Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Watoto kweli hawezi kupoteza physically, ila emotionally. Ajitahidi pindi akutnapo nao awachie kitu cha kukumbukwa (sio lazima tangible things
Ewaaaah! touch your kids emotionally
Wala sio kwa kulipa ada.
wlaa sio kwa kupeleka mchele.
Awe na nyakati na watoto ambazo watabaki kumtafsiri yeye kama baba hata kama anakaa nao mbali!
 
Siku zote mtu kiburi huwa yupo anayeshindana nae, ni Mungu. Sio wewe mumewe wala mtu mwingine yeyote bali anashindana na Mungu.

Upe muda nafasi mkuu, kisha utaona vile ambavyo Mungu atakavyompa somo huyo mjinga asiyejitambua.
 
Pole kwa mapito
 
Daah! Umetumia hekima... ungeanza ubishi tu!! Angeona kakuweza angezidi kukusumbua hadi ungeona dunia chungu..

By the way,,,,, alikutafuta au kukutumia ujumbe baada ya kutoka mahakamani?
 
Pole kwa mapito
Shukran, it was mapito yenye mafunzo kuhusu maisha, binadamu, mapenzi, ndoa!
Leo niko na tafsiri pana sana kuhsu vyote hivyo.
Namshukuru Mungu sijabaki na bitterness, nimejifunza , ninaamini katika kukua, kubadilika, kupoteza mwelekeo wa maisha.
Wakati fulani ili usonge mbele ni lazima unaoongozana nao mbadilishane njia!
 
On top ya huu uzoefu kuna kitu kigumu sana kimejiumba kwako
.....kutokumwamini mtu mwingine kirahisi.....
Kitu nilichogundua cha muhim, ukikutana na kiumbe mpya jaribu sana kwa akili uchimbe taratibu ujue historia au maumivu alopitia kabla yako ili ikiwezekane imponye kwanza ndipo safari ianze.

Nimegundua ukikutana na mtu aliyeumizwa sana huwa kuna uwezekano mkubwa wa uhusiano kufa au kuyumba sana.
 
nzuri sana.
Huwa inadhaniwa watu hawawezi kuishi bila ndoa , sio kwlei aisee.
Ndoa yenye majeraha na machozi kila siku, better off kukaa mwenyewe ukisikia mgongoni kunawasha unajikuna ukutani!
aH
Na hivi mna kuta artificial sokoni ndio mnaringaaaa
 
Kuna mazingira ndoa za kikristo sio mpaka kifo mwanamke
 
Partly yes.
Although mi nimekataa hii kuikiri kwenye mahusiano yangu next after.
Ntajikosea sana haki kuendelea kujeruhika na maisha ya awali.
Watu hawafanani.
Hata mimi had part kwenye kuvunjika ndoa hiyo so kubaki hujisamehi kila siku unaacha na kuvunja tu mahusiano kisa ex alikujeruhi hii hapana.
So yes, imenipa uzoefu na kuwafahamu binadamu zaidi na kujua when to stop and when to persue and when to keep a person.
Mapenzi bado kitu muhimu sana in life.
Ndoa bado ni kitu chema sana

inavunjika leo, unaheal, unatizama your role, your lessons ah mbna unafall tena tu.
Ila sasa , watu wa aina yetu pia as you are saying hatuogopi pia kuvunja iwapo uhusiano umezingua.
Lakini hatutavunja tu alimradi kwa kuwa tunajua gharama ya kuvunja ndoa au uhusiano unaostahili kutunzwa.

Tu, ukiamua kuwa postive about it!
 
Na hivi mna kuta artificial sokoni ndio mnaringaaaa
Kwanini artificial?
HAPANA!
Mapenzi huisha bro, yakiisha unayaacha yaende.
Unapona unapenda upya and the cycle inaendelea.
Sasa unatarajia mtu akiachana na mwenzi akae tu kiseja, sio kweli!
Wanaopata wa kuwapend after tht, wapo na wanaishi maisha mazuri tu!
Hakuna tafsiri moja kuhusu maisha.
 
Nakubaliana na wewe. Maisha lazima yaendelee hakuna kujinyima
 
maisha yasonge mbele kwasasa, Focus your energy kwenye mambo yako,
usipoteze muda wako kutengeneza mashindano ya kuonesha maisha baada ya ndoa,
ishi maisha yako,
kwa kila nafasi unayopata ya watoto wako, itumie ipasavyo..
 
