Humjui Mbowe wewe!
Ni rahisi, Kama ulikuwa unawasikiliza vizuri wale waliotoka CHADEMA, ungeng’amua mapema ‘ugaidi’ wa viongozi wa CHADEMA. Angalia tu aina ya viongozi wa CHADEMA!
Watu wanapanga kulipua ofisi zao alafu wanasingizia serikali. Mbona usanii mwingi waliokuwa wanafanya ukichunguza ulikuwa unajulikana! Kujiteka, au wakiitwa polisi wanadanganya wametishiwa kutekwa, na wakikamatwa wanastage kwamba wametekwa. Kumbuka hata usanii wa kuchapa karatasi za kura siku ya uchaguzi!
Fuatilia hata kupotea kwa Ben Saanane kwa vyanzo vya watu wa CHADEMA, kwamba Saanane alimtishia Mbowe kuwa atatoa siri zake zote endapo atamuachisha kazi kama alivyopanga. Jiulize ni siri gani hizo? Alafu baadaye Mbowe anamvuta Saanane karibu na kumpandishia mshahara! Kisha anapewa safari ya kwenda SA kwa kazi maalum, ghafla anapotea! Alafu vijana waliopangwa mitandaoni wanaendeleza propaganda za kupotosha,
Au umesahau Mbowe alivyosingizia kapigwa na kuumizwa na watu wasiojulikana! Na jinsi viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA walivyokuwa wanaigiza kwa waandishi wa habari jinsi Mbowe alivyovamiwa! Kina Msigwa! alafu ukweli unakuja kujulikana in usanii tu!
Kesi hii itawafungua macho waliokuwa hawaijui CHADEMA, kwangu sishangai na najua mengi zaidi yanaweza kujulikana.