Hata mkiruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa mtatueleza nini cha maana tuwaelewe?

Ni ishu mpya?
Madawati na zahanati ni ishu mpya? Mbona kila mkisimama mnaongelea hayo hayo?
Kuandikisha watoto wengi wa darasa la 1 nayo ni ishu kwenu hadi mnajivunia utafikiri miaka ya nyuma walikuwa wanakatazwa na upinzani.
Msikitini na Kanisani wanahubiri kupitia maandiko yaleyale kila siku mbona huwapingi kwamba aya wanazosoma siyo ishu mpya?
 
Miaka mitano ya hayati JPM imewafumbua watanzania mambo mengi. Imewafumbua watanzania kuwa kulikuwa na pesa nyingi hazikusanywi kwa manufaa ya umma bali zilikuwa zinaingia mifono mwa watu. Lakini pia imefumbua watu juu ya mambo mengi tu. Kama hawa wanasiasa ambao hawana hoja za msingi bali kupotezea muda wananchi wasifanye shughuli za maendeleo.

Hivi hata hii leo ruhusa ya mikutano ya kisiasa ikipata ruhusa mtakuja kutuambia nini cha maana? Ripoti ya CAG imeibua ufisadi? Mbowe alifungiwa akaunti zake? Mradi wa JNHPP hauna manufaa?

Sioni haja ya kupewa nafasi ya kupoteza muda wa wakulima na wafanyabiashara.
Kuna kitu sielewi, Wanoshabikia awamu ya mwenda zake wengi wao ni watu roho mbaya ,sura ngumu yaani ile mijitu katili inayo jifanya mema mbele za watu .Sura ngumu .Watu moderate and low huezi kuta group hii.
 
Ndugu kama wewe ulilelewa kwa manyanyaso na wazazi wako- ni wewe. Wengine tulilelewa kwa uhuru ndio maana tunathamini kila mtu kuwa huru. Kuleta chakula kizuri nyumbani isiwe tiketi ya kunyanyasa watoto.
Isitoshe mama kaomba akosolewe hivyo uovu wako utabaki nao moyoni mwako . Mungu akusamehe sana.[emoji120]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mkuu futa hii post unajiabisha. Yaaani ishu ya malezi inahusika vipi na mikutano ya siasa? Wazazi wako walikulea kwa uhuru kuwa unaropoka pumba hata wakati wa kazi? Uhuru wa kipuuzi.
 
Madawati na zahanati ni ishu mpya? Mbona kila mkisimama mnaongelea hayo hayo?
Kuandikisha watoto wengi wa darasa la 1 nayo ni ishu kwenu hadi mnajivunia utafikiri miaka ya nyuma walikuwa wanakatazwa na upinzani.
Msikitini na Kanisani wanahubiri kupitia maandiko yaleyale kila siku mbona huwapingi kwamba aya wanazosoma siyo ishu mpya?
Umeandika nini sasa? Huna hata aibu?
 
Kumbe umeanzisha thread kwa ajili ya wenye aibu? Samahani Mimi sina aibu za kidemudemu kama wewe.
Mbona unapost pumba kama huna akili? Mahubiri ya kanisani yanaingia vipi mamii?
 
Operation Sangara ilipoteza muda wa watanzania wengi.
Acha u chawa!
IMG_20210329_125220.jpg
 
Tukiruhusiwa kufanya mikutano ya siasa na nani?Unaandika kama mtu ambae kichwani hamna kitu!Suala la kufanya mikutano ya kisiasa siyo mapenzi,hisani,kudra wala takwa la Rais au mtu mwingine yoyote yule.

Suala la kufanya mikutano ya kisiasa ni haki yetu kikatiba.

Haki huwa haiombwi wala huwa haitolewi bure kama unavyodhania bwana mleta uzi bali haki huchukuliwa kwa nguvu.

Rais hana wajibu wala haki wala nguvu wala amri ya kuzuia au kuruhusu mikutano ya kisiasa na pia hatuna haja wala wajibu wa kumuomba Rais aruhusu mikutano ya kisiasa bali ni haki yetu na mtu yoyote yule ikiwa ni pamoja na Rais akituzuia tuna wajibu kikatiba wa kuchukua haki hiyo kwa nguvu.

Rais atake asitake suala la kufanyika mikutano ya kisiasa ni haki yetu kikatiba wala siyo mapenzi yake na asipotaka tuna wajibu kikatiba wa kumlazimisha.

Umeelewa mleta mada?
 
Kuna lipi jipya watanena

Kuna lipi jipya watanena?

Mhu 1:9 SUV​

Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
SUV: Maandiko Matakatifu ya Mungu ,ataa mwendazake hakuna jipya alilolileta .kwa upinzani awataleta mapya zaidi sana wanayo yakusemia mema ya zamani yarudishwa na kusemea mema mapya yaongezwe
 
Miaka mitano ya hayati Magufuli imewafumbua Watanzania mambo mengi. Imewafumbua Watanzania kuwa kulikuwa na pesa nyingi hazikusanywi kwa manufaa ya umma bali zilikuwa zinaingia mikononi mwa watu. Lakini pia imefumbua watu juu ya mambo mengi tu. Kama hawa wanasiasa ambao hawana hoja za msingi bali kupotezea muda wananchi wasifanye shughuli za maendeleo.

