Umeona sasa? Mnaenda kumfanya huyo binti aone mahusiano ya ndoa ya hovyo..!!
Mkeo itakuwa amekurupuka kudai talaka ila atajutia na itamtesa sana baadae..!!
Mkuu km kuna uwezekano wa kuahirisha maamuzi fanya hivyo kwa mustakabali wa watoto wenu..!! Mkishindwa sana gawaneni vyumba mlee mtoto.
Unajua kinachoenda kutokea? Wewe utaanzisha familia na mwanamke mwingine, na mkeo nae ataanzisha familia na mwanaume mwingine..!!
Hapo mtawaweka katikati watoto wenu, wakiwa kwa baba wanakuta mama mwingine na watoto wake, wakiwa kwa mama wanakuta baba mwingine na watoto wake..!!! Hao watoto watakuwa na huzuni miaka yote.. 😥
HOnestly sina mpango huo mkuu. Na hii ni kwaajili yao hapo badae. Maana najua mama yao yeye plan yake ni kuishi na mtu sasa mimi siwez tena hizo habar zitakua zinamalizwa juu kwa juu.
Yaani mke amet*mbwa pamoja na kupigwa picha za utupu,jamaa amehoji kistaarabu lakini mke amemjibu sh!t mke akaona haitoshi akamtia sell,kidogo akarudi akabeba home appliances akaona haitoshi akaenda kudai talaka tena mahakamani na mgao wa mali mume amekubali halafu inakuja kenge moja hapa inasema huku imebana pua ”huyo msamehe tu maisha yaende”.
Ndiyo nikamuuliza labda ana experience zaidi yetu yeye alipofumaniwa alisamehewa na mumewe?
Si mhusika.
Alitoa mawazo yake kwa namna hakumuoffend mtu..kuandika matusi, kuaddress watu hara hawajakukosea wewe personally si namna sahihi ya kutoa mawazo.
Ungeweza kupita comment yake, au kumuelewesha in a very positive manner kiasi angeona kosa lake(iwapo lipo bila kuandika matusi.
Anaweza kuamua kuahirisha. Kwani unafikiri hizo siku zote zimewekwa kwa ajili ya nini?
Ndani ya hizo siku 45 mnaweza kufanya reconciliation na kutangua torati.
Mke wa rafiki yangu aliomba talaka. Wakiwa katika process za mwisho mke huyohuyo akaamua kuahirisha baada ya kupata ushauri toka jamaa na marafikii. ...
Kwa case mezani jamaa akaze hakuna kurudi nyuma huyo malaya atakuja amtie maradhi amuue,mwanamke na watoto wanne (4) anayekubali kuvuliwa chupi hovyo akachomekwa uume na hawara huyo ni kichaa.
Wa hivi utakuta bodaboda wanaweka,Wagogo mabuchani wanaweka,Mangi dukani anaweka Wasambaa wauza mkaa wanaweka yaani ni ronya watu wanajiokotea tu jamaa ameshapata upenyo hii ni chance adhimu a-dump hiyo kenge....stupid kabisa tia sana hasira
Wakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu. Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana. Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya...
www.jamiiforums.com
"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.
Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.
Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"
Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto
Akauliza "unasemaje?"
Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"
Akauliza "umekubaliana na haya yote?"
Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"
Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.
Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.
Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.
Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.
1. Talaka.
Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.
2. Mgawanyo wa mali.
Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.
3. Matunzo ya watoto
Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.
4. Kuishi na watoto.
Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.
Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.
Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"
Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"
Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.
Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.
Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.
PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.
Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.
Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.
Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!
Ikaisha hivyo.
Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.
ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani
Kabisa ametunyima uhondo! Mimi nilikataa kama yeye mbele ya mchungaji,siku tunapiga stori ananiambia yeye alitaka ile siku tumeonana kwa mchungaji alitaka yaishie pale ila mimi kukataa kuongea pembeni ikabidi aendelee mbele mpaka hatua ya mahakamani then talaka...hayo ananiambia kipindi tumezaa tena baada ya Talaka , alipokuja kwangu kumleta mtoto baada ya kujifungua,alikaa wiki mbili akarudi kwake.
