Nchi ya Tanzania ni ya Watanzania wote. Mtu kuikimbia nchi yake kwa kuhofia kuuawa kisa kuwa na mawazo tofauti na watawala, sababu ya uongozi na siasa chafu, ni aibu ya nchi husika. Alichokifanya Mh. Samia kilisaidia kumjenga kisiasa zaidi. Hii ni kama ilivyotokea wakati wa utawala wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Salmin Amour, alitesa wapinzani mpaka kuwazushia kesi ya uhaini. Kesi ambayo hata mwanasheria wake mkuu aliiponda, na Salmin akashupaza shingo na kumtimua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Alipomaliza muda wake, aliingia Aman Karume akaifutilia mbali kesi hiyo, sifa zote zikaenda kwake Mh. Karume.
Nahitimisha kwa kusema Rais ni raia kama raia wengine. Kinachomtofautisha ni ulinzi na matumizi ya vyombo vya Dola ambavyo kwa udhaifu wa katiba yetu wakati mwingine vinajikuta vinatumika kiasiasa.
Haiwezekani kulinganisha tabia za Wakenya na Tanzania. Siasa za Kenya bado zinakabiliwa na wingu la ukabila na vurugu kutokana na asili yao.
Issue hii ya bandari imepewa nguvu kutokana na ubabe na unafiki wa bunge letu na baadhi ya viongozi wa CCM na mawakala wao.
Unakuta mtu kama Rostam Aziz akiitetea Serikali, mtu aliyetamka wazi amejiondoa kwenye siasa. Wakati anajiuzuru ubunge, leo amejitosa kuitetea Serikali kwenye mkataba wa bandari.
Ipo shida gani kuzijibu hoja kwa ustaarabu zilizoibuliwa? Hukumu ya Mbeya, majaji wanasema bunge halihusiki na makubaliano. Kinachokwenda bungeni ni mkataba. Huoni hii ni aibu kiasi hata kama mahakama imesema haioni shida kwenye mkataba, lakini imeasaidia kuonyesha nia ovu kwenye huu mkataba. Mahakama inashangaa kipengele kinachozuia mahakama zetu kushughulikia migogoro kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya maliasili ya 2017. Bado huoni kuna shida mahali? Tunaheshimu maamuzi ya mahakama, japo hatuamini uwezo wao kwenye kesi zinazoihusu Serikali. Siyo ajabu mahakama ya rufaa ilisita kutoa uamuzi kwenye kesi ya mgombea mwenza (Rev. ,Mtikila), tena ikiwa full benchi majaji saba wakiongozwa na Jaji Mkuu Augustine Ramadhani (RIP), mpaka kuwaalika marafiki wa mahakama Pro.. Kabudi na Prof. Mwaikusa (RIP) mwishoni. Uamuzi eti ni kesi ya kisiasa, hoja ipelekwe bungeni. Ni mahakama ya Afrika ndiyo ilimpa ushindi Mtikila japo alikuwa ameshakufa.