DOKEZO Hatari sana: Utapeli unaoenea kwenye biashara ya forex Tanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pole sana brother. Kwakweli vijana wengi wa Forex ni matapeli, wengi wanaojinadi mjini kuwa na maisha mazuri sababu ya Forex sio kweli, wengi hupata hayo maisha mazuri kwa kutapeli watu! Hebu fikiria amekusanya hizo pesa zote ulizomtumia kutoka kwa watu wangapi? Maana roughly ni kama TZS 4.2M dah!

Mimi nimeshangaa kwasababu unaonekana upo ready kutake risks za kutumia bots tena kwa pesa mingi tu, na nimeona katika miamala yako umewithdraw USDT kutoka Binance. Sasa kama una elimu kuhusu USDT + any other digital currency si ni afadhali ukafanya copy trading ya futures au spot hapo hapo Binance tena for FREEEEE!!! Maana copy trading ya futures kwenye Binance hata kwa $500 tu ambayo haifiki hata TZS 1.5M ingekupa return nzuri weekly kuliko hata ahadi hewa za huyo jamaa.

Anyways bro, Mungu akusaidie upate namna ya kurecover angalau 50% ya ulichopoteza!
 
Mkuu unaweza kunielekeza kidogo kuhusu spot trading nimejaribu kupitia youtube tuotorials ila bado sijapata uelewa
 
Katika vitu kichwa changu kimegoma kuelewa ni hizo forex, mwaka jana kuna jamaa yangu kanishawishi sana tuchange tununue bot nikamgomea, ye akanunua ila saiz simsikii tena akiongelea hizo habari.

NB: Mkuu njoo tupige blog huku mtaji ni bando tu!
 
Mkuu unaweza kunielekeza kidogo kuhusu spot trading nimejaribu kupitia youtube tuotorials ila bado sijapata uelewa
Spot trading ni rahisi sana, unachotakiwa kujifunza zaidi ni namna ya kufanya uchambuzi wa currencies ili kuwa na uelewa japo kidogo wa kujua kuwa sarafu fulani kwa ilipofikia ina dalili ya kupanda au kushuka na ndio ufanye maamuzi.

Anganalia mfano kwenye hiyo chart ya sarafu ya AVAX;
  • 24H high (bei ya juu kwa saa 24): $34.19
  • 24H low (bei ya chini kwa saa 24): $31.84
  • Current price (bei ya sasa): $33.21
  • 24H volume: $54M USDT
Hii inamaana kama ulinunua hii sarafu kwa bei ya chini ya leo leo ($31.84) ambayo ilikuwa ni saa 02:30 AM (yaani saa nane usiku "sijui ni alfajiri") na ungeuza kwa bei hata ya sasa ($33.21) ina maana ungekuwa na faida ya $1.37 kwa kila sarafu! Hii ndio maana ya spot trading, yani tunatafuta faida za kila siku, hatu-hold sarafu kwa muda mrefu. Hapo sasa ni wewe kuamua, kama una mtaji mkubwa faida ni kubwa, na kama mtaji mdogo faida ni ndogo pia. Ukiangalia kwenye hiyo chart utaona traders wananunua hadi za $200K (dola laki mbili - TSZ 460M+) kama sisi tunavyonunua maji ya kunywa dukani, aise! Hapo kwa faida ya haraka kwa mahesabu hizo bei za 24H kwa leo, hao jamaa wanapata faida minimum ya TSZ 21M lakini mtaji ni TZS 460M, sasa vijana wa forex wanakuambia ukiwekeza TZS 3M utapata TZS 50M chap chap, na hapo ndipo wengi wanakuja kulia.

All in all, hivyo ndio vitu vya muhimu zaidi kwenye spot trading, kwamba bei ya chini kabisa ya sarafu hiyo kwa siku ilikuwa kiasi gani na bei ya juu kabisa pia ni kiasi gani, kisha unaangalia trading volume yake ya masaa 24 ili ujue ni sarafu inayonunuliwa na kuuzwa na watu wengi au la! Sarafu yenye volume kubwa ni nzuri kwasababu hata ukinunua za $100,000 (dola laki moja - TZS 260M+) utaweza kuuza bila wasi.

Hapo upande wa kulia nilipozungushia box ndipo unachagua sarafu na kuifanyia uchambuzi, dili na sarafu zilizoshuka sana kama unavyoona hapo ni red red tu! Kwasababu kanuni moja ya spot trading ni kununua sarafu ikiwa chini uuze ikiwa juu, sio unanunua ikiwa juu maana ikishuka utapata hasara.

Hayo ni maelezo machache sana brother, endelea kujifunza taratibu tu utaelewa.

 
Aisee pole mno na ninakuhurumia hata nashindwa nikusaidiaje Ila mie ni mdau mkubwa mno wa trading,Ila trading ni ya moto mno na ndio mana wengi wanaishia kufundisha wengine, kuwafanya Kama ulivyofanywa na wengine pia wanaishia kuitukana trading kuwa ni utapeli , Ila trading ni real business sema inazingua mpaka hao hao wazungu wenyewe,.
Yaani sijui nikuaambiaje na inaonekana unapenda trading mno na upo na kazi , kiufupi kwa kukusaidia weka hela utt ambalo Kuna low risk low return, trading kujifunza ukaijua huwezi Kama uko poa kihela kwanza,, kuwa traders am sure skills zzake ni sawa na kuwa Tyson,Michael Jordan,Kobe Bryant,tiger wood, Usain bolt, and like sio kirahisi kiivyo
 
Forex ni ngumu hakuna cha bots wala EXpert advisor wala signals zitazofanya utoboe forex.

Mentor wakongwe wenyewe wameshindwa kutoboa kwenye forex trading wanakimbilia kwenye kufundisha wageni ,kuuza signals na kufanya account management yaani hawa weki pesa zao ,bali Wana trade kwa hela za newbies, wanafunzi wao ili wakibahatisha vifaida waga2ane na wanafunzi.

Hivi wew hushtuki kama forex trading ni profitable kwann Kia mtu mzoefu anakimbilia kuwa mentor, account management na kuuza signals why?

NB: KIMBIA KABISA , ACHA FOREX KABLA ITS TOO LTE.

MIMI NMESHA FANYA YOOTE HAYO HADI BOTS NMETUMIA LAKINI SJAFANIKIWA NMELOSE ZAIDI YA 5Millions.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…