Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.
mkuu FMES.

Mie bado sitaki kuamini hili suala mpaka nione mwili wa Balali ukizikwa,mambo ya kulishwa achanga la macho simo.

ndio maana nimekaa kimya kwa muda nikitafakari hili suala,nitakuja kukielezea nacho kijua kuhusu balali.

ila what i know balali alikuwa Mgonjwa siku nyingi sana hata kabla ya mwaka jana.

Mkuu Gembe nipo pamoja nawewe katika hili, siamini kabisa kwamba Kafa Balali pamoja na kwamba swala la kwamba alikuwa mgonjwa lilijulikana siku nyingi yeye pamoja na swahiba wake Liumba jinsi walivo kuwa wakipeana mipira ya kona kufunga magori ya nguvu!

Kinacho nifanya nisiamini ni hii coincidence ya taarifa za kukinzana za kifo chake, jinsi mambo yanavo pelekwa pelekwa, na huu mgongano kwamba miezi sita ya uchunguzi wa EPA inakaribia!
lakini kikubwa zaidi, usiri wa nini katika msiba??? hivi mtu umefiwa na mume/baba/mtoto badala ya kukaa na huzuni na simanzi kubwa unabaki kukimbizana na media/ watu ili wasimuone marehemu wala kujua kwamba kafa? for what?
 
1.
FMES huwa hupendi kuswalishwa na maswali unayoyaita logic. Ulicho kiongea hapo huwa huki-practice.

Mkuu wewe una matatizo yako ya binafsi ambayo siwezi kukusaidia kuyatatua, ninakuelewa kwa sababu kuna watu kama wewe waliowahi kuja hapa na kikimbia bila kuaga, mimi siwezi kukujibu maswali yanyohusiana na dataz, lakini sina tatizo na hoja, wewe weka hoja nitakujibu hoja, ili kuuliza dataz unahitaji kuwa na dataz zaidi ya dataz nilizoweka, hilo ndio so far linakushinda, kwenye ishu ya Chenge umejaribu kulilia search warrant, watu wengine walipothibitisha kuwa ni kweli chenge alipekuliwa hukurudi tena,

Kwenye hii ishu hata unacholilia sikioni, zaidi ya chuki zako binafsi kwangu na jina langu ambalo halikutoki kila unapoingia hapa, mimi ninakuona sawa tu na member wengine ingawa unajaribu sana nikuone kuwa tofauti, na kinachonifanya niite logic zako za chooni ni kwa sababu ya tabia yako ya kutumia majina mengi kunishambulia ili uonekane kuwa una point,

Kuna watu wengi sana hapa wananiuliza maswali ninawajibu, sasa ni tone zako ndio zinanifanya nikujibu kama unavyouliza kwa sababu nia na madhumuni yako ni kuharibu jina na credibility yangu hapa JF, kitu ambacho wengi wamejaribu kabla yako lakini wameshindwa kwa sababu ya kukosa ukweli, tofauti yao ni kwamba wewe ujna agenda yako ambayo ni kuivuruga hii forum kwa faida yako na waliokutuma, hilo nimekuahidi kuwa hutapata hiyo nafasi maana tunakujua tayari na majina yako yote hapa JF, sasa umauzi ni wako mkuu mimi sitishiki hata siku moja ujuha,

Ninaielewa vizuri sana strategy yako, ya kunishambulia seriously, halafu ukiona umeshidwa unajaribu kutumia utani utani, halafu unajaribu kujifanya kuwa wewe ndiye unaye-control the tempo, na kujaribu kuwavuta wengine waku-support kwa kutumia majina yako mengi sana hapa, ndio maana ninakuona kuwa ni juha!

2.
Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki? Pundit endelea kumtia disiplini!

Mkuu ni hoja kama hizi ndio ninaziiita logic za choooni, kwa sababu hiii picha sielewi inahusiana nini na hii topic, ndio maana ninakuita mjinga na juha na huna lolote la maana zaidi ya logic za choooni, sasa ninakuomba ukae pembeni ili wananchi ambao tuko serious tuendelee na mjadala, ukitaka sifa na umaarufu anzisha topic yako mkuu,

By the way vipi maandamano ya kwenda nyumbani kwa Balali bado unaendelea kuyatayarisha? au!
 
