DOKEZO Hatari sana: Utapeli unaoenea kwenye biashara ya forex Tanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Katika miaka ya hivi karibuni, biashara ya Forex imekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa Kitanzania wanaotafuta njia mbadala za kujiongezea kipato. Wakati Forex ni fursa halali kwa wale wenye uelewa na utaalamu wa masoko ya kifedha, inasikitisha kuona jinsi baadhi ya watu wameigeuza kuwa mtandao wa ulaghai, wakitumia ahadi za uongo kuwahadaa watu waliotayari kujitolea kila kitu kwa matumaini ya maisha bora.

Katika uchunguzi huu, tunamchunguza mtu anayejulikana kama Erick John (Instagram: pips_crusher), ambaye anatuhumiwa kwa kuwahadaa watu kwa kutumia biashara ya Forex, na kusababisha hasara kubwa kwa wahanga wake.

Mfumo wa Utapeli wa "PIPS_CRUSHER"

Kesi ya Erick ni mfano wa jinsi matapeli wa Forex wanavyofanya kazi. Mimi kama mhanga wa utapeli hau nimeona iwe ni darasa kwa wengine kwasababu mimi nimeshalipa hiyo gharama.

  1. Ununuzi wa Trading Bots au Expert Advisors (EA) Isiyofanya Kazi
    Mnamo tarehe 11 Desemba 2024, nilinunua mfumo wa biashara ya kiotomatiki (EA) kwa gharama ya Shilingi milioni 3.5 za Kitanzania ili uweze kutrade wakati niko busy na shughuki zingine na pia kuhakikisha kama hizi trading bots zinazotangazwa sana hivi sasa zinafanya kazi kweli. Hii sio bot ya kwanza ninanunua - ni ya 4 hivyo nimekusanya taarifa za kutosha kuhusu ufanyaji kazi wa hizi trading bots ambazo huwa ni ghali sana. Sasa turudi kwa Erick anayejinadi na trading bot yake aliyoipa jina "PIPGHOST EA" Bei yake elekezi ni dola za kimarekani 1400 (sawa na 3,553,270 TZS kwa rate ya siku ya chapisho). Baada ya kulipia (risiti ipo hapa chini) nilipokea file kwenye email yangu na nikaunganisha na account yangu. Tulipigiana simu hadi video call mpaka nikaweza kuiset vizuri. Account yangu ilikuwa na mtaji wa dola za kimarekani 1000 (sawa na 2,538,050 TZS kwa rate ya siku ya chapisho). Niligundua kuwa bot iko slow sana kuchukua faida na mara nyingi kama sio zote trade iliishia njiani na kugeukia hasara ambayo kikomo (Stop Loss) iko mbali. Nafurahi kuwa alithibitisha baadaye kuwa mfumo huo haukuwa ukifanya kazi kama alivyoahidi. Hivyo akaahidi kuleta toleo jipya Januari 2025.
    EA Purchase Receipt-2.jpg
  2. Kulipia Huduma ya VPS Isiyokidhi Viwango
    Katika siku hiyo hiyo, nililipa Dola za Marekani 125 kwa huduma ya VPS moja kwa moja kwake, ambayo ilisemekana ingeendelea kwa miezi miwili. Hii imechangiwa na mimi mwenyewe kutokujua wapi pa kuipata VPS sahihi. Hivyo tuseme nimelipa gharama ya kutokuwa na hiyo taarifa kwasababu sidhani kama VPS inafika bei hiyo kwa miezi 2 tu. Hata hivyo, sikuweza kuendelea kutumia huduma baada ya siku kumi, huku maombi ya msaada kutoka kwa Erick yakipuuzwa.
    Screenshot 2025-01-28 at 4.51.42 PM.png
  3. Ulaghai wa Huduma ya "Account Management"
    Baada ya kutoa malalamiko yangu alishauri kuwa nilipie huduma yake ya kusimamia akaunti yangu ili kurudisha hizo hasara. Bei za huduma hiyo nimeweka hapo chini. Gharama ya kuhudumia akaunti ni kubwa mno hivyo nikamsihi nimpee ada baada ya kupata faida ila akatoa wazo tuweke fedha kwenye akaunti ya pamoja ili afanye biashara mpaka mwisho wa wiki ili niwe na fedha ya kulipia huduma wiki inayofuata. Mnamo tarehe 15 Januari 2025, nlituma Shilingi 795,000 kwa Erick kwa ajili ya uwekezaji katika akaunti ya faida ya pamoja. Erick aliahidi kunishirikisha maelezo ya akaunti na kuripoti faida kufikia tarehe 17 Januari. Ahadi hizo hazikutekelezwa, na mawasiliano yote yalikatwa.
Screenshot 2025-01-28 at 4.53.09 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.49.01 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.49.56 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.50.19 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.50.38 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.51.02 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.51.22 PM.png

Njia Zinazotumiwa na Matapeli

Kama ilivyo kwa matapeli wengine wa Forex, Erick alitumia mbinu zifuatazo:

  • Ahadi za Faida Kubwa na za Haraka: Matapeli huonyesha biashara ya Forex kama njia ya haraka ya kutajirika bila kuhitaji maarifa ya kina.
  • Kuficha Habari Muhimu: Erick alificha taarifa muhimu, kama ukosefu wa ufanisi wa EA na VPS, hadi baada ya kupokea malipo.
  • Kuzuia Mawasiliano: Ili kuepuka majibu, Erick aliwazuia wahanga wake kwenye mitandao ya kijamii na kutangaza habari kupitia akaunti nyingine ambazo hawakuziona.

