YNIM
JF-Expert Member
- Aug 29, 2007
- 2,215
- 25
Field Marshall keshasema ni kifo cha ghafla
labda umeme ulikatika...najua jamaa mmoja(jewish) alivuta mwaka jana kidizaini ya hitlafu ya umeme akiwa kwenye life support nyumbani!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Field Marshall keshasema ni kifo cha ghafla
Field Marshall kesha recover credibility?
Field Marshall kesha recover credibility?
life support nyumbani inawezakana.........na hakuna sheria inayokataza bila exceptions!!! asante.
..bado kuna ile ya, "mji wa state ya Boston......informations za wagonjwa zinapatikana kwenye internet." nilipoisoma nilihisi matumbo yanakatika, if you know what i mean.
Thats a good answer to my question. Nasubiri majibu ya gharama ya kuikodi (as if.....).
Asante ES kwa taarifa kuwa hakuwa kwenye life support. Kinachonisumbua pia ni upungufu wa akili ya viongozi wetu. Wamezoea kudanganya watu na kutokana na hilo wanajaribu kui-melodramatize kifo cha huyu mwizi..oops! mheshimiwa, then what!! kwa faida ya nani?? Tumebaki na theories nyingi na hakuna majibu ya uhakika.
I pity his family and the legacy anayowaachia maana ukioa mtu toka kwenye ukoo ule utajulikana na ukoo wenye kasoro kadhaa wa kadhaa. What a bad legacy, na spin doctors wa kibongo are having their field day.
Poleni mliobaki
Listen. Kali kuliko zote ni aliposema yule dogo wa UCONN hajui huu msiba, lazima angeambiwa. Niliposoma nikasema, umesema nini? I don't believe FMarshall uttered those words!
Yani bado nacheka mpaka sasa hivi.
Can you imagine? I mean ha haaaaaaaa! This is nutso!
...gross distortion of facts!!!! hospital itakayo thubutu, itafungwa sio tu na serikali ila hiyo mi-law suits!! wabongo Ma-MD Boston mmmmmmmmmmmh siri yangu....lakini haijatulia!!! no offense mkuu FMES...happy memorial day weekend.
insuarance wata-foot the bill..kwani kiukweli ni cheap hata kwao kwa mgonjwa kuwa home zaidi ya kuwa hospitali!!! hii utokea mara nyingi sana wagonjwa hasa wanao/waliolipwa mipesa ya ku-sue aidha ajali au medical malpractice....family uamua kutake care home(hata kama yupo kwenye life support) ili kusave ngawira!!! kwa ufupi its cheap....bluecross/blueshield watachekelea kama fisi akiona mfupa..simply hii itaokoa mipesa mingi kwao!!
huyu mtu kwanza yupo busy na safari yake ya Bongo....sometime in the next five dayz!!! habari hana....
I dont wanna pile on, or anything. Lakini tatizo ni kubwa kuliko FMES. Ni idadi ya watu wanaotegemea, wanao live and die na data za Mshikaji. People just gobble up whatever the man feeds them, no questions asked. And you come to find out the source is a college Kid got here a couple of years ago, and who doesn't even live in Boston.
I mean kama hujui kwamba University of Connecticut maybe - just may be - iko Connecticut, ngoja ni cheki, you probably can't figure out jack about the sources you get info from!
Duuuh!
Halafu serikali ndio iliyokuwa ikimlipia gharama za matibabu..Sasa ndio kweli gharama ziliangaliwa hapo?
Serikali ilikuwa ikimwandikia nani hizo cheki? Je walikuwa wakitoa hizo pesa za matibabu kwa
Ballali binafsi ama insurance company ama direct to the Pivate doctor/hospital?
Nimesema na ninazisimamia dataz zangu, kuwa Marehemu Balali, alikwenda US akiwa anaumwa akalazwa hospitali na hatimaye kupona kabisaa alitoka hospitali mwezi wa pili, since then hajaumwa tena mpaka majuzi alipofariki ghafla,
Na ninarudia tena kuwa waliokuwa na interest kubwa against Marehemu, ni awamu ya tatu, looking forward kuchambua facts I mean mnyonge mnyongeni lakini ukweli uwekwe wazi! Na hatuna uoga kwenye hili, hakukuwa na life support sio ukweli, hizi ni hadithi zinazorushwa na watu wasiokuwa wema, mchukie mtu kwa sababu lakini akitangulia kwenye haki imetosha muache!