Hivi hata hii leo ruhusa ya mikutano ya kisiasa ikipata ruhusa mtakuja kutuambia nini cha maana? Ripoti ya CAG imeibua ufisadi? Mbowe alifungiwa akaunti zake? Mradi wa JNHPP hauna manufaa?

Sioni haja ya kupewa nafasi ya kupoteza muda wa wakulima na wafanyabiashara.
Kwako unataka hoja gani
 
Huo ugonjwa unaitwa uoga wa hoja tofauti/mbadala, na ndio ugonjwa mkuu aliyokuwa nao Jiwe.
Yaonekana wewe na wengine mliokuwa mmemkabidhi AKILI mmeurithi.
Tunazidi kumwomba Mungu awaepusha wanenu pamoja na vizazi vyao ili kulinusuru TAIFA letu.
AMEN
 
Miaka mitano ya hayati Magufuli imewafumbua Watanzania mambo mengi. Imewafumbua Watanzania kuwa kulikuwa na pesa nyingi hazikusanywi kwa manufaa ya umma bali zilikuwa zinaingia mikononi mwa watu. Lakini pia imefumbua watu juu ya mambo mengi tu. Kama hawa wanasiasa ambao hawana hoja za msingi bali kupotezea muda wananchi wasifanye shughuli za maendeleo.

Hivi hata hii leo ruhusa ya mikutano ya kisiasa ikipata ruhusa mtakuja kutuambia nini cha maana? Ripoti ya CAG imeibua ufisadi? Mbowe alifungiwa akaunti zake? Mradi wa JNHPP hauna manufaa?

Sioni haja ya kupewa nafasi ya kupoteza muda wa wakulima na wafanyabiashara.
Kwenye sayansi ya biblia inasema Yesu aliulaani mtini ambao haukuwa na tini (matunda) ambayo haukuwa wakati wake wa kutoa tini. Swali je Yesu hakujua kuwa si mda wake wa mtini kutoa tini? Je aliuonea ule mti kulani? Ndipo ujue mawazo yako si ya Mungu na njia zako si za Mungu pia. Hii ni kwa wenye akili tu.
 
Miaka mitano ya hayati Magufuli imewafumbua Watanzania mambo mengi. Imewafumbua Watanzania kuwa kulikuwa na pesa nyingi hazikusanywi kwa manufaa ya umma bali zilikuwa zinaingia mikononi mwa watu. Lakini pia imefumbua watu juu ya mambo mengi tu. Kama hawa wanasiasa ambao hawana hoja za msingi bali kupotezea muda wananchi wasifanye shughuli za maendeleo.

Hivi hata hii leo ruhusa ya mikutano ya kisiasa ikipata ruhusa mtakuja kutuambia nini cha maana? Ripoti ya CAG imeibua ufisadi? Mbowe alifungiwa akaunti zake? Mradi wa JNHPP hauna manufaa?

Sioni haja ya kupewa nafasi ya kupoteza muda wa wakulima na wafanyabiashara.
Unahofu gani wakifanya mikutano yao ya kutafuta wanachama na mashabiki? Kutowapa nafasi ya kufanya hivyo ni sawa kuwazuia Simba au Yanga kufanya mazoezi kwa ajili ya mapambano. Hata hivyo katiba ya nchi inaruhusu. Usiwe na hofu. Acha timu zifanye mazoezi kwa mpambano wa 2025.
 
Mna nini cha kutueleza wakati mnatuta wanachama?
 
Miaka mitano ya hayati Magufuli imewafumbua Watanzania mambo mengi. Imewafumbua Watanzania kuwa kulikuwa na pesa nyingi hazikusanywi kwa manufaa ya umma bali zilikuwa zinaingia mikononi mwa watu. Lakini pia imefumbua watu juu ya mambo mengi tu. Kama hawa wanasiasa ambao hawana hoja za msingi bali kupotezea muda wananchi wasifanye shughuli za maendeleo.

Hivi hata hii leo ruhusa ya mikutano ya kisiasa ikipata ruhusa mtakuja kutuambia nini cha maana? Ripoti ya CAG imeibua ufisadi? Mbowe alifungiwa akaunti zake? Mradi wa JNHPP hauna manufaa?

Sioni haja ya kupewa nafasi ya kupoteza muda wa wakulima na wafanyabiashara.
Du we kiazi kweli yapo mengi ambayo wewe na wenzako mnatakiwa kuambiwa, Ripoti ya CAG imeonyesha pesa nyingi zimepotelea serkalini zaidi kuliko kwa watu:
a. mikutano itakuambia kwanza rushwa ndani ya jeshi la polisi sio imekuwa kero bali inaumiza waliojiajiri na kuajiliwa katika sekta za usafirishaji, inafanya mazingira ya kufanya biashara Tanzania kuwa mabaya kuliko ubaya wenyewe, rushwa hiyo pia inatupaka matope kama nchi kwa wageni wanaokuja kutembea na kufanya biashara.
b. \notifications wanazotoza traffic ni ujambazi wa serikali kwa raia wao
c. Mkulima ndio mjonge kuliko wanyonge wenyewe mfano wanaolima tumbaku tu yaani serikali, vyama vya ushirika, wazabuni, wanunuzi wote wametolea macho hicho kidogo anachpata mkulima wakitafune.
d. serikali inatumia mabavu kulinda makosa ya watangulizi, mtu alikosea kufanya maamuzi na hayupo kivuli kinawatesa waliobaki
Yapo mengi tu
 
Mkuu idugunde itabidi uvumilie za uso Leo.
 
Back
Top Bottom