Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio cha Wastaafu na hivyo imepandisha Malipo ya Mkupuo kutoka 33% hadi 40%

Pia, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameagiza kuongezwa kwa malipo hayo kwa Wastaafu waliokuwa wakilipwa 25% sasa watalipwa 35% katika Mwaka huu wa Fedha

====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
kwanza hii hela ni serikali au ya mtumishi? kwa nini umpangilie mtu hela yake cha kuifanyia? wangeweka sheriak kuwa nusu atapewa ,nusu nyengine iwekwe UTT
 
UVCCM tuko kwenye kikao hapa tunajiandaa kumsifia mama.. Kwa kweli anaupiga mwingi 😅
 
Shida ninayo iona mimi kwenye pension sio hiyo asilimia ya ‘lump sum’ iwe 33%, 40%, 50% ata 100%.

Shida ipo kwenye replacement ya 1/580 hapo ndio kwenye tatizo ni ndogo sana hiyo ndio inafanya upate hela kidogo wakikokotoa.

A fair replacement rate inatakiwa kuwa between 1/100 to 1/150 a good rate 1/below 100.

Sasa replacement rate ya 1/580 they can afford to pay that bila ya hata kufanya investment zozote, kama awawezi lipa hata lum sum ya 100% kwa replacement rate hiyo maana yake hela inachezewa sana huko na hakuna uwekezaji wa maana.

Watu wanaofanya uwekezaji mzuri on average baada ya kustaafu unapata pension ya between 65%-70% ya mshahara wako.

Kutokana na replacement ya 1/580 hela inakuwa ndogo sana ndio maana watanzania mnalilia lump sum, ili mfanye biashara mkistaafu.

Wakati shida ni replacement ingekuwa nzuri na watu wanapata hata 50% ya mshahara wao sidhani kama kungekuwa na makelele ya asilimia za lump sum.

Badala ya kupambana na kiini cha tatizo, ni watu mliokubali matokeo sasa hivi mnapambania kupunguza makali ya kuishi na hiyo dhulumati ambayo mmeikubali.
 
Kwanini wasiweke 50-50!
This how was before it changed to 33%.

Tulipokuwa kwenye 50% (lump sum) na 50% (monthly pension), hakukuwa na mstaafu aliyekuwa ana complain.

Ghafla jamaa hawa (CCM) wakatuingiza kwenye mgogoro wa 33% halafu haohao CCM - serikali wakajitengenezea na sababu ya mabadiliko hayo.

Hii serikali ya maCCM ni ya ajabu sana. Imekaa kiwiziwizi tu kwenye kila eneo na kila sekta.
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Wapeni watu hela zao acheni wizi.
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
hukata upesi kama huna akili mwachetu achukue chake alale mbele kwamba unataka kudanganya jamii kwamba serikali inawapenda sana wananchi wake? kama kuna sehemu hawana maji safi na salama na serikali haichukui hatua iweje iwapende wafanyakazi kwemye kustaafu kwao.....
 
Hivi hiyo monthly payment huwa inategemea vigezo gani? Kwa mwalimu anaweza kupata ngapi kwa makario eg kama atalipwa 40% kwa mkupuo.
1. Swali la kupata ngapi sio universal. Inategemeana na number of factors

2. Baadhi ya factors zinazo determine lump sum payment (40%) na pension ya kila mwezi ya mstaafu yeyote ni:

(a) Mstaafu ni member wa mfuko upi.

(b) Muda aliofanya kazi kabla ya kustaafu. Miaka michache basi, matokeo yake ni kiinua mgongo na pension kidogo; na miaka mingi kazini, kiinua mgongo na pension kubwa pia

(c)Kiwango cha mshahara ulichokuwa unapata kabla ya kustaafu: Mshahara mkubwa, basi inakupa kiinua mgongo na pension kubwa na mshahara kiduchu, tegemea pia kupata kiinua mgongo na pension kidogo

Mathalani mtu mwenye mshahara wa 1,500,000 mpaka wakati anastaafu, hawezi kuwa na kiinua mgongo na pension sawa na mtu aliyestaafu na mshahara wa 3,000,000 na wote wakiwa wametumika miaka 35 labda!!
 
