Wazee wa zamani waliona mbali sana kifikra kuhusu maisha. Awakuruhusu watoto wao watumie chombo kimoja cha usafiri, wakae pamoja au kuambatana mara kwa mara; waliogopa kuteketeza familia at once.
Leo hii imekuwa fashion kwa ndugu kusafiri pamoja, tunapotumia chombo kimoja cha usafiri upo uwezekano mkapotea kwa pamoja. Chukueni taadhari; kawia ufike.
Poleni wote mliowahi kupoteza ndugu kwenye ajali au majanga ambayo endapo tungetenganisha wana familia may be baadhi wangekuwa hai leo
Mkuu Resilience,
Naomba kwenda kinyume na hoja yako, Mzee wangu kishatangulia mbele ya haki akiwa na kama miaka 87, alianza kutubeba ndani ya Volkswagen (Beatle) TDQ.....Tukiwa wadogo, mimi na dada zangu wawili, na Mama na mzee mwenyewe toka Moshi hadi Mbeya! Na kipindi hicho barabara ni mbaya na sehemu kubwa ni ya vumbi! Tumefanya hizo safari mara nyingi mno!
Mzee wangu akiwa ni kibosile wa serikali, mara nyingi mno alipenda kutumia gari yake ya binafsi, na hata ya ofisini akiendesha mwenyewe. Hivyo mkuu tumezunguka zunguka Tanzania mno, kama familia, na mojawapo ya kumbukumbu tamu ni safari za familia na ndugu zangu, ilisaidia sana kutu bond pamoja.
Na kwa upande wangu na hata kwa dada zangu, ni watu wa kusafiri na familia mno! Dada zangu huko walikoolewa. mmoja Songea na Mwingine Musoma, mara nyingi wanakwenda Ukweni wakienda toka Dar, na huwa naona ni dereva wazuri kuliko shemeji zangu!
Ukweli ajali haina kinga! Lakini Mzee wangu alitupa tips nyingi mno za kuendesha gari kwa usalama (Defensive Driving) na Kuhakikisha kila safari yako, gari inakaguliwa, matairi, break, taa nk! Alitufundisha kutozoea safari yoyote ile wala barabara hata kama umepita njia hiyo jana! Alitilia mkazo kuwa anaendesha asionje ulabu! Na kila baada ya masaa manne simamisha gari hata Dk 20! Cheki tairi zako! Kunywa Kahawa au snacks endelea na safari!
Nasema tena, ajali haina kinga, lakini watu wengi leo, maadam gari inaenda mbele inatosha! Hivyo Mkuu watoto wangu ni wakubwa leo.....lakini mpaka sasa wanakumbuka safari za utotoni......Na tukianza safari tu wakiwa wadogo...tukifika Chalinze tu, unasikia baba tumefika.....! Naawambia bado mno.....!