Hatari! Majasusi wengi wa Rwanda wanawekeza Kagera, Geita na Kahama mkoani Shinyanga

Hatari! Majasusi wengi wa Rwanda wanawekeza Kagera, Geita na Kahama mkoani Shinyanga

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Hii ni hatari mno kwa usalama wa nchi yetu!

Majasusi wengi wa Rwanda wanawekeza kwenye nyanja mbalimbali kuanzia kilimo,viwanda na biashara mbalimbali kwenye maeneo niliyoyataja hapo.

Ifahamike, sera na wanahistoria wa Rwanda wanatambua eneo lote kuanzia Kagera, Kigoma, Geita na hata Kahama kuishia pale Isaka ni eneo waliloporwa na hayati Mwalimu Nyerere jambo ambalo si la kweli.

Vyombo vya dola vya Tanzania yetu shtukeni-Rwanda si rafiki mwema hata kidogo!

Hata sasa vita anavyovifadhili huko mashariki ya Congo ni kwa sababu ya tamaa ya eneo lile ili wajitanue na wanyakue Kivu belt yote kwa maslahi ya madini.

Tanzania itambue Rwanda haipaswi kuchekewa hata kidogo
 
Andika taratibu kwa ufafanuzi wa kina. Suala la uwekezaji ni la kisheria na kisera, Tanzania inawawekezaji kutoka mataifa mengi Duniani, kwa nini una nongwa na Rwanda?!!

Kuna sheria za uwekezaji, badala ya kuwa na nongwa na Rwanda waambie CCM wenzako wafanyie kazi sheria na sera za uwekezaji ili kujilinda na hatari unazosema. Siyo kwa Rwanda tu, bali wawekezaji wote wa kutoka ndani na nje ya nchi.
 
Haya madai yako umeyathibitisha vipi?
Ni rahisi mrundi au mnyarwanda kuingia huku na kuishi ikiwa anajua Kiswahili kuliko Mtanzania kuingia Rwanda na kuishi kwa sababu
1. Watanzania walio wengi hawana interest na nchi za Rwanda na Burundi.
2. Hakuna Mtanzania wa kawaida atatia nia kujua Kinyarwanda na Kirundi kwa sababu sio dili kwao ILA ni rahisi kwa Mnyarwanda na Mrundi kujibidisha na Lugha ya Kiswahili ili aje huku.

Ukiishi mipakani kule utaamini unayo ambiwa.
 
Suala la uwekezaji ni la kisheria na kisera, Tanzania inawawekezaji kutoka mataifa mengi Duniani, kwa nini una nongwa na Rwanda?!!
Inawezekana ni kweli unachokisema lakini pia inawezekana hujataka kumuelewa mleta mada.

Sheria na Sera kwa Tanzania? Labda

Kipindi cha Msoga, kulikuwa na general mmoja wa jeshi, wakasema ni wa huko, kelele kelele zile baada ya operation ile, jambo likafanyika aisee, sisi ndo tukajua kumbe ni kweli na wamepenyezwa wengi. Nadhani M23 alichapika kipindi hicho pia.
 
Ni rahisi mrundi au mnyarwanda kuingia huku na kuishi ikiwa anajua kiswahili kuliko mtanzania kuingia rwanda na kuishi kwa sababu
1. Watabzania walio wengi hawana interest na nchi za rwanda na burundi
2. Hakuna mtanzania wa kawaida atatia nia kujua kinyarwanda na kirundi kwa sababu sio dili kwao ILA ni rahisi kwa mnyarwanda na mrundi kujibidisha na lugha ya kiswahili ili aje huku.

Ukiishi mipakani kule utaamini unayo ambiwa
So maana yake ulinzi wetu mipakani ni dhaifu, sioni ubaya mkitoa taarifa kwa mamlaka husika ili hao wavamizi wakamatwe na kuchukuliwa hatua stahiki.
 
Wapo na wengine ni mawaziri katika jamuhuri yetu, asili yake ni huko huko kwa PK wamewekeza nyanja nyingi tuu madini,burudani, usafirishaji.

kifupi walijipanga muda mrefu tuu wengine walikuwa watumishi kwenye majeshi yao na wakaja huku kujifanya wafanyabishara.
 
Rwanda, hasa Kagame anaiogopa Tanzania kuliko kitu chochote kile maisha yake yote, sbb anajua tulichomfanya enzi za JK, na akijaribu tena, we must have his thin legs and ass up 4 good..!! Bahati nzuri sana PK anatujua sana, ujinga wake atafanya hapo mashariki ya DRC tu.
 
Nyerere alisema Binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja.Waafrika tuache kutuhumiana ndio maana hatuendelei .Wazungu wa Ulaya ruksa kuishi popote Ulaya mradi uwe na shughuli yako halali Sisi tunazibiana bila sababu za msingi. Tunafungua nchi kwa wazungu wakati Sisi kwa Sisi tunafungiana
Mtu kama ana shughuli halali mwache

Waafrika tufike mahali tuone Afrika kama nchi moja ambako ni kwetu tusiwe na vimawazo vya kila mmoja kuwaza ohh mimi kwangu Rwanda au kwangu Tanzania au Uganda ni ujinga.