Shida ninayo iona mimi kwenye pension sio hiyo asilimia ya ‘lump sum’ iwe 33%, 40%, 50% ata 100%.

Shida ipo kwenye replacement ya 1/580 hapo ndio kwenye tatizo ni ndogo sana hiyo ndio inafanya upate hela kidogo wakikokotoa.

A fair replacement rate inatakiwa kuwa between 1/100 to 1/150 a good rate 1/below 100.

Sasa replacement rate ya 1/580 they can afford to pay that bila ya hata kufanya investment zozote, kama awawezi lipa hata lum sum ya 100% kwa replacement rate hiyo maana yake hela inachezewa sana huko na hakuna uwekezaji wa maana.

Watu wanaofanya uwekezaji mzuri on average baada ya kustaafu unapata pension ya between 65%-70% ya mshahara wako.

Kutokana na replacement ya 1/580 hela inakuwa ndogo sana ndio maana watanzania mnalilia lump sum, ili mfanye biashara mkistaafu.

Wakati shida ni replacement ingekuwa nzuri na watu wanapata hata 50% ya mshahara wao sidhani kama kungekuwa na makelele ya asilimia za lump sum.

Badala ya kupambana na kiini cha tatizo, ni watu mliokubali matokeo sasa hivi mnapambania kupunguza makali ya kuishi na hiyo dhulumati ambayo mmeikubali.
Yes, kinachopaswa kufanyika sasa ni pamoja na kurekebisha kanuni hii ya kimahesabu ya ukokotoaji wa kiinua mgongo na pension za watumishi.

CCM ni wezi tu by nature na kujipendelea wao na familia na matumbo yao.

Wafanyakazi wa umma wanaweza kushangalia kuiona asilimia 40 au 50 na hata 70 lakini kumbe wanakuja kukamatiwa kwenye kanuni ya ukokotoaji mafao yao!!
 
Kwa nini mtu asilipwe hela yake yote? Mtu kafanya kazi kwa asilimia 100 kwa nini alipwe asilimia 30 ya mafao yake? Kwa nini wabunge wao wanachukua mzigo wote hamuwawekei hiyo pesa? Hiyo asilimia inayobaki kwenu ndio mnaichezea kwa safari zisizo za lazima. Hebu hili lifike mwisho sasa. MTU CHAKE APEWE!
Nadhan ingekuwa ni OPTION ili kila mtu achague.

Shida maamuzi mengi hufanyika kwa idea ya mtu mmoja tu ; while decision Kama hizo zilitakiwa ziwe evidence based statistically significance kwamba based on findings
Ulichunguza wastaaf wengi are not satisfied na hii kitu , govt inatumia mabavu kuwa mfuko utakufa,

maafrica ni matumbili, hivi why can’t they cut off expenditures , ma vi 8
, mishahara ya wabunge, mfano Rais mstaafu anakula 80% ya salary Yake ya 198M plus mke wake pia zote hizo za nini wakati majitu hayo ni majizi tu ; safari za Rais zipunguzwe akae ofisini afanye kazi, peediem ya Rais na jopo lake ni pesa ndefu…. Why hawa focus kwenye kuminimize hizo cost ambazo ni sio muhimu.

Mtu anastaafu akiwa na 60 , unampa 40M , anakufa at his 66, hiyo sio dhulma, ?

Serikali ya TZ ya hovyo snaa . Ila siwalaumu. Tatizo kubwa wasomi hamtàki kujipenyeza , chukueni form muingie bungeni , msiache standard 7 failures ndio wawatungie sera, tatizo lingine hata wasomi nao wakifika juu wakipewa ofisi wanakuwa machawa. Serikali, wananchi na wasomi wote ni sehemu ya tatizo.
Mkufe tu , tulishachomoka na tuliona mapema TZ hakuna maisha, ni Jehanam ya duniani.