Athari kwa Wahanga

Wahanga wa utapeli huu si tu wanapoteza fedha zao bali pia wanapoteza muda, matumaini, na imani yao kwa biashara halali kama Forex.

Wito kwa Vyombo vya Sheria na Jamii

Vitendo vya matapeli kama Erick vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Tunatoa wito kwa:

  1. Vyombo vya Sheria: Kufuatilia matapeli hawa kwa kutumia ushahidi unaotolewa na wahanga.
  2. Jamii: Kuwaelimisha watu kuhusu mbinu za utapeli katika Forex ili waweze kuchukua tahadhari.
  3. Wahanga: Kupaza sauti na kushirikiana na vyombo vya sheria kufanikisha haki.

Zingatia​

  • Kaa mbali na mtu anayeahidi faida za haraka na zisizo za kawaida.
  • Kumbuka hakuna anayeruhusiwa kufanya biashara ya uwekezaji bila ya kuwa na leseni.
  • Hakikisha unapata taarifa zote muhimu kuhusu huduma au bidhaa kabla ya kufanya malipo.
  • Uliza vyeti vya uthibitisho na historia ya mtu au kampuni anayejihusisha na biashara yoyote ya uwekezaji nchini kutoka CMSA.

Hitimisho

Ulaghai wa Forex ni tatizo linaloongezeka, na ni jukumu letu kama jamii kulinda watu wasio na hatia dhidi ya matapeli kama Erick. Kupitia uandishi huu, tunatumaini kuwa hatua za haraka zitachukuliwa dhidi yake na wengine wanaofanya vitendo vya aina hii.

Kama una ushahidi au unataka kushiriki hadithi yako, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe au simu. Sote tuna jukumu la kuhakikisha kuwa biashara inakuwa ya uwazi na halali.
Kaka hao ni matapeli kabisa ,how $1000 inakuwa $35,000 within 7 days ? kuna post anasema 100 imekuwa 10000+within 3 hrs .

swali la kujiuliza ,why asiweke yeye $1000 apate $350,000 within 7 days? ,hio $350,000 akiipata hatahitaji tena kuchukua management fees zenu maana anauhakika kutengeneza $4m per year?

sasa mtu anaetengeneza 4m a year anaweza kaa intagram kuchukua management fees yaani akutajirishe wewe?.

forex ni biashara legal kabisa ,ila utapeli ni 90%
 
Forex ni ngumu hakuna cha bots wala EXpert advisor wala signals zitazofanya utoboe forex.

Mentor wakongwe wenyewe wameshindwa kutoboa kwenye forex trading wanakimbilia kwenye kufundisha wageni ,kuuza signals na kufanya account management yaani hawa weki pesa zao ,bali Wana trade kwa hela za newbies, wanafunzi wao ili wakibahatisha vifaida waga2ane na wanafunzi.

Hivi wew hushtuki kama forex trading ni profitable kwann Kia mtu mzoefu anakimbilia kuwa mentor, account management na kuuza signals why?

NB: KIMBIA KABISA , ACHA FOREX KABLA ITS TOO LTE.

MIMI NMESHA FANYA YOOTE HAYO HADI BOTS NMETUMIA LAKINI SJAFANIKIWA NMELOSE ZAIDI YA 5Millions.
Wew ni mpuuzi tu
 
Kama ukishindwa kujifunza kutrade wewe km wewe utaendelea kupigwa daily.kwenye forex bosi na kila kitu ni wewe,ukiona mambo ya signal sijui trading robot ujue unapigwa.Hakuna mtu anayeweza kumake profit ya kutosha akaomba dollars 1000 akufanyie trading,hakuna upendo wa hivyo babulai.Kuna jamaa alikua twitter anajiita erick aliwapiga watu vidola 10 kumi,akampiga hadi sir jef $10 afu akablock na account. Nahisi ndo huyo kaja insta kuwapiga,hakuna trader pale
Upo sahihi. Kwa yoyote anayetarajia kuingia kwenye ulingo wa trading ni vema akafahamu hakuna bot wala mtu wa kukutengenezea pesa sokoni. Usije thubutu kulipia Account management/bot/signals

Shortcuts hua zina madhara mno, ili uweze kuingiza faida kwenye soko la Forex huna budi kutafuta maarifa/elimu sahihi kuhusu biashara hio.

