Hata kama mkeo na watoto unawapenda usisafiri nao kwenye gari moja; wahenga waliishi muda mrefu kwa kukwepa haya

Hata kama mkeo na watoto unawapenda usisafiri nao kwenye gari moja; wahenga waliishi muda mrefu kwa kukwepa haya

Haya mawazo ya ufukara wa akili. Mawazo ya kuamini miujiza na ushirikina. Hoja ya mkleta mada ipo sahihi lakini umeamua kuleta ushirikina wako bila sababu.
Hili lizingatiwe sana dunia hii haiko fair watu wanawindana kama Simba na swala. Safari yako usiage sana watu wasio wa muhimu INASAIDIA.
 
Treni ni salama zaidi kwa familia,barabara zetu siyo salama kabisa,ni nyembamba,leseni za udereva kutolewa kiholela.Wewe unaweza kuwa dereva mzuri lakini dereva mwenzako siyo makini anahama njia anakufuata.Treni ni bora sana kwa mikoa yenye mtandao wa reli.
 
Wazee wa zamani waliona mbali sana kifikra kuhusu maisha. Awakuruhusu watoto wao watumie chombo kimoja cha usafiri, wakae pamoja au kuambatana mara kwa mara; waliogopa kuteketeza familia at once.

Leo hii imekuwa fashion kwa ndugu kusafiri pamoja, tunapotumia chombo kimoja cha usafiri upo uwezekano mkapotea kwa pamoja. Chukueni taadhari; kawia ufike.

Poleni wote mliowahi kupoteza ndugu kwenye ajali au majanga ambayo endapo tungetenganisha wana familia may be baadhi wangekuwa hai leo
Hii si kweli, mr. Mutabingwa alitoka Uganda na familia yake ya watoto wawili na mkewe wakaingia Tanganyika wakapita Morogoro kwenye mashamba ya mkonge kisha wakaenda kwenye milima ya Usambara, wakaelekea Kilimanjaro kando ya mlima Kilimanjaro. Mr. Mutabingwa akavuka mpaka na kuingia Kenya akavuka mstari wa Ikweta Nairobi kisha akaingia Uganda kupitia maporomoko ya mto Naili(Nile) na wakafika salama nyumbani kwao.
 
Wazee wa zamani waliona mbali sana kifikra kuhusu maisha. Awakuruhusu watoto wao watumie chombo kimoja cha usafiri, wakae pamoja au kuambatana mara kwa mara; waliogopa kuteketeza familia at once.

Leo hii imekuwa fashion kwa ndugu kusafiri pamoja, tunapotumia chombo kimoja cha usafiri upo uwezekano mkapotea kwa pamoja. Chukueni taadhari; kawia ufike.

Poleni wote mliowahi kupoteza ndugu kwenye ajali au majanga ambayo endapo tungetenganisha wana familia may be baadhi wangekuwa hai leo
hao wazee wako wa zamani walikuwa wanatumia usafiri gani
 
Maisha ya mwanadamu ni fumbo kubwa sana. Mtu anaboast kazaa watoto wanne, watano, sita..lakini kifo sasa..kinakuja kinawafagia wote. Mungu tupe kuhesabu siku zetu zilizobaki hapa duniani.
 
penye uwezekano lifanyike, umakini barabarani kama ni usafiri binafsi ni MUHIMU. Uzoefu barabarani na kukumbushana ni MUHIMU. Tatizo gari za AUTOMATIC kila mtu anaona anaweza kuendesha mwendo mrefu.

Mambo ya vinywaji vikali safarini ni SUMU. safari za jioni ni HATARI !! jiulize mchana kutwa ULIKUWA UNAFANYA NN? mwili umechoka kiasi GANI?

Wengine mlikuwa mmepumzika majumbani kwenu /hotelini , je ? Dereva wenu yy amepata mapumziko?
 
Sema tu haya mambo huwa yanatokea lakini pia kuna mazingira yanalazimisha mpande gari moja hakuna namna. Hebu fikria mmepata msiba na wote mnahitajika kuwepo gari private ipo moja hapo mnafanyaje? Mnataka kwenda kanisani hapo hapo mjini mtawezaje kujitenga? Na wakati huo ajali hazichagui hata kama uko mjini kwako inatokea tu! Yote huwa tunamwachia Mungu!
 
