Hatimaye bondia kutoka Ufilipino avalishwa gloves zenye rangi ya bendera ya Tanzania ya jiwe Tanzania ya viwanda

Hatimaye bondia kutoka Ufilipino avalishwa gloves zenye rangi ya bendera ya Tanzania ya jiwe Tanzania ya viwanda

Mm nahisi twaha kiduku ndo alipaswa apambane pambano la mwakinyo
Na mwakinyo apambane pambano la twaha kiduku.
Ni ukweli usiyopingika mwakinyo hajamfikia hata mfaume au twaha kiduku
 
Majaji waliyokuwepo ni kutoka wapi

Ova
 
V A R Tumieni tuu hapo kama refa wa Liverpool na Man City. Hureee Mwakinyooo!
 
Mpaka wafatiliaji wa michezo wanakili tumepigwa japo tumeshinda[emoji3][emoji3]
20191130_013028.jpeg
 
V A R Tumieni tuu hapo kama refa wa Liverpool na Man city ,hureee Mwakinyooo
 
Wamezingatia uzalendo tu lakini mwakinyo kapigwa,ngoja apewe pambano na bondia wa USA utacheck atapigwa kama alivyopigwa dula mbabe KO round ya 2 siku aliyorudi hakuna mtu amejua.
 
Sijawahi kuwaelewa Wabongo 99.5% ni majitu ya hovyo, majuaji na yasiyopenda vya kwao ni malimbukeni sana.

Big up Mwakinyo umefanya vema sana.
 
Binafsi nimeshuhudia pambano tangu mwanzo mpaka mwisho. Mwakinyo amezidiwa pointi na Mfilipino. Mwakinyo kupewa ushindi siyo kweli Mfilipino alimzidi karibu kila raundi. Tuwe na haki pambano hili Mwakinyo ameshindwa kwa pointi ingawaje amejitahidi sana.

Pongezi nyingi sana kwake bondia wetu Hassan Mwakinyo na za dhati kabisa kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu mpendwa Jemedari Mh. Dk. John Pombe Joseph Magufuli maana ni mojawapo ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika sanaa, michezo na burudani kama kipaumbele na chachu ya maendeleo.

Yaaah! Tunatekeleza. Sisi ni Tanzania Mpya+

Kanyaga twende baba, tumechelewa sanaa, huu ni ushindi wa kitaifa.
 
Ameshinda kiana aina.......muda wote anakimbia kimbia tu

Boxing ni art; nguvu na maarifa vinahitajika ili kushinda.

Kwenye pambano November 9, 1996 kati ya Mike Tyson na Evander Holyfield, Holyfield alitumia muda mwingi wa rounds zile za kwanza kumkumbatiakumbatia Tyson ili kumzuia asifanye ile aina ya mashambulizi yake ya nguvu na kasi kubwa iliyokuwa ikiwatoa knock out wapinzani wake ndani ya rounds 1 - 2 tu.

Mbinu hiyo ya Holyfield ilisaidia kumchosha Tyson, ambaye hakuwa na mazoea na stamina ya kupigana rounds nyingi.

Holyfield alianza kumpa kibano Tyson baada ya kuwa ameshamchosha kwa mbinu ambayo baadhi yetu hatukuipenda!
 
Tatizo wabongo wengi wanashindwa tofautisha kati ya professional boxing na ngumi za mitaani.

Nina clip hapa sina tu utaalam wa kuattach, yule Mfilipino wenu kapiga ngumi km 30 hv zote za tumbo Mwakinyo ka-guard tu, mlitaka afanyaje?

Halafu anatoka mtu anasema jamaa kashinda kwa points, zipi? Ngumi za tumbo na zinazoishia kwenye guard? Km vitu hamjui ulizeni Mayweather alirushiwa ngumi nyingi sana na Pac mwisho wa siku akashinda ikaibua maneno km hivi boxing ni ku-score sio kupiga piga tu!
 
Back
Top Bottom