TAHADHARI:
1. ELIMU YA TRADING SI NYEPESI
2. KUPATA MTU WA KUKUPA ELIMU SAHIHI NI CHANGAMOTO
3. PESA PEKEE UNAYOPASWA KUTOA NI KULIPIA MAARIFA NA BAADA YA HAPO NI KULIPIA KWA BROKER (WAKALA) ILI UANZE KUTRADE MWENYEWE KWENYE MT4/MT5 YAKO.
4. TRADING SI KWAAJILI YA KILA MTU ( KAMA HUWEZI KUWEZEKEZA MUDA NA NGUVU ZAKO KUELEWA KIUNDANI HII BIASHARA NASHAURI NI VEMA UKAIOGOPA ZAIDI YA UKOMA)
 
- Baada yaa maombi ya watu wengi nitoe somo kuhusu forex, andiko hili litaelezea kwa undan forex ni nini, uhalisia ukoje na undan wake ambao huezi kuskia kokote

- Kwa kuanza ningependa kutoa disclaimer, huenda maudhui haya yakawa hayaaminiki na wengi ila as long ni uhalisia hayana budi kusomeka kma yalivo! kwa uzoefu wangu wa forex benki kuu basi maudhui haya ndo uhalisia kamili wa forex na unaweza kutumia maudhui haya kama reference kokote, pia nitaelezea uhalisia kwanini haiwezekan kutengeneza pesa kwa kutumia forex bila njia special

Bila kupoteza mda FOREX ni nn, forex ni KITENDO cha kubadilishana SARAFU ni SOKO bali kile kitendo ndo kinaitwa FOR-EX(FOREIGN EXCHANGE)! Forex imeanza mda kidogo kwa kua mataifa mengi yalianza kubadilishana pesa miaka ya nyuma baada ya idelogy za uchumi kuanza mfano mtu alietoka uingereza angeweza kuja kununua nguo india kwa makubaliano maalum ya kiasi gan ni sahihi, Misingi hii ndo inayotumika mpaka leo katika FOREX kwa mfano: kwa wale ambao wanavuka mipaka kwa usafiri wa barabaran hukutana na madalali wa kubadilisha sarafu na kila machinga ana rate yake, unapoenda kubadilishana pesa na huyo dalali basi apo umefanya forex TRANSACTION: shika ili neno TRANSACTION lina umuhimu mbelen

Kwanini forex ipo? well forex ipo kwa lengo kubwa kama MUONGOZO wa ubadilishaji pesa endapo mtu atapenda kufanya biashara na nchi husika, FOREX inafanyika 100% na benki kuu na hakuna mtu mwingine anaruhusiwa kufanyia biashara ya forex pesa ya nchi husika, unaweza kua na maswali vp kuhusu byuro de change, Hao wanafanya offline transactions kama wale wa kwenye borders, na wanafanya biashara kwa mitaji midogo midogo, kwa mfano unaweza kwenda byuro de change ukabadilisha mil 10, transaction hii haina athari yoyote kwa sababu ni kiasi kidogo sana, offline transactions zinaweza kua na athari pale zitakapofanyika katika BLACK MARKET kwa mfano kunaweza tokea vikundi ama watu wanauza kiasi kikubwa kwa siri bila muongozo, hii hutokana sana kama kuna uhaba wa sarafu flan, kwa mfano kukiwa na uhaba wa dola basi kwakua uhitaji wa dola nchini upogo always atapandisha kwa kiasi anachoona mtu atakubali, kwa mfano:

1740049314972.png

tukichukula mfano wa apo juu, dola 1 ni 2600 kukiwa na uhaba wa dola, basi mtu anaweza kuuza mpaka 3000 na akauza vizuri ukizingatia nchi yetu inapokea wageni wengi

najua wengi mna maswali kuhusu wale wa mt4/5, tutafika uko msijali kwa sababu tuelewe forex yenyewe halisi mpaka tunafika uko somo litakua easy, kwakua tumesema forex ipo kama mwongozo basi benki kuu inategemea biashara zote za forex zifanyike kupitia kiasi iki, ukiangalia huo mfano wa google unaweza kuona price ni 2600Tsh, hio ni price ya kufanyia biashara ila kuna price inaitwa FLOATING PRICE kwa mfano nikienda kwenye tovuti ya benki kuu, bei ni

1740049634429.png

Unaweza kujiuliza kwanini tunazohizi bei kama kila mtu anaweza jipangia, jibu ni rahisi uchumi wa nchi husika na jiran zote zitakufa, kwa sababu bei hizi sio bei halisi inayoendana na uchumi bali ina mahesbu yake jinsi ya kuipata, pesa yako iko strong haiimaanishi una uchumi mkubwa hapana bali ina mahesabu yake namna ya kuipata na kuna levels haitakiwi kuvuka, kwa mfano tuchukulia USD/TSH kama mfano:

ikitokea dola inatumika sana nchini kuna uhitaji umetokea mfano extra $1B inahitajika na mabenki ya kawaida wamekauka kufikia $1B basi banki kuu itanunua Tsh kutoka kwenye mabenki na kuwapa $2B, na itaendelea kununua tsh kwa mda kiasi mpaka uwiano upatikane, kwa mfano $2B ni zaidi ya mahitaji ya benki ndogo ivo wanaotaka tsh watakuta kuna upungufu wataomba tsh zaidi na tsh itapanda kwan rate mpya itawekwa, scenario hizi hutokea na kusababisha kitu kama hiki:
1740050310818.png

maaana yake kuna mtu kafanya uuzaji mkubwa mmoja, kitu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba! ikitokea Tsh inaenda mbio sana nkimaanisha ikitokea tsh inatishia nguvu dola basi benki kuu wanatakiwa kuirudisha Tsh chini, same same ikitokea dola inapanda sana benki kuu wanatakiwa kuirudisa chini.

