DOKEZO Hatari sana: Utapeli unaoenea kwenye biashara ya forex Tanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kaka hao ni matapeli kabisa ,how $1000 inakuwa $35,000 within 7 days ? kuna post anasema 100 imekuwa 10000+within 3 hrs .

swali la kujiuliza ,why asiweke yeye $1000 apate $350,000 within 7 days? ,hio $350,000 akiipata hatahitaji tena kuchukua management fees zenu maana anauhakika kutengeneza $4m per year?

sasa mtu anaetengeneza 4m a year anaweza kaa intagram kuchukua management fees yaani akutajirishe wewe?.

forex ni biashara legal kabisa ,ila utapeli ni 90%
 
Wew ni mpuuzi tu
 
Upo sahihi. Kwa yoyote anayetarajia kuingia kwenye ulingo wa trading ni vema akafahamu hakuna bot wala mtu wa kukutengenezea pesa sokoni. Usije thubutu kulipia Account management/bot/signals

Shortcuts hua zina madhara mno, ili uweze kuingiza faida kwenye soko la Forex huna budi kutafuta maarifa/elimu sahihi kuhusu biashara hio.

TAHADHARI:
1. ELIMU YA TRADING SI NYEPESI
2. KUPATA MTU WA KUKUPA ELIMU SAHIHI NI CHANGAMOTO
3. PESA PEKEE UNAYOPASWA KUTOA NI KULIPIA MAARIFA NA BAADA YA HAPO NI KULIPIA KWA BROKER (WAKALA) ILI UANZE KUTRADE MWENYEWE KWENYE MT4/MT5 YAKO.
4. TRADING SI KWAAJILI YA KILA MTU ( KAMA HUWEZI KUWEZEKEZA MUDA NA NGUVU ZAKO KUELEWA KIUNDANI HII BIASHARA NASHAURI NI VEMA UKAIOGOPA ZAIDI YA UKOMA)
 
- Baada yaa maombi ya watu wengi nitoe somo kuhusu forex, andiko hili litaelezea kwa undan forex ni nini, uhalisia ukoje na undan wake ambao huezi kuskia kokote

- Kwa kuanza ningependa kutoa disclaimer, huenda maudhui haya yakawa hayaaminiki na wengi ila as long ni uhalisia hayana budi kusomeka kma yalivo! kwa uzoefu wangu wa forex benki kuu basi maudhui haya ndo uhalisia kamili wa forex na unaweza kutumia maudhui haya kama reference kokote, pia nitaelezea uhalisia kwanini haiwezekan kutengeneza pesa kwa kutumia forex bila njia special






tukichukula mfano wa apo juu, dola 1 ni 2600 kukiwa na uhaba wa dola, basi mtu anaweza kuuza mpaka 3000 na akauza vizuri ukizingatia nchi yetu inapokea wageni wengi





ikitokea dola inatumika sana nchini kuna uhitaji umetokea mfano extra $1B inahitajika na mabenki ya kawaida wamekauka kufikia $1B basi banki kuu itanunua Tsh kutoka kwenye mabenki na kuwapa $2B, na itaendelea kununua tsh kwa mda kiasi mpaka uwiano upatikane, kwa mfano $2B ni zaidi ya mahitaji ya benki ndogo ivo wanaotaka tsh watakuta kuna upungufu wataomba tsh zaidi na tsh itapanda kwan rate mpya itawekwa, scenario hizi hutokea na kusababisha kitu kama hiki:


maaana yake kuna mtu kafanya uuzaji mkubwa mmoja, kitu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba! ikitokea Tsh inaenda mbio sana nkimaanisha ikitokea tsh inatishia nguvu dola basi benki kuu wanatakiwa kuirudisha Tsh chini, same same ikitokea dola inapanda sana benki kuu wanatakiwa kuirudisa chini.

unaweza kuuliza kwann ilihali inaonekana ni manufaa kwa tsh kua na nguvu zaidi ya dola: kwa mfano leo dola 1 ni tsh 2600, kesho tumeamka pap dola moja ni tsh 100, maaana yake nn!
Maana yake ni wote unaofanya biashara nao nje ya nchi mfano rwanda alikua ananunua maindi tanzania ya $100 anapata gunia 10, basi sasa anatakiwa kuja na $1000 kununua kiasi kile kile, ivo basi kuepuka haya benki kuu inatakiwa kushusha tsh kidogo ikae stable, dola ikipanda yenyewe kama yenyewe sio issue sana kwan inapanda against nchi zote kwahio bado ukija kubadilisha kwa tanzania utapata same same Tsh!


