Hapo namba 3 na 5 ndo nitajitahidi nisiwapigie. Waliobaki kama watanipa msaada fresh tu hata wakiniongelea vibaya ili mradi wamenisaidia. Maneno hayaui. Mzee Mshana kuna shida ikikukuta utaomba ardhi ipasuke ikumeze.Hata kama umekwama kiasi gani kifedha au kihisia, hakikisha kuna namba za simu ambazo huzipigii kamwe ili kujiepusha na madhara makubwa zaidi.
Dharura
Watakutaka uweke dhamana ya vitu vya thamani kubwa sana kama viwanja au magari kwa mkopo mdogo wa dharura wakijua fika huwezi kulipa kwa wakati ili wavichukue.
Ni kweli shida ikipiga aibu zote pembeniShida zikikushika ndo utapata akili, hapa kwenye mada ngoja tuendelee kudanganyana
Na kuna wale wa jana na kesho...Kuna watu, hasa ndugu wakikusaidia hata buku kumi, basi siku ukitoboa wewe lazima kila wakikuomba msaada uwasaidie, la sivyo watakuwa wanakukumbusha mara vile walivyowahi kukusaidia 😂
Nyambafu sana watu wa aina hii.
Sasa mtoa mada muache apige Taarabu Labda hajawah kupatwa na shida itakayomfikisha hukoNi kweli shida ikipiga aibu zote pembeni
Kuna yule ukianza kumwelezea shida yako, akiona dalili unataka kumuomba msaada anakuwahi kwa kukuhadithia shida yake ambayo ni kubwa kuliko yako (shida ya kutunga) 😂Na kuna wale wa jana na kesho...
Yaani jana tu nilikuwa na hiyo Ila kina kaishu nimeifanyia.. Hebu nicheki kesho tuone🙌🏿😂
Mkuu Mshana vipi zipe pisi kausha damu pale Sinza Kitambaa cheupe tunaruhusiwa kupokea simu zao??Hata kama umekwama kiasi gani kifedha au kihisia, hakikisha kuna namba za simu ambazo huzipigii kamwe ili kujiepusha na madhara makubwa zaidi.
Dharura na shida ni mambo ya mpito, lakini maamuzi unayoyafanya ukiwa katika hali ya kukata tamaa yanaweza kukuandama na kukuharibia heshima na furaha yako kwa miaka mingi ijayo.
1. Watu wanaokutunzia akiba ya maneno (Wambea):
Hawa ni watu ambao ukiwaomba msaada leo, kesho unakuwa mada kuu ya mazungumzo kwenye vikundi vyao au mitandaoni.
Wanatumia shida yako kujifanya wasamaria wema huku wakikuharibia sifa na heshima yako kwa watu wengine.
2. Wapenzi wa zamani waliokuumiza (Ma-Ex): Kupiga namba hizi ukiwa kwenye uhitaji au dharura kunakushusha thamani na kukufanya uonekane huna msaada mwingine.
Mara nyingi wanatumia fursa hiyo kukuharibia amani ya akili, kukuwekea masharti magumu, au kukurudisha kwenye maumivu uliyoyakimbia.
3. Wakopeshaji wa mtandaoni wasio rasmi (Kausha Damu):
Kampuni hizi hukupa pesa haraka lakini zinakuja na riba kubwa na mbinu za kinyari za kudai.
Ukichelewa kulipa, hawasiti kupiga namba za ndugu, marafiki, na wafanyakazi wenzako ili kukudhalilisha na kukuharibia amani ya akili.
4. Marafiki wanafiki na watu wenye wivu:
Hawa ni wale wanaofurahia kuona umekwama ili wajione wako juu yako au wamefanikiwa kukuzidi.
Ukiwapigia simu watajifanya wanakuhurumia lakini kiuhalisia watakupa majibu ya kukatisha tamaa na hawatakusaidia lolote zaidi ya kueneza habari zako.
5. Matapeli na watu wanaotaka dhamana zisizo na uwiano:
Kundi hili linajumuisha watu wanaovizia ukiwa kwenye shida kubwa ili wakupore mali zako. .
Watakutaka uweke dhamana ya vitu vya thamani kubwa sana kama viwanja au magari kwa mkopo mdogo wa dharura wakijua fika huwezi kulipa kwa wakati ili wavichukue.
Hao mliachana kwa furaha.Nina namba za maex kibao na bado nawapiga vizinga
ukishageuka kuwa mtu mbaya ni kazi sana kurudi kwenye hali ya kuwa mwema💪🏿🙏🏿Maisha yanaweza kukufanya vile yanavyoona ni sawa wewe uwe .
Hakika tunaishi mara moja ila ukipata nafasi ya kuwa mwema utunze wema huo ndani ya moyo wako udumu maana ukishageuka kuwa mtu mbaya ni kazi sana kurudi kwenye hali ya kuwa mwema .
Mungu anisamehe na anisaidie Sana... Nina roho ngumu ya kuomba assist kwa mtu ambaye tulishamalizanaKuna lakujifunza hapa wengi wame yapitia ila wanajisahsulisha. mwenyekusia na asikie na mwenye kuona na aone siyo mpaka likufike ndo uanze kutafuta mchawi maishani mwako.