unaweza kuuliza kwann ilihali inaonekana ni manufaa kwa tsh kua na nguvu zaidi ya dola: kwa mfano leo dola 1 ni tsh 2600, kesho tumeamka pap dola moja ni tsh 100, maaana yake nn!
Maana yake ni wote unaofanya biashara nao nje ya nchi mfano rwanda alikua ananunua maindi tanzania ya $100 anapata gunia 10, basi sasa anatakiwa kuja na $1000 kununua kiasi kile kile, ivo basi kuepuka haya benki kuu inatakiwa kushusha tsh kidogo ikae stable, dola ikipanda yenyewe kama yenyewe sio issue sana kwan inapanda against nchi zote kwahio bado ukija kubadilisha kwa tanzania utapata same same Tsh!

tuje sasa kwa wale wa mt4, sasa hawa wao wanaumia mawakala ama broka kufanya (BETTING) ya bei halisi, mfano ukideposit dola zako $100 kwa broka ukasema nataka kutumia GBP/USD maaana yake una USD unataka kupewa GBP means GBP ikipanda ukirudisha dola unapata dola nyingi zaidi ya ulizodeposit, making a profit, kwanini nimesema betting

kwa sababu zile pesa anachukua broka anakaa nazo ukiwin basi anachukua pesa za walioloose anakupa wewe, same same ukiloose pesa yako anachukua anapewa aliepata, hakuna kitu kama kuingia sokoni kwa sababu hakuna trading yoyote inafanyika, when you press buy broka atakupa PERPETUAL CONTRACT kwa kiswahili MKEKA, likewise kwa gold, oil zote izi ni mikeka hakuna sehem broka atapeleka pesa yako kwa sababu forex sio soko na halipo pesa itabaki kwake

kwanini unaloose kwenye betting forex: reason kubwa kwanini unaloose kwenye forex ni kwa sababu unasoma charts,
1740051162446.png

pair zozote zilizopo kwa broka ni exchange halisi ya pesa kwenye nchi husika na sio thoughts of candles, kwa mfano unaweza kua na chart kama hii
1740051290707.png

kwa kua ulifundishwa matango pori wewe utaona kama ni mda wa kusell price itashuka bila kuelewa price hizi znaendna na sera za benki kuu moja kwa moja ukiwaza kusell benki kuu wanaona ni mda wa kupandisha zaidi pesa yetu ama kushusha, wapo wanaoskiliza news za benki kuu kabla ya kufanya trades but forex is complex kwa sababu kitakachodetermine price ni average summary ya transactions, yupo mtu anaweza kuja kubadilisha $100M anataka kuagiza magari nje ila hawa huezi kuwaskia kwenye news,

itoshe kusema ulimwengu uliwadanganya you can predict price movement kwa charts, sasa basi unaweza jiuliza tutumie njia gan kupata faida, mpaka sasa ni njia mbili tu za uhakika unaweza tengeneza pesa kwenye financial markets
1) LUCK
2) High frequency trading (HFT)

ili kuelewa HFT unatakiwa kuelewa financial markets znafanyaje kazi, ukitrade forex kwa broka maaana yake ukiweka buy basi yeye ameweka sell, unabet one to one na broka kama vile unavobet spot pesa ukiwin pesa inatoka kwenye kampuni
ila kitu usichokijua TRADING ni fani kabisa mtu anasomea anaenda ofisini asubui anarudi jioni, ili sasa kuelewa HFT unatakiwa kuelewa jinsi trading inafanya kazi

tuchukulie mfano DSE(Soko la Hisa Dar es salaam) ukinunua hisa 1 ya CRDB pale hanunui kutoka CRDB bali unanunua kutoka kwa mtu anaeuza hisa, yaani kama hakuna muuzaaji huezi pata hio hisa na muuzaji sio CRDB bali ni mtu mmoja mmoja, so broka anapokea oda zote anetaka kuuza anapewa tsh zake na anaenunua anapewa hisa zake, kitendo hiki kinaitwa (LIQUIDITY) kampuni zenye liquidity nzuri ni rahsi kupata mnunuaji na muuzaji apo apo na lazima broka akupe status inasema FULLY FILLED kama hazikupatikana zote utapewa PARTIALLY FILLED, same same kama binance na exchanges zingine, sasa basi kwa soko lenye liquidity nzuri kama New york stock exchange kila sekunde kuna wauuzaji wa mamilioni ya share na wanunuaji, hivo sasa HFT ni program ya computer unaitengeneza kazi yake ni kuzinunua hizi hisa na kuziuza haraka sana ndan ya sekunde moja unaweza kufanya biashara 1000 za kuuza na kununua, kwa kua kwenye hio sekunde price imesogea kidogo sana basi faida yako inakua visenti vidogo vidogo but as long umefanya nyingi basi mwisho wa sku adds up na kupata faida kubwa

