Naomba nikuambie tu ukweli, usije dhani tuna nia ovu kusema jamii x ina tamaduni flani flani ambazo ni mbaya ukadhani jamii zingine hazina mambo ya hovyo.
1. Kwa mikoa ya kusini, watoto wanasoma shule vizuri tu kama wengine wa mikoa mingine ingawa wanaofaulu kuendelea mbele ni kundi dogo, hili halina ubishi.
2. Mtoto akishatoka jandoni/unyagoni huwa yuko huru kiasi flani na ana maamzi ndani ya familia, kama ni binti baba hauna maamzi makubwa juu yake ingawa mama/wajomba wanaweza amua jambo lolote juu ya binti husika.
3. Suala la ngono ni kitu cha msingi kwa mabinti wengi tena wazazi wanabariki hilo na kama mhusika utakuwa unawapa ofa ndogo ndogo utakuwa unaitwa "baba" kabisa kutoka kwa wazazi wa yule binti.
Utasikia baba kesho uwahi kutusaidia kupuliza mikorosho, hapo huwa inafikia hatua baadhi wanakukabidhi chumba unaishi na binti yao kwao na huku huyo binti akiwa anaendelea na masomo.
N:B Hali hii haiwahusu mabinti wote ni baadhi miongoni mwao.
4. Ushirikina, uchawi na mambo yote ya kimila ni jambo jumuishi kwa familia KARIBU zote bila kujalisha ni familia za swala tano au wafuasi wa Gwajima.
Angalizo, kuna wateule wachache mno wameamua kujitenga na mila.
5. Ndoa, ni kitu kisichothaminiwa kwa kupewa heshima yake sitahiki.
a) Mfano, ukimshika ugoni mwanandoa, huwa unalipishwa fedha kiasi flani na maisha yakaendelea
b) Wanawake wengi hawadumu kwenye ndoa, ukichukua kundi la wanawake 20 wenye umri wa miaka 30, wanawake zaidi ya 13 wameshaachika na kuolewa pengine zaidi ya mara moja.
c) Asilimia kubwa ya wanaume, wana watoto wa nje ya ndoa
Hayo machache niliyoyaongea ni kweli tupu hususani maeneo yote ya vijijini kwa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Leejay49 naomba uje na data za kukanusha hayo machache niliyoyaandika hapo juu.