Wakinywa sumu mafisadi 10 hivi wakafilia mbali huko, Tanzania will be a safer place. Si wanahatarisha uchumi na usalama wa nchi hawa, au mi ndo sikusikia vizuri!!
Tanzania will not be a safer place kwa kuondoka mafisadi au kwa kufikishwa mafisadi na kukutwa na tuhuma kama ikibainika hivyo watafungwa.
Hakuna uhusiano wa safer place na mambo yaliopo ya ufisadi.
Hali hiyo itapatikana ikiwa tu wananchi wa Tz wataridhika na hali ya maisha waliyonayo ,kwa maana kuondoka kwa vitendo vya wizi wa kuuwana kwa kuiba simu ya mkononi,kuuwana kwa kutamania utajiri,kuuwana kwa kuiba kadi za simu na viselula viliomo,kuingia kweny nyumba kuuwa kwa ajili ya kuiba TV na redio,kuuwana kwa ajili ya kumkwapulia mtu vijisenti vilivyo mfukoni,watu wanaua kwa kuvamia kambi ya watalii porini na kuwakwapua laki tano na kuwaibia miwani na kofia.
Tanzania itakuwa na amani na utulivu kama hivi vifo vinavyosababishwa na watu wachache kwa gharama ndogo vitaondoka.
Nategemea vifo vya aina hii katika miji au nchi nyingi vimeanza kutoweka ,Tanzania kama tunavyosifiwa kuwa tunapiga hatua katika maendeleo basi serikali haina budi kutupa nusu ya nguvu zake katika kupambana na hali hii. Naweza kusema bado WaTanzania wengi wapo katika ujinga ,na ujinga ni adui wa maendeleo ,wanasiasa wetu,wabunge na viongozi hawana budi kuwahutubia wananchi maneno matamu na kuwagusia gusia mambo haya ili yafike kwa walengwa kwani tone la maji linaweza kupasua jiwe au kichwa(watu wa usalama wanelewa namna tone la maji linavyotesa).
Matokeo ya vifo vya kiholela vimekuwa ni vya kawaida kwa Watanzania na hasa hivi vinavyosababishwa na ujambazi wa vitu vidogovidogo kama simu na tv redio au vijisenti vya kutumia siku moja au nusu siku,mtu anapoteza roho ya mwenziwe kwa lakitano tu. Hivi Tanzania ya leo Laki tano utatumia siku ngapi ,itakuhitajia kuuwa watu wangapi ili ujitosheleze kwa maisha ya kila siku.
Tanzania ni nchi nzuri sana na inasifiwa kikweli kweli lakini wanasema hakuna Peace of Mind wananchi wake wanaishi kwa wasiwasi kwa ufupi hakuna usalama , au usalama wa raia zake ni sifuri au mdogo sana kiasi cha kuwafanya watu wawe kama wehu.
Hivyo unaposikia safer place basi ujue simu tv na redio sio vitu vinavyoweza kumfanya mtu kumkatisha maisha mtu mwengine.
tatizo ni kubanwa kwa njia za uchumi na masheria kibao ambayo kama yangeondolewa vitu hivi vingelijaa mpaka simba na chui nao huko mbugani wangekuwa wanamiliki redio,tv na vijiselula ,kusingekuwepo ukabaji wa kukwapua vitu hivyo,unakwapua unaenda kumuuzia nani ,na ikiwa vimejaa kila kona nani atanunua kwa mtu na haswa kitu cha wizi. bado tupo mbali sana kuwa safe country.