Kwa mfano yapo makampuni yanaojulikana kaama CITADEL faida yao ni around kila sekunde hua ni $70
 
- Baada yaa maombi ya watu wengi nitoe somo kuhusu forex, andiko hili litaelezea kwa undan forex ni nini, uhalisia ukoje na undan wake ambao huezi kuskia kokote

- Kwa kuanza ningependa kutoa disclaimer, huenda maudhui haya yakawa hayaaminiki na wengi ila as long ni uhalisia hayana budi kusomeka kma yalivo! kwa uzoefu wangu wa forex benki kuu basi maudhui haya ndo uhalisia kamili wa forex na unaweza kutumia maudhui haya kama reference kokote, pia nitaelezea uhalisia kwanini haiwezekan kutengeneza pesa kwa kutumia forex bila njia special

View attachment 3242788
tukichukula mfano wa apo juu, dola 1 ni 2600 kukiwa na uhaba wa dola, basi mtu anaweza kuuza mpaka 3000 na akauza vizuri ukizingatia nchi yetu inapokea wageni wengi

View attachment 3242803

ikitokea dola inatumika sana nchini kuna uhitaji umetokea mfano extra $1B inahitajika na mabenki ya kawaida wamekauka kufikia $1B basi banki kuu itanunua Tsh kutoka kwenye mabenki na kuwapa $2B, na itaendelea kununua tsh kwa mda kiasi mpaka uwiano upatikane, kwa mfano $2B ni zaidi ya mahitaji ya benki ndogo ivo wanaotaka tsh watakuta kuna upungufu wataomba tsh zaidi na tsh itapanda kwan rate mpya itawekwa, scenario hizi hutokea na kusababisha kitu kama hiki:
View attachment 3242812

maaana yake kuna mtu kafanya uuzaji mkubwa mmoja, kitu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba! ikitokea Tsh inaenda mbio sana nkimaanisha ikitokea tsh inatishia nguvu dola basi benki kuu wanatakiwa kuirudisha Tsh chini, same same ikitokea dola inapanda sana benki kuu wanatakiwa kuirudisa chini.

unaweza kuuliza kwann ilihali inaonekana ni manufaa kwa tsh kua na nguvu zaidi ya dola: kwa mfano leo dola 1 ni tsh 2600, kesho tumeamka pap dola moja ni tsh 100, maaana yake nn!
Maana yake ni wote unaofanya biashara nao nje ya nchi mfano rwanda alikua ananunua maindi tanzania ya $100 anapata gunia 10, basi sasa anatakiwa kuja na $1000 kununua kiasi kile kile, ivo basi kuepuka haya benki kuu inatakiwa kushusha tsh kidogo ikae stable, dola ikipanda yenyewe kama yenyewe sio issue sana kwan inapanda against nchi zote kwahio bado ukija kubadilisha kwa tanzania utapata same same Tsh!

kwa sababu zile pesa anachukua broka anakaa nazo ukiwin basi anachukua pesa za walioloose anakupa wewe, same same ukiloose pesa yako anachukua anapewa aliepata, hakuna kitu kama kuingia sokoni kwa sababu hakuna trading yoyote inafanyika, when you press buy broka atakupa PERPETUAL CONTRACT kwa kiswahili MKEKA, likewise kwa gold, oil zote izi ni mikeka hakuna sehem broka atapeleka pesa yako kwa sababu forex sio soko na halipo pesa itabaki kwake

kwanini unaloose kwenye betting forex: reason kubwa kwanini unaloose kwenye forex ni kwa sababu unasoma charts,
View attachment 3242824

pair zozote zilizopo kwa broka ni exchange halisi ya pesa kwenye nchi husika na sio thoughts of candles, kwa mfano unaweza kua na chart kama hii
View attachment 3242825

kwa kua ulifundishwa matango pori wewe utaona kama ni mda wa kusell price itashuka bila kuelewa price hizi znaendna na sera za benki kuu moja kwa moja ukiwaza kusell benki kuu wanaona ni mda wa kupandisha zaidi pesa yetu ama kushusha, wapo wanaoskiliza news za benki kuu kabla ya kufanya trades but forex is complex kwa sababu kitakachodetermine price ni average summary ya transactions, yupo mtu anaweza kuja kubadilisha $100M anataka kuagiza magari nje ila hawa huezi kuwaskia kwenye news,

itoshe kusema ulimwengu uliwadanganya you can predict price movement kwa charts, sasa basi unaweza jiuliza tutumie njia gan kupata faida, mpaka sasa ni njia mbili tu za uhakika unaweza tengeneza pesa kwenye financial markets
1) LUCK
2) High frequency trading (HFT)

ila kitu usichokijua TRADING ni fani kabisa mtu anasomea anaenda ofisini asubui anarudi jioni, ili sasa kuelewa HFT unatakiwa kuelewa jinsi trading inafanya kazi

Kwa mfano yapo makampuni yanaojulikana kaama CITADEL faida yao ni around kila sekunde hua ni $70
Wewe jamaa unataka watu wote wakuone kuwa ndo kipimo Cha uelewa kuhusu forex trading humu ndani kuna watu Kama Mwl.RCT , Crimea na wengine wanaielewa forex na kuiishi kila siku.

