Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Yah sure it pains. Mwanangu wa kwanza, 14yrs, wa kike, siku ya kikao cha familia, alisikia ule mzozo na mabishano, baadae nikiwa naondoka akaniwahi akaniuliza kwa upole hukuna machozi yanamtoka "baba, kwani wewe unataka kumuacha mama?"
Nikamshika bega nikamwambia "usilie, kuna haviko sawa ndio tunavifanyia kazi, kila kitu kitakua sawa, usijali ,sawa?".
Akasema sawa.
Nilipoingia ndani ya gari , i cried
Kiukwel inaumiza sana kweny maisha usiombe yakukute
 
Wakuu heshma kwenu.
Habari za jioni.

Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu 👇👇👇👇

"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.

Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
  • nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
  • leo hii mahakamani, hakimu alikua mwanamke.
Hakika wanawake wametaradadi everywhere, tukiendelea kwa mwendo huu, wanaume twafaaa
😁😁😁😁😁.

Anyway,.

Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.

Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"

Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto

Akauliza "unasemaje?"

Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"

Akauliza "umekubaliana na haya yote?"

Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"

Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.

Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.

Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.

Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.

1. Talaka.

Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.

2. Mgawanyo wa mali.

Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.

3. Matunzo ya watoto

Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.

4. Kuishi na watoto.

Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.

Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.

Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"

Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"

Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.

Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.

Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.

PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.

Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.

Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.

Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!

Ikaisha hivyo.

Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.

ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani

SHUKRANI WAKUU.
Usiku mwema
Huu ndo uanaume malizana nae na utainjoy sana, uko huru, kumbuka kwa Mimi kuwa na migogoro sipendelei Bora nimpe vitu vyote, hapo nakupa big up ndugu, kwanza watoto unao, pili hakuna majukumu zaid ya hiyo 150,000, ,na komea hapo usiongeze Kaa tulia enjoy, kama utafikiria kuoa baadae Rafiki usiende kwa wataftaji, chagua kuku wa kienyeji mrembo kazi yake kupika kupakua ajirembe kwa ajili Yako tu, ambaye si mjuaji asiye na makuu, mkuu umaskini hauishi utaendelea kuwepo zaid na zaaid, usimtoe mke wako nje kufanya kazi kazi fanya wewe hudumia familia, ona mgao umepita na bado jukumu la kulea ni lako, yeye pesa zake ni za nini? Ndo maana waerevu tunasema Mwanamke Kaa nyumbani hutaki huo ndo mwisho wetu, ndugu chagua kuku wa kienyeji utafaidika.
 
Yah sure it pains. Mwanangu wa kwanza, 14yrs, wa kike, siku ya kikao cha familia, alisikia ule mzozo na mabishano, baadae nikiwa naondoka akaniwahi akaniuliza kwa upole hukuna machozi yanamtoka "baba, kwani wewe unataka kumuacha mama?"
Nikamshika bega nikamwambia "usilie, kuna haviko sawa ndio tunavifanyia kazi, kila kitu kitakua sawa, usijali ,sawa?".
Akasema sawa.
Nilipoingia ndani ya gari , i cried
Umeona sasa? Mnaenda kumfanya huyo binti aone mahusiano ya ndoa ya hovyo..!!

Mkeo itakuwa amekurupuka kudai talaka ila atajutia na itamtesa sana baadae..!!

Mkuu km kuna uwezekano wa kuahirisha maamuzi fanya hivyo kwa mustakabali wa watoto wenu..!! Mkishindwa sana gawaneni vyumba mlee mtoto.

Unajua kinachoenda kutokea? Wewe utaanzisha familia na mwanamke mwingine, na mkeo nae ataanzisha familia na mwanaume mwingine..!!
Hapo mtawaweka katikati watoto wenu, wakiwa kwa baba wanakuta mama mwingine na watoto wake, wakiwa kwa mama wanakuta baba mwingine na watoto wake..!!! Hao watoto watakuwa na huzuni miaka yote.. 😥
 
