Hatimaye nipo kazini. Shukrani kwa WanaJamiiforums kwa mawazo na ushauri wenu

Hatimaye nipo kazini. Shukrani kwa WanaJamiiforums kwa mawazo na ushauri wenu

Shikamoon wakubwa zangu wadogo zangu hamjambo?

Jamani kumekucha,ni siku nzuri ya jumatatu nafurahia mazingira nikiwa kazini,kuwa na kazi kuna unafuu na Raha fulani,yaani unaamka unajua naenda wapi,kufanya nini ni vizuri sana.

Ni wiki chache nyuma sikuwa na lolote la kufanya ,niliwaza kufanya hata biashara ndogo ndogo lakini Kwa msaada na Mawazo ya watu wa Mungu wenye mioyo Safi walinishauri vizuri na wapo walioniunganisha na watu hata kufikia kuwa kazini Leo hii kweli Dunia bado ina watu wenye ubinadamu.
Moyo wa kujali na kutambua Thamani halisi ya ubinadamu

Watu wa jamiiforum mbarikiwe kwakweli ,most of them mnatambua Thamani ya mwanamke,japo kuna kikundi cha watu wachache,eti hawezi kukupa msaada mpaka ulale naye na vijiahadi vyenu vya pesa ndogondogo,yaani unanitajia pesa ambayo mama yangu ananipa muda na saa yoyote nikitaka.

Tusitumie nafasi ya udhaifu wa mtu kutimiza matakwa yetu mabaya pamoja na kudhalilisha na kutweza utu wa mtu.

Siwezi kujiuza na kuwa Mtumwa wa dhambi aslani
Hongera Dada ila fanyia Kazi huu Ushauri wangu Kuntu. Ukipokea tu Mshahara wako wa Kwanza kama una Wazazi wako wape kidogo na jitahidi (uwezo ukiwepo) mtafute Mtoto Yatima mmoja au nenda Wodi ya Wazazi katika Hospitali yoyote ile kisha omba kuonana na Mzazi aliyezaa ila ana upungufu wa Chakula au Dawa na msaidie kwa ulichonacho.

Nina uhakika wa 100% kwa yatakayokutokea baada ya kufanya haya ya muhimu niliyokueleza hapa utakuja Kunishukuru GENTAMYCINE hapa JamiiForums.

Nimekupa Code muhimu ya Kubarikiwa haraka sana na Mwenyezi Mungu pasipo hata sijui kwenda kwa Mganga na Kujiganga.

Kila la Kheri.
 
Back
Top Bottom