kwa sababu zile pesa anachukua broka anakaa nazo ukiwin basi anachukua pesa za walioloose anakupa wewe, same same ukiloose pesa yako anachukua anapewa aliepata, hakuna kitu kama kuingia sokoni kwa sababu hakuna trading yoyote inafanyika, when you press buy broka atakupa PERPETUAL CONTRACT kwa kiswahili MKEKA, likewise kwa gold, oil zote izi ni mikeka hakuna sehem broka atapeleka pesa yako kwa sababu forex sio soko na halipo pesa itabaki kwake

kwanini unaloose kwenye betting forex: reason kubwa kwanini unaloose kwenye forex ni kwa sababu unasoma charts,


pair zozote zilizopo kwa broka ni exchange halisi ya pesa kwenye nchi husika na sio thoughts of candles, kwa mfano unaweza kua na chart kama hii


kwa kua ulifundishwa matango pori wewe utaona kama ni mda wa kusell price itashuka bila kuelewa price hizi znaendna na sera za benki kuu moja kwa moja ukiwaza kusell benki kuu wanaona ni mda wa kupandisha zaidi pesa yetu ama kushusha, wapo wanaoskiliza news za benki kuu kabla ya kufanya trades but forex is complex kwa sababu kitakachodetermine price ni average summary ya transactions, yupo mtu anaweza kuja kubadilisha $100M anataka kuagiza magari nje ila hawa huezi kuwaskia kwenye news,

itoshe kusema ulimwengu uliwadanganya you can predict price movement kwa charts, sasa basi unaweza jiuliza tutumie njia gan kupata faida, mpaka sasa ni njia mbili tu za uhakika unaweza tengeneza pesa kwenye financial markets
1) LUCK
2) High frequency trading (HFT)

ili kuelewa HFT unatakiwa kuelewa financial markets znafanyaje kazi, ukitrade forex kwa broka maaana yake ukiweka buy basi yeye ameweka sell, unabet one to one na broka kama vile unavobet spot pesa ukiwin pesa inatoka kwenye kampuni
ila kitu usichokijua TRADING ni fani kabisa mtu anasomea anaenda ofisini asubui anarudi jioni, ili sasa kuelewa HFT unatakiwa kuelewa jinsi trading inafanya kazi


Kwa mfano yapo makampuni yanaojulikana kaama CITADEL faida yao ni around kila sekunde hua ni $70
 
Wewe jamaa unataka watu wote wakuone kuwa ndo kipimo Cha uelewa kuhusu forex trading humu ndani kuna watu Kama Mwl.RCT , Crimea na wengine wanaielewa forex na kuiishi kila siku.

Ww umejaa porojo mfu.
 
Wewe jamaa unataka watu wote wakuone kuwa ndo kipimo Cha uelewa kuhusu forex trading humu ndani kuna watu Kama Mwl.RCT , Crimea na wengine wanaielewa forex na kuiishi kila siku.

Ww umejaa porojo mfu.
sasa mm na wewe nani anaijua forex halisi, hujawahi ata kukaa pale BOT forex unaoijua wewe ni kamari
 
Yani simple logic.
Kama mtu anaweza trade akatengeneza faida hiyo kwanini ahangaike na wewe kukuuzia mara bot mara afanye akaunti management mgawane faida.
Yani hapo ndipo hao ma fx guru wa insta na x nawaonaga matapeli.
 
 
Jamaa yuko fasta ukikoment kidg tu negative kuhusu utapeli wake unakula kufuli
 
Hiyo pesa ungebetia odd 2 tu mara tatu saa hii ungekuwa na account iliyotuna. Hivi kabisa huyo erick aache kujitengenezea mamilioni ila kwasababu ana roho nzuri sana anakwambia wewe umpe pesa zako akutengenezee mamilioni kwa malipo?🤔

Mbona hii haimake sense. Ni sawa na uwe na mkeo then atokee mwanaume aseme yeye atamsomesha mtoto wako,atampatia matunzo mkeo,atampeleka na kumrudisha kazini kwa gari lake halafu anakwambia wewe kuwa anafanya hivyo kwasababu ya ujirani mwema,wewe haushituki kabisa unakenua meno tu hapo kama farasi mwenye furaha?🤔

Huyo ni tapeli,ungana na wenzako hata 5 au 10 muende kumfungulia mashitaka ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Na mtafute wakili mzuri atakae wawakilisha kwenye hii kesi. Atawalipa na fidia juu mpuuzi kabisa huyo erick.

Hizo pesa umempa ni nyingi sana kukubalia zitoweke tu.
 
Mwanangu unaonekana una uchawi fulani wa uchumi,hebu nigaie na mimi hats hirizi mbili nikawange niwe tajiri.
 