Mimi najiuliza;

1. Kwani iwapo kama ni kweli Balali amefariki kwa ugonjwa familia inaona kutakuwa na madhara gani iwapo wataweka msiba huo public.

2. Kwa nini hawaoni kuwa itawauma zaidi iwapo ni kweli Balali amefariki na watu bado wanasema hajafa kwa sababu hawaamini.

3. Ni sababu zipi hasa zinazompa huyu Mjane kiburi cha kufanya msiba private; iwapo kweli Balali amefariki.

My Take: Balali hajafa...time will tell also NAAMINI 100% kuwa Balali alikuwa Raia wa USA.
 
Jamani mwenye taarifa yoyote kuhusiana na maziko ya Ndugu yetu Marehemu Balali Aziweke hapa.
 
Mimi najiuliza;

1. Kwani iwapo kama ni kweli Balali amefariki kwa ugonjwa familia inaona kutakuwa na madhara gani iwapo wataweka msiba huo public.

2. Kwa nini hawaoni kuwa itawauma zaidi iwapo ni kweli Balali amefariki na watu bado wanasema hajafa kwa sababu hawaamini.

3. Ni sababu zipi hasa zinazompa huyu Mjane kiburi cha kufanya msiba private; iwapo kweli Balali amefariki.

My Take: Balali hajafa...time will tell also NAAMINI 100% kuwa Balali alikuwa Raia wa USA.

Yeboyebo,

Nakubaliana na imani zako zote mbili. Balali hajafa na pia ana uraia wa USA.
 
Tatizo ni kuwa ndugu zangu... hamjaanza kuuliza swali moja muhimu kweli in its proper context...when you do that.. baadhi ya majibu yenu yataclick "Aha"...
 
Tatizo ni kuwa ndugu zangu... hamjaanza kuuliza swali moja muhimu kweli in its proper context...when you do that.. baadhi ya majibu yenu yataclick "Aha"...

Mwanakijiji,

Tusaidie kutuulizia. Pia unaweza kutusaidia kutabiri maswali ya baadaye kama ulivyotabiri kifo cha Ballali.
 
3.
Ni sababu zipi hasa zinazompa huyu Mjane kiburi cha kufanya msiba private; iwapo kweli Balali amefariki.

Mkuu mengine sijui, ila kwenye hili nafikiri ni haki yake kulingana na facts nyingi alizonazo kuhusiana na kifo hicho cha mumewe against serikali.

Ninawafahamu watu wawili watakaohudhuria mazishi leo, na mmoja aliyekataa kwenda kwenda huko pamoja na kualikwa.

Ahsante Mkuu!
 
Nafurahia kuona kwamba kuna wana JF ambao hawataki kuamini kama Ballali amekufa kutokana na utata uliogubika tukio zima,lakini nawasihi kuendelea kujiridhisha japo taarifa ni za upande mmoja sana.

1.Timing ya taarifa za kifo chake kama mwana JF mmoja alivyokwishasema inaleta utata kidogo hasa ukizingatia kamati ya EPA ndiyo hiyooo inakaribia kumaliza muda wake!

2.Lakini kubwa zaidi kwa desturi na mila zetu nilitegemea kuona ndugu kama Kaka au mdogo wa kiume wa Daudi Ballali akiwa ndiyo msemaji mkuu lakini inaonyesha nguvu kubwa anayo mama!

3.Kutowashirikisha watanzania waishio marekani ukiondoa ubalozi nao unanitia mashaka kwamba there is something fishy hapa.

Lakini kama utata huo unatokana na giza tu lililogubika kashfa nzima ya EPA linalopelekea tuwe maTOMASO hata kwenye mambo ya kweli basi hiyo ni bahati mbaya.
 
3.

Mkuu mengine sijui, ila kwenye hili nafikiri ni haki yake kulingana na facts nyingi alizonazo kuhusiana na kifo hicho cha mumewe against serikali.

Ninawafahamu watu wawili watakaohudhuria mazishi leo, na mmoja aliyekataa kwenda kwenda huko pamoja na kualikwa.

Ahsante Mkuu!
Hapo manake more nuz coming.... safi sana
 
Serikali nayo imegawanyika kwenye kuamini kuhusu kifo cha Balali?
Mbona waliwapakazia BOT ndio watoe taarifa?
Hawataki kuingia mtegoni noma likisanuka!
 
