mgunga pori
JF-Expert Member
- Jul 23, 2016
- 4,092
- 4,896
Home advantage huwa inaongeza point kwa bondia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kibongo bongo hata umpige mtu kisogoni wao wanahesabu tu bondia akiwa anakimbia kimbia kuegemea kamba inaonekana kapigwa.Mwakinyo kashinda kwa point kosa la mpinzani wake nikwamba alikua anapiga ngumi za tumbo lkn mwakinyo alikua anapiga za usoni ambazo zilimpatia point nyingi
Hapa ndio wabongo wengi hawatakuelewa wao kila ngumi wanahesabu tu!Mfilipino Kapigwa Ngumi Nyingi Usoni Na Ndo Zenye Pointi Arifu.
Hakuna bondia anaitwa Dula kiduku Tanzania!Bora game ya Dulla Kiduku vs Msouth
Si lazma sote tufatilie boxing hawa wengine wangeendelea tu na football!Hakudondoshwa kwa punch.
Alikwepa. akakosa balance, akasukumwa kidongo akateleza na kuanguka ndio maana hakuhesabiwa hadi 10 na refa.
Hii ni chuki kwa mbongo mwenzenu au hamjui boxing?
Sasa wewe kwenye boxing reference yako Kitenge? anakijua nini huyu? Mdomo tu mwingi hakuna lolote kaangalieni tena Mayweather vs Pac hamtakuja tena kupiga kelele hapa!Mpaka wafatiliaji wa michezo wanakili tumepigwa japo tumeshinda[emoji3][emoji3]View attachment 1276728
Mzee ngumi sio futibolu, unaeza ukarusha ngumi nyiiiingi halafu mi nikarusha ngumi tano tu na nikashinda, so kama hujui sheria za ndondi bora utulize kipago tu.Huu mchezo umechezwa hadharani siyo chumbani,kila mtu ameona, Mwakinyo mwenyewe hana furaha na ushindi wake utakuwa wewe?
Bongo bado sana tunatia aibu kabisa yani refa anakata kamba za glov kwa meno huu ni upuuz mkubwa sana
Huu mchezo umechezwa hadharani siyo chumbani,kila mtu ameona,Mwakinyo mwenyewe hana furaha na ushindi wake utakuwa wewe?
Hujajibu swali kwa ufasaha.Ukikua utaelewa.
Karibu duniani
Ngumi mfululizo za Tinampay zilikua zikiishia kwenye Gloves na Tumboni Wakat Ngumi moja moja za kudokoa za Mwakinyo zilikua zikiishia kwenye uso.Kiukweli kwa aliyeshuhudia mpambano huu ameona jinsi mpambano ulivyokwenda. Labda wajuzi mtusaidie sababu iliyopelekea Hassan Mwakinyo kuibuka mshindi.
Ukicheza Uwanja wa Ugenini na Majaji wawe wa kutoka huko Ugenini Basi formula ni moja tu, piga mtu kwa knockout.Binafsi, nimeshuhudia pambano tangu mwanzo mpaka mwisho. Mwakinyo amezidiwa pointi na Mfilipino.
Mwakinyo kupewa ushindi sio kweli Mfilipino alimzidi karibu kila raundi. Tuwe na haki pambano hili Mwakinyo ameshindwa kwa pointi ingawaje amejitahidi sana.
Kwa hiyo angefurahi angeambiwa kashindwa?Unaona hata ushangiliaji ni wa kusuasua sana, hata Mwakinyo mwenyewe hanafuraha na ushindi wake.
Mwakinyo uwezo wake ni wa kawaida sana kuliko tunavyoaminishwa....hayuko vizuri kwenye kushambulia (mikono ni mizito sana) hata kujilinda pia(anapaki basi sana)...ameruhusu ngumi nyingi za tumboni ambazo zinakata pumzi...kwa kifupi amejitahidi lakini amebebwa....Dogo Mfaume...yule aliepigana pambano la mwisho la utangulizi ni bondia mzuri sana....anajua kushambulia na kujilinda pia anajiamini sana...Mwakinyo aachane na mapromo makubwa wakati uwezo wa kawaida...afanye mazoezi kwanza.Yeah Mfaume Mfaume vs Kiasi Ally pia ni wanaume
Mfilipino kakosea kujaza fomu.Kiukweli kwa aliyeshuhudia mpambano huu ameona jinsi mpambano ulivyokwenda. Labda wajuzi mtusaidie sababu iliyopelekea Hassan Mwakinyo kuibuka mshindi.
Ha ha ha ha Muacheni huyo mphilipino akaeleze kuwa tuna demokrasia [emoji1787][emoji1787][emoji1787] maana huwa hawatuelewi vizuri.... Anae jua ki philipino anisaidie kueleza "Bao la mkono"