DOKEZO Hatari sana: Utapeli unaoenea kwenye biashara ya forex Tanzania

DOKEZO Hatari sana: Utapeli unaoenea kwenye biashara ya forex Tanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Katika miaka ya hivi karibuni, biashara ya Forex imekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa Kitanzania wanaotafuta njia mbadala za kujiongezea kipato. Wakati Forex ni fursa halali kwa wale wenye uelewa na utaalamu wa masoko ya kifedha, inasikitisha kuona jinsi baadhi ya watu wameigeuza kuwa mtandao wa ulaghai, wakitumia ahadi za uongo kuwahadaa watu waliotayari kujitolea kila kitu kwa matumaini ya maisha bora.

Katika uchunguzi huu, tunamchunguza mtu anayejulikana kama Erick John (Instagram: pips_crusher), ambaye anatuhumiwa kwa kuwahadaa watu kwa kutumia biashara ya Forex, na kusababisha hasara kubwa kwa wahanga wake.

Mfumo wa Utapeli wa "PIPS_CRUSHER"

Kesi ya Erick ni mfano wa jinsi matapeli wa Forex wanavyofanya kazi. Mimi kama mhanga wa utapeli hau nimeona iwe ni darasa kwa wengine kwasababu mimi nimeshalipa hiyo gharama.

  1. Ununuzi wa Trading Bots au Expert Advisors (EA) Isiyofanya Kazi
    Mnamo tarehe 11 Desemba 2024, nilinunua mfumo wa biashara ya kiotomatiki (EA) kwa gharama ya Shilingi milioni 3.5 za Kitanzania ili uweze kutrade wakati niko busy na shughuki zingine na pia kuhakikisha kama hizi trading bots zinazotangazwa sana hivi sasa zinafanya kazi kweli. Hii sio bot ya kwanza ninanunua - ni ya 4 hivyo nimekusanya taarifa za kutosha kuhusu ufanyaji kazi wa hizi trading bots ambazo huwa ni ghali sana. Sasa turudi kwa Erick anayejinadi na trading bot yake aliyoipa jina "PIPGHOST EA" Bei yake elekezi ni dola za kimarekani 1400 (sawa na 3,553,270 TZS kwa rate ya siku ya chapisho). Baada ya kulipia (risiti ipo hapa chini) nilipokea file kwenye email yangu na nikaunganisha na account yangu. Tulipigiana simu hadi video call mpaka nikaweza kuiset vizuri. Account yangu ilikuwa na mtaji wa dola za kimarekani 1000 (sawa na 2,538,050 TZS kwa rate ya siku ya chapisho). Niligundua kuwa bot iko slow sana kuchukua faida na mara nyingi kama sio zote trade iliishia njiani na kugeukia hasara ambayo kikomo (Stop Loss) iko mbali. Nafurahi kuwa alithibitisha baadaye kuwa mfumo huo haukuwa ukifanya kazi kama alivyoahidi. Hivyo akaahidi kuleta toleo jipya Januari 2025.
    EA Purchase Receipt-2.jpg
  2. Kulipia Huduma ya VPS Isiyokidhi Viwango
    Katika siku hiyo hiyo, nililipa Dola za Marekani 125 kwa huduma ya VPS moja kwa moja kwake, ambayo ilisemekana ingeendelea kwa miezi miwili. Hii imechangiwa na mimi mwenyewe kutokujua wapi pa kuipata VPS sahihi. Hivyo tuseme nimelipa gharama ya kutokuwa na hiyo taarifa kwasababu sidhani kama VPS inafika bei hiyo kwa miezi 2 tu. Hata hivyo, sikuweza kuendelea kutumia huduma baada ya siku kumi, huku maombi ya msaada kutoka kwa Erick yakipuuzwa.
    Screenshot 2025-01-28 at 4.51.42 PM.png
  3. Ulaghai wa Huduma ya "Account Management"
    Baada ya kutoa malalamiko yangu alishauri kuwa nilipie huduma yake ya kusimamia akaunti yangu ili kurudisha hizo hasara. Bei za huduma hiyo nimeweka hapo chini. Gharama ya kuhudumia akaunti ni kubwa mno hivyo nikamsihi nimpee ada baada ya kupata faida ila akatoa wazo tuweke fedha kwenye akaunti ya pamoja ili afanye biashara mpaka mwisho wa wiki ili niwe na fedha ya kulipia huduma wiki inayofuata. Mnamo tarehe 15 Januari 2025, nlituma Shilingi 795,000 kwa Erick kwa ajili ya uwekezaji katika akaunti ya faida ya pamoja. Erick aliahidi kunishirikisha maelezo ya akaunti na kuripoti faida kufikia tarehe 17 Januari. Ahadi hizo hazikutekelezwa, na mawasiliano yote yalikatwa.
Screenshot 2025-01-28 at 4.53.09 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.49.01 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.49.56 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.50.19 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.50.38 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.51.02 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.51.22 PM.png

Njia Zinazotumiwa na Matapeli

Kama ilivyo kwa matapeli wengine wa Forex, Erick alitumia mbinu zifuatazo:

  • Ahadi za Faida Kubwa na za Haraka: Matapeli huonyesha biashara ya Forex kama njia ya haraka ya kutajirika bila kuhitaji maarifa ya kina.
  • Kuficha Habari Muhimu: Erick alificha taarifa muhimu, kama ukosefu wa ufanisi wa EA na VPS, hadi baada ya kupokea malipo.
  • Kuzuia Mawasiliano: Ili kuepuka majibu, Erick aliwazuia wahanga wake kwenye mitandao ya kijamii na kutangaza habari kupitia akaunti nyingine ambazo hawakuziona.