And you come to find out the source is a college Kid got here a couple of years ago, and who doesn't even live in Boston.
Mkuu Mtanzania,
Sina sababu yoyote ya kuwayumbisha wananchi hapa, kwa sababu sijawahi hata siku moja sijawahi kuwayumbisha hapa wananchi an dataz zisizokuwa na ukweli, sasa mkuu wangu kama as far as this ishu ya kifo, niarudia kuwa ni kweli amefariki Jumapili usiku tena ghafla bila ya kutegmewa na atazikwa kesho kwenye hayo makaburi niliyoyasema.
Mkuu Kuhani,
Sijakuelewa ulichosema, kwenye ujumbe wangu wa jana nilisema kuwa hoja ya msingi niliyoiweka ilikuwa kwamba Balali hajafariki, na kwamba hakufariki Boston, na nikaweka all the reasons kwa nini ninaamini hivyo, na sasa imethibitishwa kuwa maneno yangu yalikuwa kweli kuwa hakufariki Boston, na wala hakuwa amelazwa kwenye Hospitali yoyote ya Boston,
Sasa hapa ni lazima niweke wazi kuwa wewe akili zako sio sawa mkuu kwa sababu unachotafuta ni cheap umaarufu, lakini hapa JF nafikiri unapaswa kuelewa kuwa unaanza kuchekesha, kwa sababu hoja huna, dataz huna, ukweli huna, facts huna, unajua watu wa aina yako huwa wana vichwa vikubwa sana lakini ndani hewa tupu, wewe kilichokuleta hapa JF ni agenda ya CUF, ukaamini kuwa watu hapa ni wajinga sana utawa-divide and rule, sasa unaona kila unachojaribu hakifanikiwi,
Wamekutuma uje hapa ujaribu kumuweka Salim vizuri ili labda agombee na CUF ambayo ndio the agenda hapa tuko macho na imar sana, sasa unaendelea kuhangaika hangaika, wewe ni mdini wa kiisilamu na unapenda sana waarabu, niasema hivi kuwaamusha wale ambao hawajakushitukia kuwa huna nia njema na hii forum, na ninakuhakikishia kuwa tutakukabili ipasavyo tena kwa lugha na vitendo unavyoonekana kuvielewa vizuri zaidi, hao waarabu waliokutuma waambie kuwa tupo macho mkuu!
JF mbele Zaidi!
ijumaa ishaanza ? namtafuta brazameni aje pamoja na injinia moh'd !
Habari hii hapo chini ime confirm mambo kadhaa na pia kubakisha baadhi ya maswali yafuatayo:
1)Ballali alishaamua kuwachukia watanzania kama vile walivyoamua kumchukia.
2)Hakutaka kujisafisha licha ya kwamba alikuwa na nafasi hiyo badala yake akachagua kususa kwa visingizio ili kuonekana ameonewa.
3)Alikuwa akifanya shughuli na shirika la fedha duniani kwa miaka 23 hivyo ni mtu kubwa mwenye connection kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri!
4)Na baada ya hapo akaletwa Tanzania na inaonyesha alikuwa kama expert kutoka nje na si mtz
5)Ballali aliamua kuwa betray wananchi kama vile anavyofikiri na sisi tuli mbetray!
6)Alijua kuwa hatarudi halafu then akaumwa?
7)Alisema kuwa hatarudi hata kama ni mzima ama amekufa...Hivyo basi kama muda wa kumhitaji ulifika halafu akafa ghafla...Ni kwasababu ya presha,ama alijiua ili asirudishwe,ama amefake kifo!
8)Aliwaaminisha watu kuwa hatapona..atakufa na hawataonana hata kabla hajaanza kuumwa!
Alijua haponi!
2008-05-22 16:24:05
Na Mwandishi wetu, Jijini
Wakati Watanzania wakiwa bado kwenye mshtuko wa kifo cha utata cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT, Dk. Daud Balali, imebainika kuwa marehemu alishajua kitambo kuwa kutokana na mazingira yaliyomzunguka, kamwe asingeweza kupona.
