Hatimaye nimeanza mchezo wa kubet na mwanzo mzuri

Avicii

Senior Member
Joined
Sep 16, 2023
Posts
102
Reaction score
173
Habari zenu Wana Jamvi, hope ni wazima. Ebana, hatimaye katika harakati za hapa na pale, baada ya kuona washkaji stori zinazoongelewa ni za masuala ya kubeti, ikabidi na mimi niwaombe wanielekeze kutokana na kwamba nina ujuzi wa kutosha wa masuala ya soka.

Basi msela mmoja aka-download app moja kwa jina la Bet PAWA. Nikazama Mpesa, nikatia alfu tano. Kutokana na uchambuzi na mwenendo wa mechi, nikaamua kuchagua mechi kati ya Man City na Leicester. Nikaweka option ya “both teams to score,” nikachagua “no.” Wana wakawa wananiambia hiyo mechi wanafungana zaidi ya goli nne. Nikawaambia tulieni, mtaona mambo. Ndo kama unavyoona hapo chini.

Basi baada ya kupata huo mkeka, sikupooza damu. Nikaandaa mkeka mwingine wa timu tatu nao pia ukatiki. Sasa nimekaa najiuliza, mbona jamaa kila siku wanalalamika wanachaniwa mkeka wao wakati mi naona ni kazi rahisi? Na uelewa wako juu ya mpira. Nawasilisha, wakuu.
 

Attachments

  • Screenshot_20241230-090350.png
    154.6 KB · Views: 6
  • Screenshot_20241230-090429.png
    173.1 KB · Views: 12
Mkuu ili upate pesa nyingi katika hii betting basi kila pesa unayokula unaibet tena, kama ilivyo yote. Hapo utakua unakuza mtaji mkuu. Na hatimae siku una mtaji mkubwa unakula hadi milioni kumi. So hiyo yote uliyoshinda ibet tena. Na chagua both team to score. Mi nilianza na mtaji wa shilingi 500 (tamka mia tano), leo mtaji umekua nimefikisha laki 3 ninayobetia. So tupia yote tena mkuu uwahi kutoka kimaisha..
 
Mkuu mimi kwanza nilikuwa si mpenzi wa mpira mara ya kwanza na bet blindly japo nilikuwa na idea ya jinsi ya kuweka stakes, nilijikuta nimeweksa stakes za mechini za ndani ya siku 4. Niliweka 15000 na nikaja kupokea 245000 hivi. Nikaona mambo si haya nikawa addicted na kubet.
Baadaye nikahamia kwenye basket. Mimi stakes zangu ilikuwa ni kuanzia 50000 hadi laki mbili. Nikawa ninakula sana.
Ila upepo ulivyobadilika.... nilikuwa napigwa. Kuna siku nilipigwa pesa ndefu na ndipo nilisema naacha rasmi. Now ni miaka toka niache kubet.
 
UShauri mbaya huu. Abet kila anayokula si atapigwa zote sasa
 
Hakika Kama Jana naona washkaji wanaweka timu 15+ Sasa hapo unaanzaje kushinda
Yea ni kweli...

Kuna wakati unaziona odds 2 kabisa kwa kumpa liver over 2.5...

Ambapo ukiweka 10 inakuja 20 which is sio mbaya...

Lakini tamaa inakudanganya unaishia kuongeza mechi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…