Hakuna mke unayeweza kumuita Golikipa. Anapobaki nyumbani anashinda amelala tu na kuangalia TV? Mwanamke anaamka asubuhi anaandaa watoto kwenda shule, anakuandalia kila kitu uende kwenye mihangaiko yako; anasafisha nyumba, anapika, anafua, anahakikisha kila kitu ndani ya nyumba kinakaa sawa. Unarudi nyumbani kutoka ulikokuwa anakupokea na kukuandalia chakula, una-relax na kuwa na akili ya kuendelea kutafuta mkate wa kesho na kwa watoto anafanya hivyo. Leo wewe ni wa kumuita Golikipa!!!! Hivyo vyote anavyofanya unaona SIYO kazi???? Wanaume mna matatizo sana ya uelewa na ni wabinafsi sana.
Huyo ni mtoto mdogo sana anajulikana humu kwa maandishi yake asikuumize akili,umetumia nguvu nyingi sana kutaka kumpa ufahamu mtu ambae hajakua.
 
Mmmmhhh KUANZA UPYA SI UJINGA,,, ila kuna vit VITACHELEWA SANAAA,,, akiomba msamaha fanya jambo maisha haya jawah kueleweka na hayata eleweka TUNAISHI SEHEMU NDOGO SANAAA YENYE furaha kiduchu,,,,, upendo utamalaki juu yako
Simple hivyo eti???

Wewe mumeo alivyojua umevuliwa nguo na hawara ulimuomba msamaha maisha yakaendelea?kama cha kuandika hamna kwanini usikae tu kimya kuliko kumshauri mtu ujinga?
 
Hatuchangii sana kwasababu wanaume huwa ni chanzo cha wanawake kuteseka kwenye ndoa.

Mnachepuka sana halafu mnaomba misamaha tunawasamehe lakini vinyongo tunaweka moyoni tunaogopa kukimbia ndoa kwa sababu kadhaa.

Siku hizo sababu kadhaa tukizipatia ufumbuzi tunakimbia ndoani, mnabaki kutusema hamjaona kosa lenu huku mnasahau makosa ya zamani ambayo sisi huwa tunarundika moyoni.

Naamini Fanton Mahal kuna sehemu alizembea na wajanja wakatumia huo mwanya kuruka na mkewe.
Kuna hii comment, af kuna mmoja pia nasubiri ajibu... asipojibu nitamtafuta nimtag😅
Huwa natamani hawa kufahamu umri wao, na kama ni wakubwa natamani kufahamu kama wana watoto wa kike... kama una D2 utanielewa😂😂
 
We kweli the worst.

Kwanini umuattack hivyo.

Huwezi kupresent hoja yako bila kumdhihaki mtu?
Ulikiona lakini alichomshauri mwenzako?

Yaani mke amet*mbwa pamoja na kupigwa picha za utupu,jamaa amehoji kistaarabu lakini mke amemjibu sh!t mke akaona haitoshi akamtia sell,kidogo akarudi akabeba home appliances akaona haitoshi akaenda kudai talaka tena mahakamani na mgao wa mali mume amekubali halafu inakuja kenge moja hapa inasema huku imebana pua ”huyo msamehe tu maisha yaende”.

Ndiyo nikamuuliza labda ana experience zaidi yetu yeye alipofumaniwa alisamehewa na mumewe?
 
Wakuu heshma kwenu.
Habari za jioni.

Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu 👇👇👇👇

"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.

Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
  • nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
  • leo hii mahakamani, hakimu alikua mwanamke.
Hakika wanawake wametaradadi everywhere, tukiendelea kwa mwendo huu, wanaume twafaaa
😁😁😁😁😁.

Anyway,.

Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.

Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"

Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto

Akauliza "unasemaje?"

Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"

Akauliza "umekubaliana na haya yote?"

Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"

Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.

Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.

Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.

Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.

1. Talaka.

Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.

2. Mgawanyo wa mali.

Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.

3. Matunzo ya watoto

Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.

4. Kuishi na watoto.

Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.

Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.

Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"

Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"

Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.

Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.

Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.

PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.

Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.

Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.

Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!

Ikaisha hivyo.

Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.

ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani

SHUKRANI WAKUU.
Usiku mwema
Pole sana ila Kuna sehem umetunyima uhondo ,pale ulipokataa kuongea naye pembeni,
 
Back
Top Bottom