Mleta mada hata wewe ruksa nenda Rwanda kawekeze tena kule Taratibu za uwekezaji rahisi mno.Wame digitalize kila kitu husumbuki

Mawazo ya kila ukimuona mnyarwanda kutuhumu jasusi hiyo si sahihi .Nchi zetu maskini mno tuna hitaji kubwa la kiuchumi tuinuke kuliko kuhangaika na kujasusiana na kila mtu kutuhumu maskini mwenzie kuwa anamfanyia ujasusi
 
Hii ni hatari mno kwa usalama wa nchi yetu!

Majasusi wengi wa Rwanda wanawekeza kwenye nyanja mbalimbali kuanzia kilimo,viwanda na biashara mbalimbali kwenye maeneo niliyoyataja hapo.

Ifahamike, sera na wanahistoria wa Rwanda wanatambua eneo lote kuanzia Kagera, Kigoma, Geita na hata Kahama kuishia pale Isaka ni eneo waliloporwa na hayati Mwalimu Nyerere jambo ambalo si la kweli.

Vyombo vya dola vya Tanzania yetu shtukeni-Rwanda si rafiki mwema hata kidogo!

Hata sasa vita anavyovifadhili huko mashariki ya Congo ni kwa sababu ya tamaa ya eneo lile ili wajitanue na wanyakue Kivu belt yote kwa maslahi ya madini.

Tanzania itambue Rwanda haipaswi kuchekewa hata kidogo
Mimi nilishangaa walipotaka kuwapa mkoa wao wa Chato. Hii nchi siku hizi hatupo siriasi.
 
Yani mama angenipa tender yakuanzisha jeshi binafsi kama la Putin Wagner. Tunashuka Kigali na miamvuli at night under cover of darkness with highlytech sophisticated assault weapons na kutandanza mkong'oto wa aina yake na baada ya hapo tunabadilisha regime na Rwanda inakuwa mpya na upuuz hautaendelea tena East Africa na maziwa makuu kwa jumla.
 
Ni rahisi mrundi au mnyarwanda kuingia huku na kuishi ikiwa anajua kiswahili kuliko mtanzania kuingia rwanda na kuishi kwa sababu
1. Watabzania walio wengi hawana interest na nchi za rwanda na burundi
2. Hakuna mtanzania wa kawaida atatia nia kujua kinyarwanda na kirundi kwa sababu sio dili kwao ILA ni rahisi kwa mnyarwanda na mrundi kujibidisha na lugha ya kiswahili ili aje huku.

Ukiishi mipakani kule utaamini unayo ambiwa
Chaguzi zilizopita wanyarwanda baadhi hasa wadada walijichomeka kugombea nafasi za udiwani na serikali za mitaa huko kanda ya ziwa
 
Hii ni hatari mno kwa usalama wa nchi yetu!

Majasusi wengi wa Rwanda wanawekeza kwenye nyanja mbalimbali kuanzia kilimo,viwanda na biashara mbalimbali kwenye maeneo niliyoyataja hapo.

Ifahamike, sera na wanahistoria wa Rwanda wanatambua eneo lote kuanzia Kagera, Kigoma, Geita na hata Kahama kuishia pale Isaka ni eneo waliloporwa na hayati Mwalimu Nyerere jambo ambalo si la kweli.

Vyombo vya dola vya Tanzania yetu shtukeni-Rwanda si rafiki mwema hata kidogo!

Hata sasa vita anavyovifadhili huko mashariki ya Congo ni kwa sababu ya tamaa ya eneo lile ili wajitanue na wanyakue Kivu belt yote kwa maslahi ya madini.

Tanzania itambue Rwanda haipaswi kuchekewa hata kidogo
Iyo aya ya 3, mkuu hao wa rwanda wana bakwa kama kweli wana amini huo upuuzi ...kwanza sio sahihi

Maana kama ni hivyo wanataka kuijumuisha na kagera, basi waka kwapue na eneo la M7 ambako nako jamii ya wahaya ndio wana unasaba kabisaaa na jamii ya waganda waishio kusini ...kutoka bukoba mpaka mtukula ni almost 6 km kama sikosei...

Na pia hii tabia ya kukahofia hako kanchi sasa ifike tamati jaman .....Tz sio DRC ...hako kanchi unafikiri kenyewe hakajui wapi pa kuchokoza na wapi pakutochokoza ..... Ifahamike Drc wana changamoto nyingine pia ambazo zina kuza na kidhoorotesha amani nchini kwao ....

Ila umetoa alert nzuri na amini vyombo vyetu vipo makin muda wote
 
Back
Top Bottom