Hatimaye David Kafulila akabidhi ofisi, aendelea kusisitiza Rais Samia hakamatiki utekelezaji wa Ilani, amtaja kuvunja rekodi ya miaka 20 kwenye maji

Hatimaye David Kafulila akabidhi ofisi, aendelea kusisitiza Rais Samia hakamatiki utekelezaji wa Ilani, amtaja kuvunja rekodi ya miaka 20 kwenye maji

Nenda kafanye research uje utuambie kati ya wanachama wa CHADEMA na Wale wa CCM, Ni wepi wananjaa kali
Mtu awapo ccm hasa akishaonja teuzi anakua na alosto ya njaa endelevu, yani unakabidhi ofisi maneno ya mapambio Kama yote ya kusifu Ili iweje? Je wenzake hufanya hivi ,Kama fulsa ipo ipo tu sio lazima tumia nguvu nyingi , ,some time yanakua hayatoki moyoni
 
Katiba mpya ya nini?

Kwanini msianze na hiyo yenu inayomwacha Mbowe kuwa mkt miaka 30,

CHADEMA UZENI TU HICHO CHAMA MGAWANE MTAKACHOPATA
Hofu yako KUU ni kutopata uteuzi holela tena. Katiba mpya yaja kujenga uwajibikaji na sio u-chawa
 
Mtu awapo ccm hasa akishaonja teuzi anakua na alosto ya njaa endelevu, yani unakabidhi ofisi maneno ya mapambio Kama yote ya kusifu Ili iweje? Je wenzake hufanya hivi ,Kama fulsa ipo ipo tu sio lazima tumia nguvu nyingi , ,some time yanakua hayatoki moyoni
Labda ungesema tu maneno aliyoyasema KAFULILA ni kweli au sio kweli,

SIKILIZA JAMAA,

Sasa kama upatikanaji wa Maji Simiyu umepanda kutoka 56% hadi 73% na huu ni mwaka mmoja tu, JE UNATAKA MTU ASISEME KISA KATUMBULIWA?

Sasa kama Rais samia amepeleka 400BL UNATAKA MTU ASISEME KISA KATUMBULIWA?

Sasa kama Mama kaongeza bei ya Pamba mpka tsh 1,800 toka tsh 800 mwaka wa juzi UNATAKA MTU ASISEME KISA KATUMBULIWA?

KAFULILA GO,

HUYU MAMA ANAFANYA MAMBO MAKUBWA SANA ILA TU MENGI HAYASEMWI


UPINZANI TUPA KULE 2025
 
Hofu yako KUU ni kutopata uteuzi holela tena. Katiba mpya yaja kujenga uwajibikaji na sio u-chawa
Sawa anzeni na hiyo ya CHADEMA tuone mfano,

Ivi kwenye nchi hii kuna mtu anaweza kumzidi Mbowe kwa Machawa?
 
Anamsifia Samia wakati yeye alipanga kuua uchumi wa Simiyu kwa kupiga marufuku michomoko mjinga sana Kafulila

Mama Samia hahitaji kusifiwa na mtu.aliyemteua na kumuapisha anachotaka ni utendaji wa huyo mteuliwa full stop

Kama kuna mteuliwa anadhani kuwa mama anachotaka ni kusifiwa anapiteza muda

Mama Samia anachotaka akikukabidhi cheo na kukuapisha aone kazi sio pambio na nyimbo za nani kama Mama

Mama Samia hateui wanamziki au waimba kwaya au waimba pambio au nyimbo za kumsifu!!!

Wateuliwa hii awamau sio ya walitunga nyimbo za kwaya au za mziki au pambio au kaswida za kumsifu Raisi

Angalia tu umepewa kazi ipi ufanye.Akija eneo lako ziara hahitaji pambio na nyimbo za kusifia jiandae kuonyesha umetekelezaje wewe ilani na maelekezo na utekelezaji wa pesa za maendeleo zilizokuja eneo lako

Haji kutembelea eneo lako kuja kusikiliza kwaya,au muziki au pambio au kaswida za kumsifia

Kila kiongozi ajitathimini yeye kafanya nini sio Mama Samia kafanya nini
 
Kama kuna RC alimwelewa na kumwelezea Vizuri Rais Samia kwa Umma basi ni Kafulila

Hamu yangu RCs waige mazuri ya Kafulila hasa kusema mazuri ya Rais wetu na Serikali anayoiongoza.