Mwanangu unaonekana una uchawi fulani wa uchumi,hebu nigaie na mimi hats hirizi mbili nikawange niwe tajiri.
Haha! Unajua brother haya ni mambo ya ku-take risk kweli kweli, ukimpa mtu hirizi halafu upepo ukamuendea kushoto ataona ulimpatia hirizi ya kumloga na sio kumsaidia
 
sasa vijana wa forex wanakuambia ukiwekeza TZS 3M utapata TZS 50M chap chap, na hapo ndipo wengi wanakuja kulia.
Kama.biashara imenyooka hivyo kama unavyoielezea mtu anakuja kulizwa namna? Hebu fafanua vizuri namna mtu anavyolizwa! Kama bei imeshuka ukaamua kui-hold hiyo Sarafu yako kuna ubaya gani?
 
Kama.biashara imenyooka hivyo kama unavyoielezea mtu anakuja kulizwa namna? Hebu fafanua vizuri namna mtu anavyolizwa! Kama bei imeshuka ukaamua kui-hold hiyo Sarafu yako kuna ubaya gani?
Naamini unazungumzia hizi crypto na sio forex, okay.

Kwenye crypto kuna faida lakini sio kwamba ndio faida tu pasipo hasara pia, hapana! Mtu anaweza kuumia kwa kununua sarafu mbaya, yaani sarafu yenye liquidity ndogo au isiyo na roadmap nzuri. Na ndio maana kwenye andiko langu nimesisitizia ku-deal na sarafu zenye liquidity kubwa na trading volume kubwa ili ukifia target yako ya faida uuze mara moja pasipo kusua sua.

Ku-hold sarafu sio mbaya, ila muhimu ni kuzingatia niliyokueleza ambayo ni liquidity au roadmap. Ngoja nikupe mfano mzuri; Tarehe 18/01/2025 $TRUMP coin ilikuwa ni $6.24 sasa watu wengi sana walinunua sababu ya ushawishi mkubwa wa Trump, ilipofika kesho yake tarehe 19/01/2025 $TRUMP moja ilifika $75.35 na trading volume yake ilikuwa ni $39B, kuna watu walikuwa mabilionea aise! Unaweza search habari ya hiyo coin ilivyowapa watu utajiri. Lakini kuanzia tarehe 22/01/2025 ilianza kushuka na kufikia $44.19 kwahiyo kama kawaida watu wengi wakaanza kununua wakiamini itapanda tena! Bro, iliendelea kushuka hadi kufikia bei ya leo ya $12.20 kwa $TRUMP moja kuishia kuwaliza watu wengi. Ukiangalia haka ka-story ni kwamba ushawishi wa Trump ndio uliofanya watu wakanunua hii memecoin ya $TRUMP lakini haina roadmap yoyote na ndio maana ilikuwa rahisi kushuka sana baada ya wahusika kuuza kiasi kikubwa cha sarafu hiyo na kununua Bitcoin (unaweza search kuhusu habari hii google utaona makala nyingi sana) kwahiyo lengo la kukuambia kuhusu hii coin ni kukuonyesha kuwa ku-hold sio vibaya lakini sikuzote hold sarafu yenye roadmap nzuri, liquidity, trading volume, na hata ikiwezekana iwe ni utility coin/token. Kwasababusarafu yenye sifa hizo sio rahisi kushuka sana, na hata ikishuka sana haitochukua muda kurudi kwenye nafasi yake na hata juu zaidi, ila kwa memecoin kama hiyo $TRUMP mara nyingi upanda kwa ushawishi wa mhusika tu, muda mchache badae inapoteza thamani.

Mimi crypto imenibadilishia maisha, lakini safari yake haikuwa rahisi hata kidogo kwasababu niliwahi kukutana na hasara ambazo sikuwahi kutegemea kwenye maisha yangu! Lakini ni kwasababu nilikuwa sina maarifa, unajua nilikuwa nanunua coin yoyote na muda wowote kwa ushawishi wa kijinga tu, lakini badae nilituliza kichwa na kuanza kujifunza, nilianza kudeal na crypto mwaka 2016, nilianza kupata faida kwenye crypto mwaka 2019 bro! All in all, crypto ni kama biashara za kawaida tu maana kuna faida na hasara pia, ila ukiamua kuwa serious na kujifunza unaweza punguza hasara na kuzidisha faida.
 
Watu wa Forex,Mwamposaa,demu aliyepata mbaba chuo na Forever living products kamwe hawashauiriki..
Nakumbuka mdada wa forever pale sinza miaka zaidi ya 10 imepita, aliniita nikaenda kwenye kambi yao ya networking nikamsikiliza, nikamsikiliza kwa makini. Baadae nikamwita kwangu. Nikamla biashara ikaishia hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…