3.

Mkuu mengine sijui, ila kwenye hili nafikiri ni haki yake kulingana na facts nyingi alizonazo kuhusiana na kifo hicho cha mumewe against serikali.

Ninawafahamu watu wawili watakaohudhuria mazishi leo, na mmoja aliyekataa kwenda kwenda huko pamoja na kualikwa.

Ahsante Mkuu!

FMES,

Heri ya huyo aliyekataa kwenda maana huko mchanga wa macho unarushwa kishenzi. Watu wanaweza kurudi nyumbani wakiwa hoi.

I hope wataruhusiwa kuuona mwili wa marehemu kabla ya kumzika.

Ninawaonea huruma tu kama watakuwa ni mashahidi wa kuzika gogo.
 
Ndani ya serikali kuna waliopewa muda wa kuimaliza hi noma na time ikaanza kurun out...Sasa waliotoa huo muda kwa wenzao ili wajaribu kuzima soo nao hawana imani 100% kuwa soo halitabumbulukiwa na hivyo ndio maana inakuwa ngumu kwa confirmation!
Kitabu chake cha kusaini cha rambi rambi hakuna hata kiongozi mkubwa wa serikali aliyesaini..Kwanini?
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Muda si mrefu funeral crasher number 2 ninaingiza timu kwenye msiba wa Balali ili kupata yaliyomo...

Mipango yote inakamilika na heshima zote zitakuwepo ikiwemo ya kuzima simu na mawasiliano ya intaneti. I have my fingers crossed here..

5
4
3

I will do it live... I will do it live.... (kwa hisani ya Bill O'reilly).

5
4
3
2
1

.........
 
1
. 2.Lakini kubwa zaidi kwa desturi na mila zetu nilitegemea kuona ndugu kama Kaka au mdogo wa kiume wa Daudi Ballali akiwa ndiyo msemaji mkuu lakini inaonyesha nguvu kubwa anayo mama!

Mkuu Heshima mbele,

Mjane ni kweli anayo nguvu kubwa kwa sababu hii ni ndoa iliyofanyika majuu, na unajua majuu ni kina mama ndio wanaokuwa -favored na sheria, na besides ndoa za majuu ni mke na mume tu, ndugu baadaye sana, ndio maana unaona kuwa mama anaonekana kuwa na nguvu sana ni sheria mkuu za huko majuu.

2.
3.Kutowashirikisha watanzania waishio marekani ukiondoa ubalozi nao unanitia mashaka kwamba there is something fishy hapa.

Ilishafahamika kuwa marehemu alikuwa akitafutwa kwa hiyo yes kulikuwa na usiri mkubwa sana kuhusiana na maisha yake huko majuu, usiri huu ulikuwa ni against serikali, sasa ninaamini kuwa ndio maana usiri unaendelea mpaka mwisho!

otherwise, maswali yako ni valid mkuu!
 
Na kwanini alikufa mara baada ya makechero kufika hapa?
Kwasababu kama that was the case then makachero hawakuweza kumuona na ndio maana serikali imeshindwa kudhibitisha kuhusu kifo na badala yake ni familia imepeleka taarifa kwa watanzania na serikali kwa kupitia BOT ambayo hakuwa mfanyakazi wake tena!
Ama pia kuna uwezekano wa sehemu kubwa ya utawala wa juu kusapoti mbinu chafu za kuwasafisha mafisadi bila kujua kuwa mapambano yatahamishiwa hata marekani ikibidi!
MPASUKO NI MKUBWA SANA NA SIRI SI SIRI TENA!
 
Kama ndugu wanavyogombana wakati wa misiba, wengine kudai wana haki zaidi kuamua Marehemu azikwe wapi, nani awe "mrithi" wa kutunza familia, nani agawiwe mali na majukumu mingine ambayo ni kawaida ya binadamu, Jumuiya yetu nayo iko katika mvutano huo huo.

Najiuliza je ni kawaida yetu binaadamu kuwa na mvutano kuhusiana na kifo na hasa wakati wa msiba? je hii ni ni kawaida wakati wa maombolezo?

Nimejiuliza ya fuatayo na maoni yangu binafsi na imani yangu pamoja na maswali haya ni kuwa Ballali hayupo nasi tena. I believe Daudi Ballali is dead and I pray that his sould rest in peace.


