Hata mkiruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa mtatueleza nini cha maana tuwaelewe?

Hata mkiruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa mtatueleza nini cha maana tuwaelewe?

Miaka mitano ya hayati Magufuli imewafumbua Watanzania mambo mengi. Imewafumbua Watanzania kuwa kulikuwa na pesa nyingi hazikusanywi kwa manufaa ya umma bali zilikuwa zinaingia mikononi mwa watu. Lakini pia imefumbua watu juu ya mambo mengi tu. Kama hawa wanasiasa ambao hawana hoja za msingi bali kupotezea muda wananchi wasifanye shughuli za maendeleo.

Hivi hata hii leo ruhusa ya mikutano ya kisiasa ikipata ruhusa mtakuja kutuambia nini cha maana? Ripoti ya CAG imeibua ufisadi? Mbowe alifungiwa akaunti zake? Mradi wa JNHPP hauna manufaa?

Sioni haja ya kupewa nafasi ya kupoteza muda wa wakulima na wafanyabiashara.
Hayo yalikuwa maneno matupu, tumeshuhudia upigani mkubwa na hajaongeza mishahara
 
Back
Top Bottom