Ww umejaa porojo mfu.
 
sasa mm na wewe nani anaijua forex halisi, hujawahi ata kukaa pale BOT forex unaoijua wewe ni kamari
 
Katika miaka ya hivi karibuni, biashara ya Forex imekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa Kitanzania wanaotafuta njia mbadala za kujiongezea kipato. Wakati Forex ni fursa halali kwa wale wenye uelewa na utaalamu wa masoko ya kifedha, inasikitisha kuona jinsi baadhi ya watu wameigeuza kuwa mtandao wa ulaghai, wakitumia ahadi za uongo kuwahadaa watu waliotayari kujitolea kila kitu kwa matumaini ya maisha bora.

Katika uchunguzi huu, tunamchunguza mtu anayejulikana kama Erick John (Instagram: pips_crusher), ambaye anatuhumiwa kwa kuwahadaa watu kwa kutumia biashara ya Forex, na kusababisha hasara kubwa kwa wahanga wake.

Mfumo wa Utapeli wa "PIPS_CRUSHER"

Kesi ya Erick ni mfano wa jinsi matapeli wa Forex wanavyofanya kazi. Mimi kama mhanga wa utapeli hau nimeona iwe ni darasa kwa wengine kwasababu mimi nimeshalipa hiyo gharama.

  1. Ununuzi wa Trading Bots au Expert Advisors (EA) Isiyofanya Kazi
    Mnamo tarehe 11 Desemba 2024, nilinunua mfumo wa biashara ya kiotomatiki (EA) kwa gharama ya Shilingi milioni 3.5 za Kitanzania ili uweze kutrade wakati niko busy na shughuki zingine na pia kuhakikisha kama hizi trading bots zinazotangazwa sana hivi sasa zinafanya kazi kweli. Hii sio bot ya kwanza ninanunua - ni ya 4 hivyo nimekusanya taarifa za kutosha kuhusu ufanyaji kazi wa hizi trading bots ambazo huwa ni ghali sana. Sasa turudi kwa Erick anayejinadi na trading bot yake aliyoipa jina "PIPGHOST EA" Bei yake elekezi ni dola za kimarekani 1400 (sawa na 3,553,270 TZS kwa rate ya siku ya chapisho). Baada ya kulipia (risiti ipo hapa chini) nilipokea file kwenye email yangu na nikaunganisha na account yangu. Tulipigiana simu hadi video call mpaka nikaweza kuiset vizuri. Account yangu ilikuwa na mtaji wa dola za kimarekani 1000 (sawa na 2,538,050 TZS kwa rate ya siku ya chapisho). Niligundua kuwa bot iko slow sana kuchukua faida na mara nyingi kama sio zote trade iliishia njiani na kugeukia hasara ambayo kikomo (Stop Loss) iko mbali. Nafurahi kuwa alithibitisha baadaye kuwa mfumo huo haukuwa ukifanya kazi kama alivyoahidi. Hivyo akaahidi kuleta toleo jipya Januari 2025.
    EA Purchase Receipt-2.jpg
  2. Kulipia Huduma ya VPS Isiyokidhi Viwango
    Katika siku hiyo hiyo, nililipa Dola za Marekani 125 kwa huduma ya VPS moja kwa moja kwake, ambayo ilisemekana ingeendelea kwa miezi miwili. Hii imechangiwa na mimi mwenyewe kutokujua wapi pa kuipata VPS sahihi. Hivyo tuseme nimelipa gharama ya kutokuwa na hiyo taarifa kwasababu sidhani kama VPS inafika bei hiyo kwa miezi 2 tu. Hata hivyo, sikuweza kuendelea kutumia huduma baada ya siku kumi, huku maombi ya msaada kutoka kwa Erick yakipuuzwa.
    Screenshot 2025-01-28 at 4.51.42 PM.png
  3. Ulaghai wa Huduma ya "Account Management"
    Baada ya kutoa malalamiko yangu alishauri kuwa nilipie huduma yake ya kusimamia akaunti yangu ili kurudisha hizo hasara. Bei za huduma hiyo nimeweka hapo chini. Gharama ya kuhudumia akaunti ni kubwa mno hivyo nikamsihi nimpee ada baada ya kupata faida ila akatoa wazo tuweke fedha kwenye akaunti ya pamoja ili afanye biashara mpaka mwisho wa wiki ili niwe na fedha ya kulipia huduma wiki inayofuata. Mnamo tarehe 15 Januari 2025, nlituma Shilingi 795,000 kwa Erick kwa ajili ya uwekezaji katika akaunti ya faida ya pamoja. Erick aliahidi kunishirikisha maelezo ya akaunti na kuripoti faida kufikia tarehe 17 Januari. Ahadi hizo hazikutekelezwa, na mawasiliano yote yalikatwa.
Screenshot 2025-01-28 at 4.53.09 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.49.01 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.49.56 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.50.19 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.50.38 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.51.02 PM.png