Wazee wa zamani waliona mbali sana kifikra kuhusu maisha. Awakuruhusu watoto wao watumie chombo kimoja cha usafiri, wakae pamoja au kuambatana mara kwa mara; waliogopa kuteketeza familia at once.

Leo hii imekuwa fashion kwa ndugu kusafiri pamoja, tunapotumia chombo kimoja cha usafiri upo uwezekano mkapotea kwa pamoja. Chukueni taadhari; kawia ufike.

Poleni wote mliowahi kupoteza ndugu kwenye ajali au majanga ambayo endapo tungetenganisha wana familia may be baadhi wangekuwa hai leo

Mkuu Resilience,

Naomba kwenda kinyume na hoja yako, Mzee wangu kishatangulia mbele ya haki akiwa na kama miaka 87, alianza kutubeba ndani ya Volkswagen (Beatle) TDQ.....Tukiwa wadogo, mimi na dada zangu wawili, na Mama na mzee mwenyewe toka Moshi hadi Mbeya! Na kipindi hicho barabara ni mbaya na sehemu kubwa ni ya vumbi! Tumefanya hizo safari mara nyingi mno!

Mzee wangu akiwa ni kibosile wa serikali, mara nyingi mno alipenda kutumia gari yake ya binafsi, na hata ya ofisini akiendesha mwenyewe. Hivyo mkuu tumezunguka zunguka Tanzania mno, kama familia, na mojawapo ya kumbukumbu tamu ni safari za familia na ndugu zangu, ilisaidia sana kutu bond pamoja.

Na kwa upande wangu na hata kwa dada zangu, ni watu wa kusafiri na familia mno! Dada zangu huko walikoolewa. mmoja Songea na Mwingine Musoma, mara nyingi wanakwenda Ukweni wakienda toka Dar, na huwa naona ni dereva wazuri kuliko shemeji zangu!

Ukweli ajali haina kinga! Lakini Mzee wangu alitupa tips nyingi mno za kuendesha gari kwa usalama (Defensive Driving) na Kuhakikisha kila safari yako, gari inakaguliwa, matairi, break, taa nk! Alitufundisha kutozoea safari yoyote ile wala barabara hata kama umepita njia hiyo jana! Alitilia mkazo kuwa anaendesha asionje ulabu! Na kila baada ya masaa manne simamisha gari hata Dk 20! Cheki tairi zako! Kunywa Kahawa au snacks endelea na safari!

Nasema tena, ajali haina kinga, lakini watu wengi leo, maadam gari inaenda mbele inatosha! Hivyo Mkuu watoto wangu ni wakubwa leo.....lakini mpaka sasa wanakumbuka safari za utotoni......Na tukianza safari tu wakiwa wadogo...tukifika Chalinze tu, unasikia baba tumefika.....! Naawambia bado mno.....!
 
Kumuomba Mungu atuepushe na mabaya yote alivyopanga kutuchukua atatuchukua tu haijalishi mkiwa pamoja au tofauti. Humu kwenye safari za magari binafsi kuna uzembe mwingi sana unafanyika. Mfano siku moja nilikua natoka dar kwenda klm njiani nikapita petrol station moja nikapaki nikaingia chooni nikakutana na jamaa yuko vyombo japo sio dereva nikamtania tukacheka kila mtu akatoka wakati naondoka wakaniuliza hapa na wapi nikawaambia naingia kilimanjaro. Basi nikatoka wakanipita kibati sana na ndani mziki mkubwa na totoz zinafurahi nilipofika maeneo ya chekereni nakuta ajali na ndio wao wamebamiza gari kwenye kalavati dereva hajaumia sana ila wale wala bata alooo hawatamaniki, hivyo uzembe na kujiachia safarini kuna mchango mkubwa sana kwenye kupoteza maisha. Napenda sana kusafiri na familia yangu ila nakua na utulivu wa hali ya juu mixer maombi ya wife na maji ya baraka lazima yahusike kabla ya safari kuanza unaweza ona jambo la kawaida ila kwenye imani nakua nimekata minyororo mingi ya mabaya
Lakini uzembe wakati mwingine ukawa wa Gari lingine na sio wewe. Lipo tukio la msabato mmoja alikuwa muhadhiri Moro miaka 20 iliyo pita ilitokea maaeneo ya urafiki basi lilihamia upande wake
 
Back
Top Bottom