Hebu angalia hii ni kazi ya Rais Samia kwa mkoa mmoja tu Simiyu ,

Yule anayebisha Rais Samia kiboko yao anashida kubwa ya akili
Whaat! Kujua kujipendekeza ndiyo kumwelewa? Kweli akili ni nywele.... BTW siku hizi watu wakitumbulia hawatoi tena maneno machafu au kuhama bali wanazidisha kusifu na kutukuza ili wakumbukwe tena. Mwasisi wa kucheza na akili za wateule wake ni Magufuli. Alikuwa anatumia ujanja wa kutumbua na kurudisha, iwapo aliyetumbuliwa aliendelea kumsifu na kumtukuza. Namna rais anakuwa ni kama ameshikia watu akili zao na anazichezea anavyopenda.
 
Tatizo lenu nyie Ufipa FC hampendi kumsikiliza Rais,

Rais alishasema yeye mwenyewe kuwa hawa wengine anawapeleka maeneo mengine
Sawa chama dola. Maeneo mengine ni kama vile aliyekuwa RC Kilimanjaro kwenda kuwa mwenyekiti wa bodi ya TBC. Je, hapo kapanda au kashushwa?
 
"RAIS SAMIA AMEVUNJA REKODI YA MIAKA 20 SEKTA YA MAJI, AMEOKOA TRILIONI 3 AMBAZO ZINGETUMIKA KUTIBU MAGONJWA YATOKANAYO NA UKOSEFU WA MAJI."

View attachment 2318672
Mhe David Kafulila akimkabidhi Katiba Mkuu wa Mkoa mpya Mhe Dkt Yahya Mawanda kama nyenzo yake ya kufanyia maamuzi


Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe David Kafulila amesema Rais Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi ya utekelezaji wa bajeti ya maji ya miaka ishirini ( 20 ) mfululizo iliyopita,

Mhe David Kafulila ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi majuzi huku akiwaahidi kuwatumia maeneo mengine anasema, " Wakati nakuja Simiyu kama mkuu wa mkoa baada ya kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan nilikuta kero kubwa kuliko zote kwa Mkoa wa Simiyu ni " Maji "


View attachment 2318673
Mhe David Kafulila akiwa katika picha ya pamoja na mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe Dkt Yahya Mawanda wakati wa makabidhiano ya ofisi


Mhe David Kafulila anaendelea kusema, Leo Mwaka mmoja huu niliokaa hapa tumeshirikiana kusimamia vizuri Sana mabilioni ya fedha za miradi ya maji zilizoletwa Mkoa wa Simiyu na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan ninyi nyote mtakuwa mashahidi wangu,

Kafulila anaendelea kusema,Leo naondoka Mkoa Simiyu wote tunaona tatizo la maji limepungua sana hapa lazima tumshukuru Sana na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,


View attachment 2318674


Simiyu upatikanaji wa maji safi na salama kwa mwaka 2020/21 nilikuta ni asilimia 56% leo tumefikia asilimia 73% na hii ni kufikia Juni 2022 lazima wana Simiyu kumshukuru Sana Rais Samia Suluhu Hassan,

Kafulila anasema, Lakini Rais Samia huyu huyu tayari ametuletea mradi mkubwa wa bomba la kilometa 190 kutoka ziwa Victoria wenye thamani ya Shilingi billioni 400.

