Mkuu ahsante sana.
Niseme tu japo sijui sheria, ila kila ulichouliza hapo juu, kilizingatiwa.
Ujue, nikaja kuelewa kwann kesi ya ndoa eapecially kwenye madai ya talaka lazima ifunguliwe kupitia form no.3 ambayo hutolewa na baraza la usuluhishi la kata.
Kesi ya ndoa mpaka inafika mahakamani, ni lazima ipite hatua zifuatazo kutafuta suluhu
Mjumbe
Dawati la jinsia la polisi
Kwa viongozi wa dini
Vikao vya familia
Baraza la kata.
Hizi aote ni hatua za kunusuru kuvunjika ndoa.
Mpaka kesi inashindikana Baraza la kata, wao wanaandika muhtasari ambao ndio unatumika kama msingi wa madai.
Kwahiyo hakimu haanzii tu juu juu.
Kwahiyo
Mali zilitajwa
Watoto walitajwa kwa majina na idadi na umri wao
Kuhusi mashahidi mahakama inaeleza wazi kupitia wito wa keai kwamba lazima uje na mashahidi hivyo usipokuja nao unatoa maelezo.
LAkini kubwa zaidi mahakama ilitupa uhuru wa kama tunataka kwenda kwa ushahidi au tunakubalina ili mambo yasiwe mengi, mahakama inawasikiliza. Na hayo yooote yalizingatiwa mkuu.
Na kiukweli sikuona procedure ambazo hazikufuatwa.
Mkuu kama ulivyoeleza kuwa haufahamu masuala ya kisheria sikulaumu hata kidogo.
Taratibu za kesi za ndoa/talaka zinaanzia Baraza la usuluhishi.wa ndoa ambap kunaeza kuwa Baraza la kata au Bodi chini ya taasisi ya kidini, huko mnachukua Fomu namba 3 tu.
Sasa hii Fomu namba tatu,inaelezea jambo moja tu kuwa barazalimejaribu kusuluhisha lakini limeshindwa. Baada ya hapo ndio mnaenda sasa Mahakamani moja kwa moja sasa hii maana yake ni kuwa Mahakamani hamtakuwa na habari ya usuluhishi tena bali ni kesi moja kwa moja yaani ni kutoa ushahidi na kupokea utetezi.
Sasa tukirudi kwenu, utaona mmeenda mkaanza usuluhishi tena Mahakamani, na ukiangalia Mahakama imegeuka kama sehemu ya nyie Wadaawa adala ya kuwa kimya ipokee ushahidi na utetezi wa Mdai na Mdaiwa.
Hapo ndio shida imeanzia na kuivuruga kabisa kesi nzima. Na hili lote naelekeza lawama kwa Mh. Hakimu husika sababu amefanya asiyotakiwa kufanya na kafikia hitimisho bila kupokea ushahidi rasmi na utetezi rasmi.
Yaani kaendesha hiyo kesi kama mpo ofisi ya kijiji 😂. Bado tuna safari ndefu sana kwenye huu mhimili.
Si umeona hata wewe umeamini kuwa utaratibu wa kushuhulikia kesi ya mgogoro wa ndoa unaanzia sijui dawati la jinsia na hizo ngazi zingine ulizozitaja hapo juu. Hii sio kweli na huo sio utaratibu uliowekwa na sheria. (Bado sikulaumu sababu haukua unafahamu hili)
Utaratibu wa kufungua kesi ya mgogoro wa ndoa/talaka ni hatua mbili tu;
1. Baraza la Usuluhishi wa ndoa Kata au Bodi ya usuluhshi wa ndoa chini ya taasisi za kidini
2. Mahakama.
Hizo njia nyingine zote hazipo kisheria na hazitambuliwi na sheria zinazosimamia masuala ya ndoa.