Katika position ya Urais , kipi Samia anafanya ambacho JPM, JK BEN hawakuweza kufanya, yote yanayofanyika TZ Hata wewe unaesoma ukipewa nchi you can do the same .hakuna viongozi ambao ni bright na wanaoitazama TZ in the next 50 years to come . Wengi wanaangalia usawa wa pua zao ndio mana ni majizi na wabinafsi
 
hukata upesi kama huna akili mwachetu achukue chake alale mbele kwamba unataka kudanganya jamii kwamba serikali inawapenda sana wananchi wake? kama kuna sehemu hawana maji safi na salama na serikali haichukui hatua iweje iwapende wafanyakazi kwemye kustaafu kwao.....
Sio kwamba kama huna akili Miaka 60 akili inakuwa imezeeka haiko sharp kama ujana uongo kusema MTU ana Miaka 60 akili ndio itaamka uongo

Akili gani inaanza kuchaji Miaka 60 Miaka yote kafanya KAZI haikuchaji ndio ichaji Miaka 60 uongo

Aishi Tu Kwa monthly pension iwe Tu iko vizuri

Miaka 60 mwajiri anaamini uwezo WA akili umefikia ukomo huko mitaani Ndiko MTU ataweza? Uongo
 
Walitakiwa kupiga hesabu na riba ya pesa kwa kipindi chote walicho kaa nazo.
Maana walikuwa wanafanyia biashara na kupata faida ndefu tu.
 
Walitakiwa kupiga hesabu na riba ya pesa kwa kipindi chote walicho kaa nazo.
Maana walikuwa wanafanyia biashara na kupata faida ndefu tu.
Riba imo ndio maana mstaafu analipwa pension hadi siku Anafariki ya kila mwezi bila kujali alistaafu ataishi Miaka 40 toka kustaafu

Uzuri mifuko ya pension ukiomba statement ya michango yako yote uone ulichochangia na mwajiri waweza kiona na waweza Fanya hesabu mwenyewe kama hicho kipesa xhako kiduchu kila mwezi ungeweka fixed deposit badala ya kwenda mifuko ya pension unapostaafu ungepata shilingi ngapi kama wangekuachia hicho kipesa unakatwa pension kuwa kawekeze mwenyewe ili usitisumbue kustaafu

Wengi wangestaafu malofa WA kufa MTU

Waliobuni mifuko ya pension na monthly pension waliona mbali Sana
 
Wsliona mbali wapi ?
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Mkuu wastaafu waachiwe wajiamulie wenyewe namna ya kutumia hela yao, serikali iangalie namna ya kuwalipa kifuta jasho kwa kuitumikia serikali na Taifa kwa ujumla.
 
Wsliona mbali wapi ?
Wajinga wanaostaafu Miaka 60 halafu wanadhani ndio mwanzo WA maisha wakistaafu wakati wamefanya KAZI serikalini au taasisi zake Miaka kibao wakiwa na mishahara na marupurupu kibao na heshima kibao na connection hawajufanya lolote la maendekeo kujipanga wakisubiri kustaafu

Mitaani MTU serikalini au taasisi zake akistaafu hata awe bosi anaonekana bwege Tu hakuna WA kumnyeyekea tena mitaani wala kijijini wala kujikomba kwake His or her glory days are over hata akigombea ujumbe wa nyumba Kumi aweza pigwa chini

Sasa kama kuna bwege mstaafu anategemea Kikokotoo kimtoe kimaisha mjinga hajielewi MTU umefanya KAZI Miaka yote hujatoka kimaisha unasubiri kikotoo jiandae kufa mapema Kwa frustration kama huna Cha maana ulijiandaa omba tu Hela ya mkupuo iwe ndogo ila monthly pension iwe kubwa ili Cha mwezi kiwe kikubwa

Nashauri kama mtaalamu
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Hiyo mothly pension ziliongezwa hela ndogo kiasi kwamba hilo ongezeko ukilichukua kwa miaka 12 ilikuwa haifiki 17% ya mkupuo uliopunguzwa kutoka 50% - 33%
 
Back
Top Bottom