Screenshot 2025-01-23 at 4.51.22 PM.png

Njia Zinazotumiwa na Matapeli

Kama ilivyo kwa matapeli wengine wa Forex, Erick alitumia mbinu zifuatazo:

  • Ahadi za Faida Kubwa na za Haraka: Matapeli huonyesha biashara ya Forex kama njia ya haraka ya kutajirika bila kuhitaji maarifa ya kina.
  • Kuficha Habari Muhimu: Erick alificha taarifa muhimu, kama ukosefu wa ufanisi wa EA na VPS, hadi baada ya kupokea malipo.
  • Kuzuia Mawasiliano: Ili kuepuka majibu, Erick aliwazuia wahanga wake kwenye mitandao ya kijamii na kutangaza habari kupitia akaunti nyingine ambazo hawakuziona.

Athari kwa Wahanga

Wahanga wa utapeli huu si tu wanapoteza fedha zao bali pia wanapoteza muda, matumaini, na imani yao kwa biashara halali kama Forex.

Wito kwa Vyombo vya Sheria na Jamii

Vitendo vya matapeli kama Erick vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Tunatoa wito kwa:

  1. Vyombo vya Sheria: Kufuatilia matapeli hawa kwa kutumia ushahidi unaotolewa na wahanga.
  2. Jamii: Kuwaelimisha watu kuhusu mbinu za utapeli katika Forex ili waweze kuchukua tahadhari.
  3. Wahanga: Kupaza sauti na kushirikiana na vyombo vya sheria kufanikisha haki.

Zingatia​

  • Kaa mbali na mtu anayeahidi faida za haraka na zisizo za kawaida.
  • Kumbuka hakuna anayeruhusiwa kufanya biashara ya uwekezaji bila ya kuwa na leseni.
  • Hakikisha unapata taarifa zote muhimu kuhusu huduma au bidhaa kabla ya kufanya malipo.
  • Uliza vyeti vya uthibitisho na historia ya mtu au kampuni anayejihusisha na biashara yoyote ya uwekezaji nchini kutoka CMSA.

Hitimisho

Ulaghai wa Forex ni tatizo linaloongezeka, na ni jukumu letu kama jamii kulinda watu wasio na hatia dhidi ya matapeli kama Erick. Kupitia uandishi huu, tunatumaini kuwa hatua za haraka zitachukuliwa dhidi yake na wengine wanaofanya vitendo vya aina hii.

Kama una ushahidi au unataka kushiriki hadithi yako, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe au simu. Sote tuna jukumu la kuhakikisha kuwa biashara inakuwa ya uwazi na halali.
Yani simple logic.
Kama mtu anaweza trade akatengeneza faida hiyo kwanini ahangaike na wewe kukuuzia mara bot mara afanye akaunti management mgawane faida.
Yani hapo ndipo hao ma fx guru wa insta na x nawaonaga matapeli.
 
Utapeli kila sehem
 
Jamaa yuko fasta ukikoment kidg tu negative kuhusu utapeli wake unakula kufuli
 
Hiyo pesa ungebetia odd 2 tu mara tatu saa hii ungekuwa na account iliyotuna. Hivi kabisa huyo erick aache kujitengenezea mamilioni ila kwasababu ana roho nzuri sana anakwambia wewe umpe pesa zako akutengenezee mamilioni kwa malipo?🤔

Mbona hii haimake sense. Ni sawa na uwe na mkeo then atokee mwanaume aseme yeye atamsomesha mtoto wako,atampatia matunzo mkeo,atampeleka na kumrudisha kazini kwa gari lake halafu anakwambia wewe kuwa anafanya hivyo kwasababu ya ujirani mwema,wewe haushituki kabisa unakenua meno tu hapo kama farasi mwenye furaha?🤔

Huyo ni tapeli,ungana na wenzako hata 5 au 10 muende kumfungulia mashitaka ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Na mtafute wakili mzuri atakae wawakilisha kwenye hii kesi. Atawalipa na fidia juu mpuuzi kabisa huyo erick.

Hizo pesa umempa ni nyingi sana kukubalia zitoweke tu.
 
Pole sana brother. Kwakweli vijana wengi wa Forex ni matapeli, wengi wanaojinadi mjini kuwa na maisha mazuri sababu ya Forex sio kweli, wengi hupata hayo maisha mazuri kwa kutapeli watu! Hebu fikiria amekusanya hizo pesa zote ulizomtumia kutoka kwa watu wangapi? Maana roughly ni kama TZS 4.2M dah!