Ndugu zangu Wanasimiyu mradi huu utapita zaidi ya vijiji vyenu 200 ambao kazi za awali nadhani mnaona zimeanza,Asanteni Sana kwa ushirikiano wenu huu mkubwa,


View attachment 2318676
Mhe David Kafulila akikishukuru Chama cha Mapinduzi mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano katika kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi 2020/25

Kafulila anaendelea kusema, Niwambie ukweli, Nimesoma bajeti za miradi ya maji za miaka 20 mfululizo kuanzia ile ya mwaka 2000 mpaka ya mwaka 2020,

Nataka niwaambie kwa miaka yote hii hakuna mwaka ambao fedha za miradi ya maji zilitolewa hata kwa asilimia 80%.

Lazima mfahamu,Bajeti ya kwanza tu ya awamu ya sita( 2021/22) fedha za miradi ya maji zilizotolewa ni billioni 743 sawa na asilimia 95% ya bajeti iliyopitishwa na bunge na hii ni ndani ya miezi 9 tu Sio mwaka.

View attachment 2318677
Mhe David Kafulila akimkabidhi Mkuu mpya wa Mkoa "SIMIYU MODEL" inayotamka kuwa "IF NO CASH THEN NO COTTON-SIMIYU"


Mhe Kafulila anaendelea kusema,Huu ni ushahidi mwingine kuwa Rais wetu anatekeleza kauli mbiu yake ya kumtua ndoo mama kichwani kwa vitendo.

Rais Samia anaelewa kuwa maji ni uchumi, maji ni ustaarabu, maji ni afya... Maji ni Uhai,

Mtakumbuka,Ripoti ya shirika la Afya duniani mwaka 2014 ilionesha kuwa kwenye kila dola moja inayowekezwa kwenye maji, inaokoa dola 4.2 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi na salama( UN- News, Nov19, 2014).

Hivyo hivyo billioni 743 za miradi ya maji katika mwaka mmoja wa Rais Samia wa 2021/22 ni sawa na kusema Rais wetu kaokoa Shilingi trilioni 3.1 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji.

Kafulila anaendelea kusema, Labda niwakumbushe tu kwamba utafiti uliofanywa na taasisi ya SYNOVATE mwaka 2008 ulionesha kuwa kero namba moja kwa mtazania ni maji.

Msiojua,SYNOVATE ni taasisi 5 kwa sayansi ya uratibu wa maoni duniani wakati huo kabla haijachukulia na IPSOS ambayo kwa sasa ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kazi hiyo(OPINION SURVEY).


View attachment 2318697


Mkuu huyu wa mkoa anasema, Hiki ni kielelezo kuwa Kiongozi anaetatua tatizo la maji anagusa maisha ya watanzania walio wengi na hasa vijijini ambao inawezekana hawana kelele nyingi kwenye mitandao..wanaitwa ' silent majority'..Hivyo tunaposema Mama anaupiga mwingi sio sisi ni takwimu za kitafiti.

Hivyo tuendelee kuwasaidia wananchi kwa kuhakikisha wakandarasi wanatekeleza mikataba na tuendelee kuvunja mikataba ya wababaishaji kama tulivyofanya siku zote kuhakikisha kuwa fedha anazoleta Mhe.Rais kukabili kero ya maji zinafanya kazi kwelikweli,


View attachment 2318678
Mhe Dkt Yahya Mawanda akiwalisha wafanyakazi wenzake keki kama ishara ya unyenyekevu wake kwao

Hayo yamesemwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kati yake na Mkuu wa Mkoa Mpya Mhe Dr Yahaya Mawanda ambapo mbali ya kueleza sura ya Mkoa wa Simiyu, Kafulila ameelezea pia maamuzi tisa ( 9 ) ya kimkakati aliyoyatekeleza ndani ya mwaka mmoja na mwezi mmoja wa Utumishi wake katika nafasi ya hiyo ya Mkuu wa Mkoa huo wa Simiyu kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Ndo njia pekee ya kufikiriwa upya, sijui tulaumu ujamaa
 
Acha kujitoa fahamu kama Kabundi na Pole pole, nenda kasome tena rasimu ya Warioba.
Sawa lakini kwanini msituoneshe mfano na Sisi nyie Chadema?

Chama kina miaka 30 kimeongoza na baba na mtoto tu kwa miaka yote
 
Back
Top Bottom