Hataki kunipa talaka

Hataki kunipa talaka

aisee omba talaka tu haiwezekani mtu akukosee kiasi hicho undelee kumvumilia huwa wanasema samee Mara saba ya sabini lakini sio ya semanini huo amevuka sabini mtupe chini
 
Ni mume wangu, mwaka wa 7 ndoani with one kid, nimefuma anachat na mwanamke kimahaba, nikajishusha tuyaongee mwenzangu ananijia juu.
Sasa nimeamua ndoa basi, nataka talaka yangu na yeye kunipa hataki.
Niko stressed jamani, nishaurini mwenzenu.

Yani Mimi ndio nimekosewa na bado nanuniwa, na nikimwambia tuachane hataki. Nifanyeje?
Umeenda mbali sana dada mpaka kwenye kuachana?Ziko sababu za watu kuachana kwa dini zote.Ni moja kati ya hiyo unayoisema?Kwanini usitumie njia ya mazungumzo kwanza hata na watu wake wa karibu basi.Ok mtoto amewakosea nini mpaka mfikie hapo?Hakuna kitu kinamuathiri mtoto kisaikolojia kama kujua wazazi wake waliachana na sasa analelewa na mzazi mmoja wakati mwingine yuko bado hai.
 
Unataka kuachwa? Wanawake wa siku hizi mna problem sana.

Ebu kaa kitako na mumeo muyamalize huko haraka
 
Moyo sukuma damu..........!!!!!; bata ukimchunguza sana hafai kabisaaaa kuwa kitoweo
 
Mahusiano changamoto zake ni hizo, cha kufanya kaeni chini mmalize changamoto zenu na si kukimbilia kuvunja ndoa.
 
Kuomba Talaka Sio Suluhisho Maana Kumbuka Tabia Hizi Za Wanaume Kuwa Na Michepuko Hanazo Mumewako tu Asilimia kubwa ya wanaume tupo hvyo sasa Ukisema Uombe Talaka Kwa sababu ya mumeo kumfuma akichat na kimada?Je Huko Utakapokwenda Nani Kakuambia Kuko Salama?Tafakari Sana Jitahid Kutetea Ndoa Yako Maana We Unae Wenzako Hawana Wanamtafuta Sasa We Muache Huyo Mumeo Utakuja Kujuta Hapo Baada,Kaa Chini Muyaonge Yaishe Mlee Mwanenu
 
Mmmh pole sana lakini Chats mbona kitu cha kawaida...hilo suala linazungumzika au humpendi mumeo? Au wote wawili mmechokana may be
 
Mijanaume ni minafiki sana, kumkuta mtu anachat kimapenzi na mtu kuonyesha wako kwenye mahusiano sio kosa? Halafu yeye ndiye alete jeuri wakati mwenzie kajishusha?? Hebu fanya hii visevesa na mvae ubinadamu.

Dada sali sana Mungu akufanyie wepesi na uvumilivu kwa muda japo hujasema kakununia mda gani
 
Ananipiga, tena hata mbele za watu wengine, nimevumilia, sasa kama kapata mwingine ndio namuachia nae zamu yake aje ayaone.

Mama yangu najua Una Baba na Mama kuna wazee wake Kwa nini usiwahusishe Hao watu ili uone kuliko kuja kushauriwa na Huyu Ambaye anajiita Ndoa yake kuwa na Amani Mrs Air.. ( Mrs Upepo/sijui Hewa)?

Huyu yeye yupo kwake anakaangiza lakini huku anakwambia uondoke.. Mama epuka wanawake wa aina ya Mrs. Air ni watu wabaya sana watu wanaofurahi wewe kuahribikiwa wakati wao wapo makwao wanasugua Gaga.. Ni Nyoka ona sasa umeona kuwa ni haki kwa ulichokiamua.

Labda ungeondoka tu bila kumshutisha kukupa karatasi yoyote sasa hilo swala la kumlazimisha akupe linaweza kuzaa mauti.

Ila nakupa Pole sana hata iweje mimi kama nisingekushauri utoke hapo bali ningekushauri Kwanza kujiangalia kwa nini anakufanyia hivyo inawezekana na wewe unakasoro fulani ya kutokuwa na break unapokuwa unajibizana naye.

Ila sikuonei Huruma hata kidogo
 
Unajua huwa siwaelewi ndoa inapofeli lawama mnatupa sisi, imagine sisi wote wafanyakazi lakini mume wangu hali chakula cha Dada wa kazi, sharti nimpikie tena nampikia vizuri, namfulia, nafukiza nyumba, sifichi kipato changu, namtii hata kwenye mambo mengine ambayo hayana maana. sitoki bila ruhusa, nifanye lipi la zaidi?

Najua kama binadamu sijakamilika, ila I can't do more than what am doing now.
Ndo mana nataka talaka ili atafute anayeona anamfaa kama Mimi nina mapungufu, na Mimi nitampata anayeridhika.
 
Mama yangu najua Una Baba na Mama kuna wazee wake Kwa nini usiwahusishe Hao watu ili uone kuliko kuja kushauriwa na Huyu Ambaye anajiita Ndoa yake kuwa na Amani Mrs Air.. ( Mrs Upepo/sijui Hewa)?

Huyu yeye yupo kwake anakaangiza lakini huku anakwambia uondoke.. Mama epuka wanawake wa aina ya Mrs. Air ni watu wabaya sana watu wanaofurahi wewe kuahribikiwa wakati wao wapo makwao wanasugua Gaga.. Ni Nyoka ona sasa umeona kuwa ni haki kwa ulichokiamua.

Labda ungeondoka tu bila kumshutisha kukupa karatasi yoyote sasa hilo swala la kumlazimisha akupe linaweza kuzaa mauti.

Ila nakupa Pole sana hata iweje mimi kama nisingekushauri utoke hapo bali ningekushauri Kwanza kujiangalia kwa nini anakufanyia hivyo inawezekana na wewe unakasoro fulani ya kutokuwa na break unapokuwa unajibizana naye.

Ila sikuonei Huruma hata kidogo

Nimeshirikisha ndugu wananambia nivumilie, nivumilie hadi lini?
 
Kwahiyo umeamua kitumbua kiliwe nje tu sasa. Kwani umejaribu kushirikisha wakubwa imeshindikana? Ila na sisi wanaume mengine tunayatafutaga wenyewe.pole Mama K
 
Ni mume wangu, mwaka wa 7 ndoani with one kid, nimefuma anachat na mwanamke kimahaba, nikajishusha tuyaongee mwenzangu ananijia juu.
Sasa nimeamua ndoa basi, nataka talaka yangu na yeye kunipa hataki.
Niko stressed jamani, nishaurini mwenzenu.

Yani Mimi ndio nimekosewa na bado nanuniwa, na nikimwambia tuachane hataki. Nifanyeje?
Mmm kuchati tu,unadai talaka,utaachika Mara ngapi?
 
Back
Top Bottom