Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Huyo mwanamke anaonesha ni material oriented, maamuzi yake yana majuto mbele, muda ni mwalimu.

Fanton Mahal umeonesha ukomavu wa hali ya juu na huo ndio uanaume yaani ile delay ya kutotaka kukubaliana na ombi lake la talaka ni kama upuuzi lakini ina maana sana na mavuno yake atayapata x mke wako.
 
Daah Leo umeonyesha uwanaume kamili nimefurahi kuona upo stable Kias hicho

Ayo yamemstaajabisha kwakuwa mategemeo yake yameenda tofauti
Huwa wanatishia kuona upepo ,ukiwa stable wanashangaa sana!Kuna mmoja aliitisha kikao Cha ghafula mbele ya watoto na house girl eti "nakutakia maisha mema baba ..."!!?

Jamaa akasema "kuachana hakuwezi sababisha tetemeko watu wakafa ghafula,halafu sio ishu tumekutana ukubwani sio lazima tuzeeke pamoja,"Mama akanuna na kuhama chumba mwenyewe na jamaa akanyuti Hadi mama aliporudi mwenyewe!
 
Ila ningekuwa ni mimi ningepinga talaka kama Mwanamke wa shoka bila aibu πŸ˜… ila mali tungegawana
Ahahahah..pole. haiiko hivyo.
MSingi wa kesi ni talaka. Hayo mengine hayawezekan kama talaka imegomewa na yeyote kati yenu.
Na talaka ikitoka hayo mengine hayakwepeki
 
Mkuu kwa heshima na taadhima na kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba ikikupendeza siku yatakapomfika atakayokutana nayo na kuja kuomba msamaha mrudiani basi utupe mrejesho maana hivi ni viumbe vya ajabu havijui vinataka nini
 
Mkuu pole sana kwa changamoto uliyopitia na hongera sana kwa maamuzi uliyofikia.

Rafiki yangu mmoja alipia haya uliyopitia mpaka kupeana talaka Mahakamani, baada ya miaka mitatu nje ya ulingo wa ndoa hatimae walirudia, sijui ni nani alimdanganya.

Sasahivi jamaa anaisoma namba, ugonjwa wa moyo na Sukari juu, anapitia njia ngumu zaidi ya awali, somtimes wanawake ni scam.

Mkuu, x wife wako hayumo humu jukwaani asome huu uzi? Atapata mawili, matatu ajifunze upya, atajutia sana upuuzi wake.

Siku njema.
 
Safi sana. Huyo takataka saivi huko aliko ana mawazo. Halafu nataka nikupe mbinu nyingine ila hii ni yako tu kujifurahisha nikuambie tu hongera sana mana umekua huru na utainjoi sana maisha ya kua huru na kufanya utakayo, wewe wawaze watoto wako tu...siku isiyo na jina siku Moja tu kama weekend hivi, tafuta picha Moja hivi ya mrembo ama rafiki yako yoyote wa kike mrembo , weka picha yake status...utakuja kunipa majibu [emoji23]
 
Humu sidhani japo alikua anajua kuwa mimi napenda sana JF yeye akaanza kuwa mtu wa mitandao huku mwishon sasa sijui kama kajiunga humu au lah!!.
 
Ahahahah..nilisha delete picha contact zake na nikazi block na hata yeye alisha delete contact hata kabla yangu. Alizifuta. Mimi nimezifuata baadae sana baada ya kukubali ukweli kwamba our thing is irrepairable
 
Kumbato na liwazo kutoka kwa pisi Kali πŸ˜›πŸ˜› unakosaje D mbili πŸ’

Hakuna kingine zaidi ya maziwa.

Kwa watu tuliofundishwa kutozoea mambo hiyo inakuwa imeisha
Tunachukulia nimekufa au huyo mwanamke ndiye amekufa. Basi!
 
Ahahahah..nilisha delete picha contact zake na nikazi block na hata yeye alisha delete contact hata kabla yangu. Alizifuta. Mimi nimezifuata baadae sana baada ya kukubali ukweli kwamba our thing is irrepairable
Kaka utaoa tena?
 
Wangapi kwenye maisha yetu wamefanya hivyo? Hata kama kuna wasaidizi unataka kusema huyo mwanamke hafuatilii kuangalia kama kila kitu kinafanyika the way she likes? After all familia ngapi hapa Tanzania zenye wanawake wa nyumbani wameajiri wasaidizi?

Zipo nyingi Sana.
Na kama hazina unakuta ndugu wa mwanamke au mwanaume wamejaa nyumbani wanafanya hizo Kazi.

Wanawake wafanye Kazi za uzalishaji
Shughuli za nyumbani sio Kazi labda kama huelewi maana ya KAZI.
 
Marriage is a scam Wala sitojali kwamba umri utaenda sijui utaenda wap ila swala la ndoa uwiii limenitoka
Marriage is not a scam madam, mnakutana wawili msiokamilika na kuunda kitu kisicho kamili don't expect a perfect marriage wakati mnakutana wasio wakamilifu.

Ndoa ni nzuri, tena maisha bila ndoa ni magumu yenye sonona kubwa, hasa ukishafika umri fulani wa kuhitaji mtu wa karibu. Marriage is sweet my dear, usiidharau kwa visa vichache vya wadau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…