Habari ambazo Alasiri imeweza kuzipata toka kwa chanzo chetu nchini Marekani na pia kwa baadhi ya jamaa wa karibu wa marehemu walioko nchini, zimeeleza kuwa marehemu alishajua hata kabla ya kuondoka nchini na kwenda kutibiwa Marekani kuwa asingeweza kupona.
Wakasema kabla ya kuondoka, marehemu aliwaaga baadhi ya ndugu kwa namna ambayo iliashiria wazi jambo hilo, kuwa alishahisi haponi.
Wakaeleza kuwa ugonjwa uliokuwa ukimkabili, kutojua kwake kuwa nani ni adui na nani ni rafiki wa kweli, ni baadhi ya mambo aliyoonekana wazi kuwa yalikuwa yakimsonga na kumfanya awe katika hali ya kumfanya ahisi kuwa haponi.
Aidha, tuhuma nyingi zilizokuwa zikielekezwa kwake, na ambazo kwa bahati mbaya hakuwahi kupata nafasi ya kuweza kuzijibu, ni sababu nyingine wanazosema zilimfanya awe katika hali ya kukata tamaa.
Chanzo kilichopo Marekani kimesema, kabla ya kufikwa na umauti, marehemu alikuwa akilalama kila wakati kuwa kutokana na yote yaliyomzunguka, kamwe asingeweza kupona na wala hana haja ya kupona kwa sababu alishachafuliwa kiasi cha kutosha.
Kikasema chanzo hicho kuwa marehemu aliacha wosia, akisema kuwa dunia haina haki na hivyo imemhukumu mapema.
Kikasema chanzo hicho kuwa marehemu akawaambia wakati akienda Marekani kuwa `harudi tena Bongo, awe hai ama amekufa`.
Kikasema chanzo hicho kuwa Dk. Balali aliamini kuwa siku zote alikuwa msafi na mchapa kazi mzuri, lakini tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwake hazikuwa na uwiano mzuri wa kumtendea haki.
Imeelezwa kuwa Dk. Balali alifariki Ijumaa ya wiki iliyopita mjini Boston huko Marekani.
Hata hivyo, kifo cha Dk. Ballali kimezua utata hasa baada ya Serikali kutothibitisha mapema, huku baadhi ya ofisi zikiwa zinarushiana mpira juu ya jukumu la kueleza msiba huo.
Baada ya jana waandishi wa habari kuhaha katika kusaka uthibitisho wa taarifa hizo, hatimaye ikathibitishwa jioni na Afisa Uhusiano wa BoT, Bw. Emmanuel Mwero huku kukiwa hakuna fursa yoyote kwa waandishi kuuliza maswali.
Kabla ya kuteuliwa kuwa gavana wa Benki Kuu mwaka 1998, marehemu Dk. Balali aliwahi kulitumikia Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, kwa miaka 23.
Baadaye, Dk. Balali akarejea nchini na kuteuliwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Benjamin Mkapa, kuwa mshauri wake wa masuala ya uchumi.
Mwezi Julai mwaka 1998, Dk. Balali akateuliwa tena na Rais Mkapa kuwa Gavana wa Benki Kuu nchini, BOT.
Hata hivyo, Januari mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, alisitisha uteuzi wa Balali katika nafasi ya gavana na kumteua, Prof. Benno Ndullu, kushika nafasi hiyo.
Hatua hiyo ya Rais Kikwete ilitokana na taarifa za uchunguzi uliofanywa ndani ya BOT na Kampuni ya Ukaguzi ya Kimataifa ya Ernst & Young kubaini upotevu wa Sh. Bilioni 133 zilizolipwa isivyo halali kwa makampuni 22, kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje, EPA.
Tangu taarifa hizo za upotevu wa mabilioni ya walipa kodi yaliyochotwa kifisadi na makampuni 22, marehemu Balali akawa gumzo, hasa kutokana na ukweli kuwa wakati hayo yakitendeka, yeye ndiye aliyekuwa kinara wa BOT.
- SOURCE: Alasiri