Mkuu Fanton Mahal kwanza pole na habari za kesi (kesi zinakula sana muda wa wadaawa) ila Mkuu nikuhakikishie jambo moja hapo hakuna mlichokifanya wala kukikwepa kwenye swala la muda. Nitakuambia kwasababu gani nasema hivyo.

Kwanza kabisa kesi zote za madai ya hamri ya talaka ni sharti la lazima zisikilizwe ushahidi hii ni ili Mahakama ijiridhishe kupitia ushahidi uliotolewa kuwa kweli hiyo ndoa imevunjika kiasi cha kushindikana kurekebishwa.

Nimesikitika sana juu ya mwenendo uliochukuliwa na Mh. Hakimu husika maana ni amefanya kituko cha aibu sana.

Tukiachana na hili la amri ya talaka embu tuangalie hapo kwenye chumo la pamoja yaani mgawanyo wa mali na mali zenyewe.

Kwanza kama imeenda hivi ulivyosimulia hapa ni dhahiri na wazi kuwa mkeo ameshindwa kuthibitisha kwanza uwepo wa hizo mali zilizotokana na ndoa, kwanini nasema hivyo ni kwasababu hizo mali ambazo bado mkapewa mgao wa 60%kwa 40% bado hata hazijatajwa hapo Mahakamani. Sasa mimi na wewe na wana JF wote tujiulize mmegawana mali gani na ipi hiyo ambayo imetajwa Mahakamani?

Tuache hili la mali na mgawanyo wake embu tuangalie hilo lingine la kuhusu watoto ambao nao mmesema wakae na mama yao, tujiulize swali tena ni watoto wapi hao?, ni nani na nani kwa majina yao?, je walitajwa hapo Mahakamani na kutambuliwa inavyopaswa kuwa?.

Hii ni aibu nyingine kwa mhimili wa Mahakama, na hapa haujatoa rushwa (sababu hujataja swala hilo) ila Mh. Hakimu kwa uzembe wa kukosa weledi amekinzana na taratibu zote na sheria zote zinazosimamia mashauri ya migogoro ya ndoa.

Nina uhakikakama utaitaja hiyo Mahakama basi hilo jalada litaitwa na Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya maana hii ni aibu na imeshakuwa mazoea sasa.

Hata kwa kuokoa muda wenu basi Mahakama ingepokea ushahidina utetezi siku hii hii moja kuliko kukanyagataratibu hivi zilivyokanyagwa. Ninaelewa kusudio lako la kuokoa muda na gharama lakini hii wiki na wewe umejifunza utaratibu usio sahihi wa namna kesi za talaka zinavyoenda.

Kesho au keshokutwa utamshauri mtu au kumpa uzoefu wako huu na akikutana na Mh. Hakimu anayejua nini kinatakiwa kufanyika ataanza kuhisi au kufikiri kuwa Hakimu husika anaweka mazingira magumu ili adai rushwa, mwisho wa yoteni kukosa imani na Mahakama na mfumo wake wote.

Hili linasikitisha sana.
 
Hayo mambo ya mwanamke pekee ndie akae kuilinda familia siku hizi hayapo.
Wote tulinde familia mwanamke na mwanaume.

Ndio maana talaka ni nyingi siku hizi sbabu wanawake wengi hawapo tayari kuteseka kwa kigezo cha kulinda familia.
Mbona huyu anaejadiliwa leo kaing'ang'ania familia yote kunani.
 
Nje ya maada,

Walio tunga hizo sheria za ndoa walikua wanawaza nini, Yani mgawanyo wa mali ni 50 50 lkn Kulea watoto hilo ni jukumu la baba kikawaida, Kawaida gani hyo? Imetafsiriwa kisheria au ni upeo wa hakimu?
mkuu nimewaza pia kama hakimu anashauri 50/50 kwenye mali pia ashauri 50/50 kuwajibika kulea watoto

kwenye kuchuma mgawane sawa kwenye majukumu apewe mwanaume huu ni uonezi

kwenye hii kesi mama angepewa 60% ya malezi pia kama alivyo pewa mali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…