jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,540
- 25,834
Nimeingiwa na wasiwasi sana na kuhisi kama vile tunaanza kutengwa na mataifa mengine. Siyo tu kwa Kenya kufunga mpaka kwa wakati mmoja na ule wa Somalia, lakini pia balozi wa Uingereza amefuata nyayo za wamarekani kuwandoa wananchi wao.
Kwenye ile hotuba mh rais aliposema kwamba walipima mbuzi na mapapai, nilimsikia akisema tuko vitani! Akatolea mfano wa barakoa za sumu.
Kama kweli rais Maghufuli anaichukulia kuwa hii ni vita, basi ni wazi tuko vitani. Lakini nashindwa kufahamu huyo adui tunayepambana naye. Wengi wanasema ni mabeberu, je ni kweli? Tuliletewa barakoa zenye corona na mabeberu? Nadhani hata kitendo cha kutokufuata taratibu na maelekezo ya mfano WHO, kimewaonyesha baadhi labda ni kweli adui ni mabeberu.
Hawa majirani zetu wao wamefuata maelekezo yote toka mwanzo na sasa inaonekana wanaanza kuelekea kwenye msimamo kama wa mabeberu. Lakini hata hivyo bado sidhani kama tunapigana vita na majirani zetu.
Lakini cha msingi zaidi, kama “vita ni vita muraa”, je tumejipanga vipi? Tunapigana kivipi kwenye vita hii?
Kiukweli naona kama vile ni suala ambalo limeshaleta mgawanyiko siyo tu ndani ya nchi, bali hata kwa majirani zetu na hata wafadhili wetu AKA mabeberu.
Kama wamewaondoa raia wao nchini mwetu peke yake na hawajawaondoa kwa jirani, basi ni wazi hata wakati wa kutangaza kuondoa masharti, sisi tutaachwa nje. Wanaweza wakaja wale wenye kazi za muhimu tu na siyo utalii.
Mimi nadhani ukitangaza vita, ni lazima ujuwe umejipanga vipi kupambana. Tatizo linalojitokeza ni either maadui kuongezeka, au labda kutokufahamika?
Kama adui yetu kwenye vita hii anatokea nje ya mipaka ya Africa, then tumewa isolate majirani ambao wangekuwa washirika wetu? Na kama vita hii ni nje tu ya mipaka ya Tanzania, je tuna umoja wa kitaifa unaohitajika?
Kwa wale wanaodhani tuko kwenye right track, labda wanaweza kutufahamisha ni kwa namna gani tunahitaji kupambana kwenye vita hivi. Na huyo adui aliyetushambulia kwa kupitia covid-19, tunapambanaje nao?
*chukuwa tahadhari dhidi ya corona.