muda sasa sijamuona jamvini, natumai yu bukheri aliko.

Pili, nianze na Zanzibar. Kama kuna fyongo iliyochezwa na CCM ni hii ya Hussein. Huyu bwana hakubaliki na kwamba aligombea ''nyumbani'' mkurunga kunamuondolea sifa ya ''uzanzibar'' hata kwa wana CCM a.k.a mapinduzi daima

Hii ilikuwa fursa ya Shamsa Vuai, lakini kamati maalumu Znz ilichezewa akili kwa kuaminishwa ni Mbarawa.
Hussein akaiangizwa katika kundi la Shamsi, Khalidi akisindikiza bila kujua huku bara ilikuwa Bw Hussein.

Kura za CCM 35 kutoka Znz zilikwenda kwa machaguo yao, huku mwana mpendwa akikomba 129 za Bara

Hili limepeleka ganzi visiwani, kwamba, CCM hawana uthubutu wa kunyanyua nyuso, wameuza ''ghala la silaha''. Zanzibar hakuna raha kwa CCM.

Wale wa Maalimu Seif alipo wapo, wakipata CCM kidogo tu hata mbinu ya kupunguza majimbo haifanyi kazi

Tegemeo la CCM Zanzibar ni moja , kupitia sera za 'Jecharism'' .
Tatizo la sera hiyo ni moja, umma ukiamua basi maji yatazidi unga kama si tui kuingia maji.
Shah wa Iran na Nicole Ceuasescu wa Romani wanatambua somo la nguvu ya umma vizuri.

Kuhusu Bara, kuna tatizo kubwa sana. Baada ya Lowassa na Sumaye wengi wanawaangalia wahamiaji kwa jicho la shaka sana.

Ni kwa msingi huo Chadema hawafikirii kurudia makosa yaliyowagharimu muda mwingi sana.
Mwaka 2015 CDM walitumia muda mwingi kwa mtu, kitu ambacho kingewapa wabunge wengi.

Kwa upande wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amekomaa na nia yake si uongozi kama yeye bali uongozi wa kuiondoa CCM kwanza. Mtazamo huu umemfanya awe 'muumini' mzuri wa ushirika kwa Wapinzani.

Zitto amegundua tatizo si yeye kuwa kiongozi bali yeye na wenzake kuongoza kuiondoa CCM.
Hii ni ''maturity'' nzuri sana na nampa big up

Pamoja na hayo, kumpokea Membe kuna maswali kama yale tuliyouliza wakati wa Lowassa.
Je, uwekezaji kwa Membe kuna manufaa? Je, kwanini ajiunge dakika za mwisho?
Lengo ni kugombea au kuamini katika demokrasia?

Je, akiwa Kachero anaweza kuleta mabadiliko gani tofauti na yale ya Waziri mkuu Lowassa?
Membe ana dhima ya kuwahahikishia Wapinzani, ana kitu tofauti vinginevyo itakuwa hadithi ile ile.

Kwa upande mwingine najiuliza sana, nini mkakati wa Wapinzani? Suala hapa si kushinda, wana uwezo huo.

Tatizo ni mfumo uliosukwa ambao sasa unahusisha vyombo vingi. Chaguzi zote za marudio zinathibitisha

Hivi Mkurugenzi anakimbia vipi ofisini kupokea fomu na hakuna kinachotokea kwa kosa hilo?

Hivi hatuoni Polisi wakikamata Wapinzani wakati CCM wakisaidiwa na Magereza kupandisha bendera.

Msajili yupo kimya kama vile ofisi yake ipo likizo, huku tume ya uchaguzi na nakala za matokeo ikifanya yake.

Wengi wanadhani Takukuru kuwakamata CCM ni kupambana na rushwa.

Siku kibao kitakapogeuka Wapinzani ''watakamatwa siku moja kabla ya kurudisha fomu''.

Wakurugenzi wataugua masaa machache kabla ya kurudisha fomu.

Mwaka huu CCM itashinda majimbo zaidi ya 50 bila kupingwa kwa namna. Haya hayajulikani?

Kukokesekana kwa tume huru na kushindwa kuidai ni kosa kubwa sana kwa wapinzani

Uchaguzi wa Afrika hauamuliwi na namba bali namna, na ni kwa wale tu wanaoweza kama Malawi , matokeo mengine hayatakuwa tofauti na zama zile”- Nguruvi3

Mkuu hebu weka hesabu hapa jinsi ACT na Chadema watakavyo ishinda CCM? Hivo kweli ACT waweke mgombea na Chadema waweke mgombea na CCM waweke mgombea halafu nani atakuwa mshindi?
Hebu bwana Mushi hebu nipe Hesabu jinsi Sisiemu watakavyo angushwa!
 
Hivi unadhani anapoongea hivyo ndo kwamba anataka tume huru? Hapo anatisha tu watu kuwa tume siyo huru, na kwamba usalama na wanajeshi ndo wanahakikisha kuwa ccm wanashinda. Na huyu ni mwana ccm humu nguli! Ambaye hadhani kwamba tume huru ni jambo la maana.

Sasa wewe labda ndo mtoto, maana haumfahamu huyu member kama mimi humu ndani. Kama na wewe ni ccm, wote ni kundi moja la akili za kitoto.
jmushi ;
Saharavoice kaangalia uhalisia siwezi kumlaumu ila mtungi upasukia mlangoni!
Mama akijiamini mtungi umefika anajikwaa kidogo tuu biashara imekwisha.
Kujiamini kwingi ni weakness!!
 
Hivi unadhani anapoongea hivyo ndo kwamba anataka tume huru? Hapo anatisha tu watu kuwa tume siyo huru, na kwamba usalama na wanajeshi ndo wanahakikisha kuwa ccm wanashinda. Na huyu ni mwana ccm humu nguli! Ambaye hadhani kwamba tume huru ni jambo la maana.

Sasa wewe labda ndo mtoto, maana haumfahamu huyu member kama mimi humu ndani. Kama na wewe ni ccm, wote ni kundi moja la akili za kitoto.
Tufanye mtashinda uchaguzi mwaka huu bila tume huru. Hongereni sana
 
Hivi wananchi waichague chadema kwa lipi hasa? kile chama kinasubiri kuzikwa tu October 2020
 
Back
Top Bottom