Hatimaye bondia kutoka Ufilipino avalishwa gloves zenye rangi ya bendera ya Tanzania ya jiwe Tanzania ya viwanda

Hatimaye bondia kutoka Ufilipino avalishwa gloves zenye rangi ya bendera ya Tanzania ya jiwe Tanzania ya viwanda

Mwakinyo kashinda kwa point kosa la mpinzani wake nikwamba alikua anapiga ngumi za tumbo lkn mwakinyo alikua anapiga za usoni ambazo zilimpatia point nyingi
Kibongo bongo hata umpige mtu kisogoni wao wanahesabu tu bondia akiwa anakimbia kimbia kuegemea kamba inaonekana kapigwa.

Sijui huwa hawamuoni Mayweather, anapigwa ngumi kibao mwisho wa siku anashinda kwa points. Boxing ni scoring, sio kupiga piga tu kama ngumi za mitaani!
 
Hakudondoshwa kwa punch.
Alikwepa. akakosa balance, akasukumwa kidongo akateleza na kuanguka ndio maana hakuhesabiwa hadi 10 na refa.
Hii ni chuki kwa mbongo mwenzenu au hamjui boxing?
Si lazma sote tufatilie boxing hawa wengine wangeendelea tu na football!
 
Huu mchezo umechezwa hadharani siyo chumbani,kila mtu ameona, Mwakinyo mwenyewe hana furaha na ushindi wake utakuwa wewe?
Mzee ngumi sio futibolu, unaeza ukarusha ngumi nyiiiingi halafu mi nikarusha ngumi tano tu na nikashinda, so kama hujui sheria za ndondi bora utulize kipago tu.
 
Kiukweli kwa aliyeshuhudia mpambano huu ameona jinsi mpambano ulivyokwenda. Labda wajuzi mtusaidie sababu iliyopelekea Hassan Mwakinyo kuibuka mshindi.
Ngumi mfululizo za Tinampay zilikua zikiishia kwenye Gloves na Tumboni Wakat Ngumi moja moja za kudokoa za Mwakinyo zilikua zikiishia kwenye uso.
 
Binafsi, nimeshuhudia pambano tangu mwanzo mpaka mwisho. Mwakinyo amezidiwa pointi na Mfilipino.

Mwakinyo kupewa ushindi sio kweli Mfilipino alimzidi karibu kila raundi. Tuwe na haki pambano hili Mwakinyo ameshindwa kwa pointi ingawaje amejitahidi sana.
Ukicheza Uwanja wa Ugenini na Majaji wawe wa kutoka huko Ugenini Basi formula ni moja tu, piga mtu kwa knockout.

Ukitegemea ushindi wa Point figisu zitakua nyingi. Sababu kiuhalisia kuhesabu ngumi zinazotua sio rahisi, Ndio maana mechi hiyo hiyo moja Majaji tofauti wanakuja na matokeo tofauti
 
Mi napendekeza wakat mwingine majaji watoke watatu kama ifuatavyo

1 katka nchi atokayo mgeni.
2katika nchi ya mwenyeji.
3 katika nchi jirani like Kenya ama Ug.
 
Yeah Mfaume Mfaume vs Kiasi Ally pia ni wanaume
Mwakinyo uwezo wake ni wa kawaida sana kuliko tunavyoaminishwa....hayuko vizuri kwenye kushambulia (mikono ni mizito sana) hata kujilinda pia(anapaki basi sana)...ameruhusu ngumi nyingi za tumboni ambazo zinakata pumzi...kwa kifupi amejitahidi lakini amebebwa....Dogo Mfaume...yule aliepigana pambano la mwisho la utangulizi ni bondia mzuri sana....anajua kushambulia na kujilinda pia anajiamini sana...Mwakinyo aachane na mapromo makubwa wakati uwezo wa kawaida...afanye mazoezi kwanza.
 
Mwakinyo ilitakiwa amalize kwa KO, ameshindwa kumdondosha mfilipino hata mara moja, ametudissapoint sana
 
Ilipo CCM kushinda kwa Point Ni Ngumu! Kuna Judge katoa hadi 98 kwa 92 [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] hili pambano kuficha Aibu wangetoa hata Draw! Msitudanganye na Ngumi za Usoni Sijui Wapii Hassani Kapigwa nyingi tuu mikona yake haina nguvuu ngumi zinapita tuu kachoka mda wote anakimbilia kwenye Kamba! Yaani Mwakinyo ni kama alikuwa na miaka 35 halafu mphilipino miaka 24! Kwenye Corner ya Mwakinyo watu wengi hajui hata amsikilize nani? halafu siku tunataka tuandae Mashindano makubwa Never Wazungu sio Wajinga

Round Zotee Mwakinyo Kalemewaaa, Waphilipino Kwenye Ngumi ndio watu professional sema Tanzania Wizii ndio Kawaida Yetuuuuu!!! kila sehemuu Zinaibiwa kura inaibiwa mitihani zinaibiwa sadaka bank hela zinapotea tuu yaani bongo ni kila Sehemu
 
Ha ha ha ha Muacheni huyo mphilipino akaeleze kuwa tuna demokrasia [emoji1787][emoji1787][emoji1787] maana huwa hawatuelewi vizuri.... Anae jua ki philipino anisaidie kueleza "Bao la mkono"

Limepita kabisaa la mkono.

Niajabu na kweli 😃😃
 
Back
Top Bottom