Mimi nlikutana na changamoto hyo miaka 10 na iliyopita...
Ila nlimaliza kibingwa na tko nkampa juu
Ukishaona umeingia kwenye vita ya mambo ya ndoa basi ujuwe hapo mtakuwa mnaviziana
Kesi za ndoa ni civil case ila wanawake/watu wengi hutafuta timing ya kukuingiza kwenye jinai (criminal case) yote kukutingisha
Hapo sasa inatakiwa akili nyingi + utulivu
Nmeshangaa tu ulivyos3ma wee ndy umemfumania na picha za uchi + sms zake alafu huyo huyo anakuja anakuburuza hadi kukuw3ka ndani na inaonesha aliku temper
Kabisa ametunyima uhondo! Mimi nilikataa kama yeye mbele ya mchungaji,siku tunapiga stori ananiambia yeye alitaka ile siku tumeonana kwa mchungaji alitaka yaishie pale ila mimi kukataa kuongea pembeni ikabidi aendelee mbele mpaka hatua ya mahakamani then talaka...hayo ananiambia kipindi tumezaa tena baada ya Talaka , alipokuja kwangu kumleta mtoto baada ya kujifungua,alikaa wiki mbili akarudi kwake.
Mimi nlikutana na changamoto hyo miaka 10 na iliyopita...
Ila nlimaliza kibingwa na tko nkampa juu
Ukishaona umeingia kwenye vita ya mambo ya ndoa basi ujuwe hapo mtakuwa mnaviziana
Kesi za ndoa ni civil case ila wanawake/watu wengi hutafuta timing ya kukuingiza kwenye jinai (criminal case) yote kukutingisha
Hapo sasa inatakiwa akili nyingi + utulivu
Nmeshangaa tu ulivyos3ma wee ndy umemfumania na picha za uchi + sms zake alafu huyo huyo anakuja anakuburuza hadi kukuw3ka ndani na inaonesha aliku temper
Tulizaa tena kabinti, na alipojifungua alikuja kukaleta...aliporudi kwake,usiku mtoto akilia sana ananipiga simu nikamsaidie kumbembeleza nae alale kidogo anachoka
Tulizaa tena kabinti, na alipojifungua alikuja kukaleta...aliporudi kwake,usiku mtoto akilia sana ananipiga simu nikamsaidie kumbembeleza nae alale kidogo anachoka
Umeonaaa 😄 wakati wa kesi ya ndoa inakuwa ni vita +chuki
Mimi aliniwinda sana anitengeneze criminal kumbeee ahh mipango yake aliyokuwa anafikiria kitambo nlikuwa najuwa
Nlikuwa mbele ya muda ,alafu mm syo mjingaaa
Nlimpiga KO moja tu hakuwa na hamu tena
Mpaka akaomba kumaliza nje ya mahakama...yaani itengenezwe deed of settlement
Kwa sababu nliona alikuja vibaya na mm nkaja vibaya aggressive mara 100000 yake
Walati ule kesi tena pale mahakama ya kinondoni nlikuwa nawamudu watu ahhh nlimnyoosha mapema sana
Yah sure it pains. Mwanangu wa kwanza, 14yrs, wa kike, siku ya kikao cha familia, alisikia ule mzozo na mabishano, baadae nikiwa naondoka akaniwahi akaniuliza kwa upole hukuna machozi yanamtoka "baba, kwani wewe unataka kumuacha mama?"
Nikamshika bega nikamwambia "usilie, kuna haviko sawa ndio tunavifanyia kazi, kila kitu kitakua sawa, usijali ,sawa?".
Akasema sawa.
Nilipoingia ndani ya gari , i cried
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.