Uchaguzi 2020 Hatimaye Gwajima, Pengo na Makonda Wamekutana Pamoja kwa furaha kubwa

Nimeona ni Kwa nini MUNGU aliona ni vyema amuepushe Lissu na kifo huyu MTU ni habari nyingine.
Mkuu mimi pia nimeendelea kuona ulichokiona, huyu mtu si wa kawaida, msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, "Hakuna mwanaume wala mwanamke awae yote ktk nchi hii kwa sasa mwenye ubavu wa kumtwanga Magufuli maneno machungu kiasi hicho! Iwe ni wakati wa kampeni ama usio wa kampeni.
 
Asante kwa Madini Mkuu
 
Mlivyo mtukana na mwenzako Gwajima hamkujua kama ni mzee wenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi maisha yangu yote kumtukana Pengo zaidi ya kumsifia

Huyo mzee ukitaka kugombea akikuwekea mkono wa haraka au kukutamkia neno lolote la heri lazima kushinda

Ndio maana CCM haijawahi dharau huyo Kardinali zaidi ya kuheshimu tofauti na Chadema

Gwajima alimtukana kardinali Pengo alipokuwa Chadema Kitivo Cha matusi Tanzania kaja CCM kaujua ukweli kuwa kuna wazee hawatukanwi au kudharauliwa hata siku moja ikiwemo huyo Kardinali Pengo kaenda kumuona
Huyo ni mzee mzito sio wa kuchezea wala kudharau
 
Makonda ana akili kuliko gwajima, na huyo gwajima kanisa linakufa kakimbilia kwenye siasa Mungu hamfichi mnafiki
Hivi wafuasi wa kanisa lake wote ni Wana ccm?? Halafu ikumbukwe 2015 huyu the so called Bishop alikuwa anaombea mikutano ya chadema! Binafsi namuogopa sana Gwajiboy!!
 
Silipendi hilo jamaa tangu liliposaliti maaskofu kwa vipande thelathini vya ccm...
 
Hivi wafuasi wa kanisa lake wote ni Wana ccm?? Halafu ikumbukwe 2015 huyu the so called Bishop alikuwa anaombea mikutano ya chadema! Binafsi namuogopa sana Gwajiboy!!
Gwajima ni ndumilakuwili tu sijui ilikuwaje ccm wakamchagua na kumwacha yule kijana aliyeshinda kura za maoni sasa matokeo yake watu inabidi tu wamchague mdee Tena. Gwajima ni kirusi hatari Ngoja magufuli msukuma mwenzake amalize mda wake atarudi upinzani gwajima ni tapeli lilo chini ya mwavuli wa dini
 
Wewe na kaka yako Gwajima mlimtukana sana nyie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes hapo ndo napoipendea siasa hakuna rafiki/adui wa kudumu.gwaji boy.
 
Wale tuliokuwa tunashadadia ugomvi yatushuke sasa! Ukiona ndugu wanagombana kashike jembe ulime! Hao wote Ccm chama dume! Ndo wameshaunganisha nguvu, chandimu na halima mjipange!
 
Lissu ni habari nyingine kabisa maana hata sasa ameweza kumteka Jiwe awache kunadi alivyo nunua ndege na kujenga madaraja sasa hivi kila mkutano ni kumjibu Lissu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kweli ukikubali kuolewa, ujue yakupasa kulala uchi, huyu Unoboy na kiburi chaka chote anajikomba kiasi hiki??
I wish I cud be mbunge!

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…