Mimi nimeshangaa kwasababu unaonekana upo ready kutake risks za kutumia bots tena kwa pesa mingi tu, na nimeona katika miamala yako umewithdraw USDT kutoka Binance. Sasa kama una elimu kuhusu USDT + any other digital currency si ni afadhali ukafanya copy trading ya futures au spot hapo hapo Binance tena for FREEEEE!!! Maana copy trading ya futures kwenye Binance hata kwa $500 tu ambayo haifiki hata TZS 1.5M ingekupa return nzuri weekly kuliko hata ahadi hewa za huyo jamaa.

Anyways bro, Mungu akusaidie upate namna ya kurecover angalau 50% ya ulichopoteza!
Mwanangu unaonekana una uchawi fulani wa uchumi,hebu nigaie na mimi hats hirizi mbili nikawange niwe tajiri.
 
Haha! Unajua brother haya ni mambo ya ku-take risk kweli kweli, ukimpa mtu hirizi halafu upepo ukamuendea kushoto ataona ulimpatia hirizi ya kumloga na sio kumsaidia
 
sasa vijana wa forex wanakuambia ukiwekeza TZS 3M utapata TZS 50M chap chap, na hapo ndipo wengi wanakuja kulia.
Kama.biashara imenyooka hivyo kama unavyoielezea mtu anakuja kulizwa namna? Hebu fafanua vizuri namna mtu anavyolizwa! Kama bei imeshuka ukaamua kui-hold hiyo Sarafu yako kuna ubaya gani?
 
Naamini unazungumzia hizi crypto na sio forex, okay.

Kwenye crypto kuna faida lakini sio kwamba ndio faida tu pasipo hasara pia, hapana! Mtu anaweza kuumia kwa kununua sarafu mbaya, yaani sarafu yenye liquidity ndogo au isiyo na roadmap nzuri. Na ndio maana kwenye andiko langu nimesisitizia ku-deal na sarafu zenye liquidity kubwa na trading volume kubwa ili ukifia target yako ya faida uuze mara moja pasipo kusua sua.

Ku-hold sarafu sio mbaya, ila muhimu ni kuzingatia niliyokueleza ambayo ni liquidity au roadmap. Ngoja nikupe mfano mzuri; Tarehe 18/01/2025 $TRUMP coin ilikuwa ni $6.24 sasa watu wengi sana walinunua sababu ya ushawishi mkubwa wa Trump, ilipofika kesho yake tarehe 19/01/2025 $TRUMP moja ilifika $75.35 na trading volume yake ilikuwa ni $39B, kuna watu walikuwa mabilionea aise! Unaweza search habari ya hiyo coin ilivyowapa watu utajiri. Lakini kuanzia tarehe 22/01/2025 ilianza kushuka na kufikia $44.19 kwahiyo kama kawaida watu wengi wakaanza kununua wakiamini itapanda tena! Bro, iliendelea kushuka hadi kufikia bei ya leo ya $12.20 kwa $TRUMP moja kuishia kuwaliza watu wengi. Ukiangalia haka ka-story ni kwamba ushawishi wa Trump ndio uliofanya watu wakanunua hii memecoin ya $TRUMP lakini haina roadmap yoyote na ndio maana ilikuwa rahisi kushuka sana baada ya wahusika kuuza kiasi kikubwa cha sarafu hiyo na kununua Bitcoin (unaweza search kuhusu habari hii google utaona makala nyingi sana) kwahiyo lengo la kukuambia kuhusu hii coin ni kukuonyesha kuwa ku-hold sio vibaya lakini sikuzote hold sarafu yenye roadmap nzuri, liquidity, trading volume, na hata ikiwezekana iwe ni utility coin/token. Kwasababusarafu yenye sifa hizo sio rahisi kushuka sana, na hata ikishuka sana haitochukua muda kurudi kwenye nafasi yake na hata juu zaidi, ila kwa memecoin kama hiyo $TRUMP mara nyingi upanda kwa ushawishi wa mhusika tu, muda mchache badae inapoteza thamani.

Mimi crypto imenibadilishia maisha, lakini safari yake haikuwa rahisi hata kidogo kwasababu niliwahi kukutana na hasara ambazo sikuwahi kutegemea kwenye maisha yangu! Lakini ni kwasababu nilikuwa sina maarifa, unajua nilikuwa nanunua coin yoyote na muda wowote kwa ushawishi wa kijinga tu, lakini badae nilituliza kichwa na kuanza kujifunza, nilianza kudeal na crypto mwaka 2016, nilianza kupata faida kwenye crypto mwaka 2019 bro! All in all, crypto ni kama biashara za kawaida tu maana kuna faida na hasara pia, ila ukiamua kuwa serious na kujifunza unaweza punguza hasara na kuzidisha faida.
 
Watu wa Forex,Mwamposaa,demu aliyepata mbaba chuo na Forever living products kamwe hawashauiriki..
Nakumbuka mdada wa forever pale sinza miaka zaidi ya 10 imepita, aliniita nikaenda kwenye kambi yao ya networking nikamsikiliza, nikamsikiliza kwa makini. Baadae nikamwita kwangu. Nikamla biashara ikaishia hapo
 
Back
Top Bottom