Athari kwa Wahanga

Wahanga wa utapeli huu si tu wanapoteza fedha zao bali pia wanapoteza muda, matumaini, na imani yao kwa biashara halali kama Forex.

Wito kwa Vyombo vya Sheria na Jamii

Vitendo vya matapeli kama Erick vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Tunatoa wito kwa:

  1. Vyombo vya Sheria: Kufuatilia matapeli hawa kwa kutumia ushahidi unaotolewa na wahanga.
  2. Jamii: Kuwaelimisha watu kuhusu mbinu za utapeli katika Forex ili waweze kuchukua tahadhari.
  3. Wahanga: Kupaza sauti na kushirikiana na vyombo vya sheria kufanikisha haki.

Zingatia​

  • Kaa mbali na mtu anayeahidi faida za haraka na zisizo za kawaida.
  • Kumbuka hakuna anayeruhusiwa kufanya biashara ya uwekezaji bila ya kuwa na leseni.
  • Hakikisha unapata taarifa zote muhimu kuhusu huduma au bidhaa kabla ya kufanya malipo.
  • Uliza vyeti vya uthibitisho na historia ya mtu au kampuni anayejihusisha na biashara yoyote ya uwekezaji nchini kutoka CMSA.

Hitimisho

Ulaghai wa Forex ni tatizo linaloongezeka, na ni jukumu letu kama jamii kulinda watu wasio na hatia dhidi ya matapeli kama Erick. Kupitia uandishi huu, tunatumaini kuwa hatua za haraka zitachukuliwa dhidi yake na wengine wanaofanya vitendo vya aina hii.

Kama una ushahidi au unataka kushiriki hadithi yako, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe au simu. Sote tuna jukumu la kuhakikisha kuwa biashara inakuwa ya uwazi na halali.
Pole sana brother. Kwakweli vijana wengi wa Forex ni matapeli, wengi wanaojinadi mjini kuwa na maisha mazuri sababu ya Forex sio kweli, wengi hupata hayo maisha mazuri kwa kutapeli watu! Hebu fikiria amekusanya hizo pesa zote ulizomtumia kutoka kwa watu wangapi? Maana roughly ni kama TZS 4.2M dah!

Mimi nimeshangaa kwasababu unaonekana upo ready kutake risks za kutumia bots tena kwa pesa mingi tu, na nimeona katika miamala yako umewithdraw USDT kutoka Binance. Sasa kama una elimu kuhusu USDT + any other digital currency si ni afadhali ukafanya copy trading ya futures au spot hapo hapo Binance tena for FREEEEE!!! Maana copy trading ya futures kwenye Binance hata kwa $500 tu ambayo haifiki hata TZS 1.5M ingekupa return nzuri weekly kuliko hata ahadi hewa za huyo jamaa.

Anyways bro, Mungu akusaidie upate namna ya kurecover angalau 50% ya ulichopoteza!
 
Pole sana brother. Kwakweli vijana wengi wa Forex ni matapeli, wengi wanaojinadi mjini kuwa na maisha mazuri sababu ya Forex sio kweli, wengi hupata hayo maisha mazuri kwa kutapeli watu! Hebu fikiria amekusanya hizo pesa zote ulizomtumia kutoka kwa watu wangapi? Maana roughly ni kama TZS 4.2M dah!

Mimi nimeshangaa kwasababu unaonekana upo ready kutake risks za kutumia bots tena kwa pesa mingi tu, na nimeona katika miamala yako umewithdraw USDT kutoka Binance. Sasa kama una elimu kuhusu USDT + any other digital currency si ni afadhali ukafanya copy trading ya futures au spot hapo hapo Binance tena for FREEEEE!!! Maana copy trading ya futures kwenye Binance hata kwa $500 tu ambayo haifiki hata TZS 1.5M ingekupa return nzuri weekly kuliko hata ahadi hewa za huyo jamaa.

Anyways bro, Mungu akusaidie upate namna ya kurecover angalau 50% ya ulichopoteza!
Mkuu unaweza kunielekeza kidogo kuhusu spot trading nimejaribu kupitia youtube tuotorials ila bado sijapata uelewa
 
Katika vitu kichwa changu kimegoma kuelewa ni hizo forex, mwaka jana kuna jamaa yangu kanishawishi sana tuchange tununue bot nikamgomea, ye akanunua ila saiz simsikii tena akiongelea hizo habari.

