Hatari! Majasusi wengi wa Rwanda wanawekeza Kagera, Geita na Kahama mkoani Shinyanga

Hivi bado Paul Kagame kuomba kujiunga East Africa community ni mjinga?? Si Kenya si Uganda wala Tanzania kote kule Kagame anawapelelezi.
Akishatupeleleza what next?

Kwani unahisi na sisi hatumpelelezi?
 
Cha muhimu ni serikali kuwabana kwenye kuajiri wafanyakazi, hakuna kuleta wanyarwanda nje ya wale walioruhusiwa kisheria. kama wanawekeza nchini kwetu, na watalipa kodi, acha wawekeze. si wanaiba huko congo wanakuja kuwekeza bongo, shida nini? wanyarwanda wanaweza kupose hatari yeyote kwa watanzania? never.
 
Akishatupeleleza what next?

Kwani unahisi na sisi hatumpelelezi?
Lengo la intelijensia huwa nini mkuu?? A somebody planned to dominate his country until his death, kwa hiyo anawahofia majirani zake wasitibue plan zake,
 
Hakuna kitu kama hicho wamiliki wa biashara na matajiri wa Tanzania ni maarufu Tena mikoa yote ukiacha waarabu, wasomali na wahindi hakuna jamii nyingine yoyote iye inayomiliki biashara kubwa tofauti na wazawa
Malori mengi ya watutsi kutoka rwanda sina namba zao za magari, Mbona tunayoona barabarani huku mengi.
 

Punguza kuangalia movie zile za video
 
Wewe humjui, alishasema hafikirii kuitawala sehemu ya Tanzania kijeshi kwa sasa. Maana yake ana mikakati ya muda mrefu. Alianza na kushika nguvu za kiuchumi hasa ufugaji, sasa ameingia kwenye biashara, na taratibu anaingia kwenye uongozi - Hii ni project ya muda mrefu.
Unaijua Karagwe wewe! Fanya utafiti uone hali ilivyo
 
Bwana elias,hiyo ni ideology ya kibaguzi amabayo unataka kuipenyeza kwa watanzania ili yawe kama ya congo,hivi kwa akili yako hatakama kuna wanayarwanda waliowekeza tanzania unafikiri wataanzisha vita kwa sababu ipi?

Watanzania sio watu wenye ubaguzi,watanzania ni watu ambao wameishi na wanyarwanda muda mrefu bila mikwaruzano,tofauti na congo tangu zamani estern congo wamekua na vikundi vyakikabila vya kujihami,mapigano kati ya makabila congo ndio kawaida yao tofauti na tanzania ambayo ina amani,nyerere aheshimiwe sana aliweza kuwaunganisha watanzania na kuwakataza ukabila,ukabila ni mbaya sana,sasa watanzania inabidi muwe makini na watu wenye fikira kama za huyu elias,uchochezi unaanzaga hivi,mtu anazua story tu na watu bila kua makini ,wanajikuta wametumbukia katika migogoro ya kipuuzi.
 
Bahima Empire !! ??
Hili neno Bahima Empire nikitu cha uzushi tu,katika karne hii utawezaje kuweka empire?hawa watu wenye chuki na watutsi walitafuta kitu cha kuwatenganisha waafrika kuwafanya watufulani kujiona watutsi/hima na wengine wahutu ili pawepo uadui kati ya makundi hayo mawili na watu waishi wakiwahofia wenzao na hata kufikia kuuana,huu ni mpango wa interahamwe kutafuta support kutoka sehemu mbalimbali dhidi ya watutsi/hima tu ,hicho kitu hima empire hakipo kabisa.
 
Hawa jamaa basi tuu ni nyoka na wanajifanya wanaakili sana.....sasa dawa yao ni kuwasaka na kuwapa haki yao, wanachokifanya DRC hakifurahishi hata kidogo.
Watutsi wa DRC walikuwepo pale hata kabla ya hiyo mipaka ya berlin ,pale ni kwao lakini kwasababu umeisha ingiwa na sumu ya uterahamwe huwezi elewa,vita ya DRC ilikuwepo tangu zamani na imekua mbaya baada ya interahamwe kuvamia estern congo,sasa wanachofanya hao M23 nikujihami na hao interahamwe na watu kama wewe wenye mtazamo mbaya dhidi ya watutsi.
 
Sio waafrika wote au wanyarwanda wote maskini

Dangote Mwafrika mwenzetu ngozi nyeusi mbona kawekeza Tanzania

Tufike mahali tukubali kuwa kuna waafrika wenzetu ngozi nyeusiwawe Rwanda nk waweza kuwekeza
Unajua watanzania sio wabaguzi tangu zamani,lakini baada ya kuingiliwa na wakimbizi wa kihutu wenye itikadi ya kibaguzi wamefanikiwa kuwaroga baadhi ya watanzania ,ndio maana tunaona watu wenye mitazamo ya kiterahamwe,mtutsi ni mtu kama mtu mwingine,kama kawekeza ni kwafaida ya watanzania na nahao wawekezaji,na cha muhimu asivunje sheria za nchi,na nina uhakika nchi hii inavyombo vya usalama ambavyo viko makini.
 
Nafikiri mnyarwanda wa sasa hahitaji uraia wa tanzania,anahitaji kufanya biashara na tanzania,na mnyarwanda yeyote mwenye pesa yake akitaka kuwekeza tanzania hawezi kuzuiliwa,uoga wa aina hii nikuonyesha kutojiamini na kuamini vyombo vya usalama vya tanzania,inabidi watu tufunguke wakati huu ni wakati wa business sio majungu
 
Nafikiri mnyarwanda wa sasa hahitaji uraia wa tanzania,anahitaji kufanya biashara na tanzania,na mnyarwanda yeyote mwenye pesa yake akitaka kuwekeza tanzania hawezi kuzuiliwa,uoga wa aina hii nikuonyesha kutojiamini na kuamini vyombo vya usalama vya tanzania,inabidi watu tufunguke wakati huu ni wakati wa business sio majungu
Mbona tanzania tuna wabunge na viongozi wa kihindi,somali,warabu n.k mbona hichokitu hamkiongei?je kwakipindi hichochote tangu 1959 mliishawahi sikia hao wakimbizi wa kinyarwanda kuisaliti tanzania?please muachane na huo ubaguzi,kama ni raia kwanini asiwe kada wa ccm ?nimeshangaa kusikia mtu akisema eti wamejaa mwanza ni walimu,sasa wanafundisha mtoto wa nani?badala ya kujivunia kua na watu kama hawa mnaanza kuleta chuki zisizokua na tija.
 
Hilo jina tu Biteko = Bhiteko
Hivi hata kama biteko ana asili ya rwanda na akawa na uraia wa tanzania na kaaminiwa na wananchi wakamchagua kama mbunge wao,nchi ikamuamini ikampa wizara na kaiongoza vizuri,hiyo wasiwasi uliyonayo unaitoa wapi?kama wewe sio interahamwe?
 
Tunaonewa sana sisi wenye asili ya wahima na tumezaliwa hapa wala hatujui chochote kuhusu Rwanda.Nilishawahi kukutana na
huo ubaguzi mala nyingi
Unachosema ni kweli wakati wote wananchi wakiingiliwa na hizo itikadi za kibaguzi hayo ndio matokeo yake,na watu ambao wanapenyeza hizo itikadi ni wahutu ambao wameweza jipenyeza tanzania.
 
Unashindwa kuelewa kidogo.

Unaowasema huko nje wanajulikana ametokea wapi pia alishachukua uraia au kazaliwa hukohuko kama Obama.

Mleta uzi anachosema ni kuwa hawa kwetu wanajipenyeza kijasusi maana yake hawana nia njema.

Think out of box
Hivi unaweza fanya ujasusi tanzania,mwaka mmoja,miwili ....tatu hujakamatwa?watanzania wako vizuri kwenye ujasusi,hebu acheni wasiwasi usio usiokua na ushahidi.
 
Umetumwa kuja kusawazisha sio?! Nani asiyewajua nyie mnacheka usoni ila moyoni mna giza nene sana, tutaishi nanyi kwa akili kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…