MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Je, CHADEMA ni CCM B?
Hili ni swali nimejiuliza kwa siku kadhaa baada ya kutokea tukio la udhalilishaji huko Mara. Tukio lenyewe ni kada wa CHADEMA aitwaye Chacha Heche kumshurutisha kwa maneno ya hovyo mzee mmoja aliyekuwa akifanya kibarua kwa ndugu Chacha kwamba avue shati la CCM. Lilikuwa mojawapo ya jambo la hovyo kwenye siasa kwa miaka ya hivi karibuni. Watu wengi tulijitokeza kukemea na kulaani kitendo hicho. CCM kupitia katibu mwenezi imeshatoa tamko la kulaani kitendo hicho.
Watu wengi wenye akili tulikuwa tukisubiri kuona CHADEMA kitajibu nini kuhusu suala hilo. Ni jambo linaloonekana dogo ila lenye mtego mkubwa. Binafsi nilidhani CHADEMA kingewajibika kwa kilichotokea ila kupitia makada wake wakaharibu zaidi hadi nikajiuliza kama hicho chama ni CCM B? Kupitia makada wake waandamizi kama Godbless Lema, James Mbowe na wengine wengi, tumeona post nyingi mitandaoni zikionyesha matukio yanayofanana na hilo la Chacha Heche ambayo yalifanywa na baadhi ya wanachama wa CCM kwa nyakati tofauti. CHADEMA wanadai kwamba CCM ndo waanzilishi wa hayo mambo kwahiyo na wao wamefanya kama CCM. Inasikitisha mno. Sasa chama kikuu cha upinzani kina nini cha kujitofautisha na chama tawala? CCM wakifanya makosa na wao watafanya? Basi wao ni CCM B.
CHADEMA hata kama wakishinda uchaguzi na kuingia Ikulu bado wataendelea kuwa wapinzani wa serikali yao wenyewe. Wakiwa madarakani watafanya upumbavu na kujitetea kwamba hata CCM walifanya. Watatumia muda mwingi sana kukilaumu Chama Cha Mapinduzi badala ya kupambana na ahadi zao kwa wananchi. Kama wamekuwa wakihubiri kukataa ubaguzi halafu wakikosea badala ya kuwajibika wenyewe wanakuja na utetezi wa kipuuzi kwamba mbona CCM walifanya?
Kimsingi sioni namna yoyote hiki chama kikiepuka adhabu kali watakayopewa na wananchi kwenye sanduku la kura 2025. Wananchi hawawezi kuchagua copy ya CCM wakati original CCM ipo. Pia naendelea kuwashauri muache hii tabia ya kila mwanachama hadi viongozi wenu wakubwa kutoa matamko hivyo bila utaratibu. Chama chenu hakina msemaji?