NB: Mkuu njoo tupige blog huku mtaji ni bando tu!
 
Mkuu unaweza kunielekeza kidogo kuhusu spot trading nimejaribu kupitia youtube tuotorials ila bado sijapata uelewa
Spot trading ni rahisi sana, unachotakiwa kujifunza zaidi ni namna ya kufanya uchambuzi wa currencies ili kuwa na uelewa japo kidogo wa kujua kuwa sarafu fulani kwa ilipofikia ina dalili ya kupanda au kushuka na ndio ufanye maamuzi.

Anganalia mfano kwenye hiyo chart ya sarafu ya AVAX;
  • 24H high (bei ya juu kwa saa 24): $34.19
  • 24H low (bei ya chini kwa saa 24): $31.84
  • Current price (bei ya sasa): $33.21
  • 24H volume: $54M USDT
Hii inamaana kama ulinunua hii sarafu kwa bei ya chini ya leo leo ($31.84) ambayo ilikuwa ni saa 02:30 AM (yaani saa nane usiku "sijui ni alfajiri") na ungeuza kwa bei hata ya sasa ($33.21) ina maana ungekuwa na faida ya $1.37 kwa kila sarafu! Hii ndio maana ya spot trading, yani tunatafuta faida za kila siku, hatu-hold sarafu kwa muda mrefu. Hapo sasa ni wewe kuamua, kama una mtaji mkubwa faida ni kubwa, na kama mtaji mdogo faida ni ndogo pia. Ukiangalia kwenye hiyo chart utaona traders wananunua hadi za $200K (dola laki mbili - TSZ 460M+) kama sisi tunavyonunua maji ya kunywa dukani, aise! Hapo kwa faida ya haraka kwa mahesabu hizo bei za 24H kwa leo, hao jamaa wanapata faida minimum ya TSZ 21M lakini mtaji ni TZS 460M, sasa vijana wa forex wanakuambia ukiwekeza TZS 3M utapata TZS 50M chap chap, na hapo ndipo wengi wanakuja kulia.

All in all, hivyo ndio vitu vya muhimu zaidi kwenye spot trading, kwamba bei ya chini kabisa ya sarafu hiyo kwa siku ilikuwa kiasi gani na bei ya juu kabisa pia ni kiasi gani, kisha unaangalia trading volume yake ya masaa 24 ili ujue ni sarafu inayonunuliwa na kuuzwa na watu wengi au la! Sarafu yenye volume kubwa ni nzuri kwasababu hata ukinunua za $100,000 (dola laki moja - TZS 260M+) utaweza kuuza bila wasi.

Hapo upande wa kulia nilipozungushia box ndipo unachagua sarafu na kuifanyia uchambuzi, dili na sarafu zilizoshuka sana kama unavyoona hapo ni red red tu! Kwasababu kanuni moja ya spot trading ni kununua sarafu ikiwa chini uuze ikiwa juu, sio unanunua ikiwa juu maana ikishuka utapata hasara.

Hayo ni maelezo machache sana brother, endelea kujifunza taratibu tu utaelewa.

1738146681354.png
 
Aisee pole mno na ninakuhurumia hata nashindwa nikusaidiaje Ila mie ni mdau mkubwa mno wa trading,Ila trading ni ya moto mno na ndio mana wengi wanaishia kufundisha wengine, kuwafanya Kama ulivyofanywa na wengine pia wanaishia kuitukana trading kuwa ni utapeli , Ila trading ni real business sema inazingua mpaka hao hao wazungu wenyewe,.
Yaani sijui nikuaambiaje na inaonekana unapenda trading mno na upo na kazi , kiufupi kwa kukusaidia weka hela utt ambalo Kuna low risk low return, trading kujifunza ukaijua huwezi Kama uko poa kihela kwanza,, kuwa traders am sure skills zzake ni sawa na kuwa Tyson,Michael Jordan,Kobe Bryant,tiger wood, Usain bolt, and like sio kirahisi kiivyo
 
Forex ni ngumu hakuna cha bots wala EXpert advisor wala signals zitazofanya utoboe forex.

Mentor wakongwe wenyewe wameshindwa kutoboa kwenye forex trading wanakimbilia kwenye kufundisha wageni ,kuuza signals na kufanya account management yaani hawa weki pesa zao ,bali Wana trade kwa hela za newbies, wanafunzi wao ili wakibahatisha vifaida waga2ane na wanafunzi.

Hivi wew hushtuki kama forex trading ni profitable kwann Kia mtu mzoefu anakimbilia kuwa mentor, account management na kuuza signals why?

NB: KIMBIA KABISA , ACHA FOREX KABLA ITS TOO LTE.

MIMI NMESHA FANYA YOOTE HAYO HADI BOTS NMETUMIA LAKINI SJAFANIKIWA NMELOSE ZAIDI YA 5Millions.
 
Back
Top Bottom