Maswali ni haya;
  • Je Ballali amekufa?
  • Ni nani ananufaika kwa kifo chake
  • Kama bado yupo hai na taarifa ya kifo ni ulaghai, ni kwa faida ya nani?
  • Je tuna haki gani kutaka kuingilia mambo ya binafsi ya familia?
  • Je kwa nini familia haitaki Ballali agwe na wananchi na kufanya msiba wake uwe jambo la familia tuu? ni wapi ule mshikamano wa kiafrika na utamaduni wetu?
  • Je ni kwa nini kumekuwa na usiri mkubwa kuhusu kuugua kwake na hata kifo chake? je mimi nina haki gani au wajibu gani kujua kuhusu Ballali? kwa nini kuna utata mkubwa katika kila kitu kuhusu Ballali?
  • Kifo chake ni pigo kwa nani?
  • Kama sababu za kifo chake ni kuuwawa kama wengi wetutunavyokisia, kudhania au kuzusha, je ni nani aliyetaka Ballali afe? Ni lini aliuawa? na ni nini kilitumika kumuua?
  • Ni siri gani ambayo amekufa nayo au kawapa familia, marafiki na wengine waitangaze?
  • Je kifo chake kina sehemu gani au mahusiano gani kuhusiana/katika uchunguzi wa tuhuma za ufujaji mali, uhujumu na ufisadi wa pesa za Taifa Benki Kuu?
  • Je kufa kwa Ballali kuna maafa gani katika vita ya ufisadi?
  • Je familia yake inaungana vipi wakati kuna mgawanyiko kati yao kuhusiana na mazingira mazima ya yeye kutuhumiwa, kuugua na sasa kufa?
  • Ni nani hao ambao wanatoa vitisho au wametoa vitisho na kutaka kila kitu kinachohusiana na Ballali kiendelee kuwa ama usiri, utata au mara nyingine kuwa ni uzushi? kwa faida gani? na ya nani?
  • Je alikufa lini na wapi?lipi ni kweli na lipi si sahihi?
  • La mwisho, kwa nini Familia ilitaka iwasiliane na Serikali kwanza kutangaza kifo cha mpendwa wao? kwa manufaa gani kama Ballali alishapoteza kazi yake na Serikali kudai haina taarifa au haijui Ballali yupo wapi? je kuna ukweli gani katika hili?
Kama nilivyosema awali, nimesikitishwa (saddened)na taarifa na kifo cha Ballali. naheshimu uamuzi wa familia na nawapa pole. Naheshimu uchu wa Watanzania kutaka kujua ukweli.

Nasikitika (disappointed) kuwa Ballai kaondoka na siri kubwa na hakuchuka fursa yeyote wakati akiwa hai (kama hakuwa anaishi katika vitisho na "kutekwa nyara") kutoa ushuhuda kuhusiana na kilichosababisha aidhinishe malipo makubwa ya EPA, CIS, Meremeta, Tangold ambayo yamegundulika kuwa yalikuwa ni batili na kwa makusudi ya kuhujumu uchumi na Taifa letu.

Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele, tugange kwa ya mbele. Katika sakata la EPA na BOT kutumika kuhujumu nchi, Ballali hakuwa Alpha na Omega, kifo chake hakijafunga au kusitisha uchunguzi.

Wale walio hai, Gray Mgonja, Basil Mramba na Ben Mkapa waje mbele na kutupa taarifa, ni vipi kulikuwa na upotevu, ufujaji na uhujumu mkubwa uliofanyika wakati wao wakiwa katika madaraka na kushikilia hazina ya Taifa? Ilikuwaje Ballali akaruhusiwa kuidhinisha malipo makubwa kiasi hicho bila kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mkubwa wake wa kazi?

Rest in Peace Ballali. You will forever be remembered.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Muda si mrefu funeral crasher number 2 ninaingiza timu kwenye msiba wa Balali ili kupata yaliyomo...

Mipango yote inakamilika na heshima zote zitakuwepo ikiwemo ya kuzima simu na mawasiliano ya intaneti. I have my fingers crossed here..

5
4
3

I will do it live... I will do it live.... (kwa hisani ya Bill O'reilly).

5
4
3
2
1

.........

Picha zinaruhusiwa ama ni word of mouth ndio utatuletea hapa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom