Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

Umembamiza na rungu la masai [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Chumvi kuntu hizi, si tuonyweshe picha ya Sasa, hizo za zamani hazitusaidii sisi, naona wanatuchosha na kamaliza mb zetu
Huwezi kuona picha ya sasa kwasababu mwanga unatumia mabilioni ya miaka kufika huko. Na ili kuona kitu ni mpaka mwanga usafiri kutoka huko na ukifikie huku...
Usipo elewa hio, fikiria kuhusu sauti. Kuna ndege (hasa ndege za kivita) zinauwezo wa kukimbia zaidi ya spidi ya sauti (supersonic speed) ushawahi kuona fighter jets zikipaa? Utaona zinapita kwanza halafu sauti utaisikia baadae. Sasa kwa concept hii ndo iweke kwenye mwanga utaona ni kwanini Huwezi kuona nyota zilizo umbali huo kwa sasa...
 
"Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita."


Mkuu hayo maelezo hapo yana kiuchachu fulani hivi.
Sio taarifa sahihi, huwezi kuurudisha muda nyuma kwa kamera iliyotengenezwa leo..hizo ni imejinasheni tu kwa kutumia viashiria vya wazi
 
Antarctica is the only continent with no permanent human habitation. There are, however, permanent human settlements, where scientists and support staff live for part of the year on a rotating basis. The continent of Antarctica makes up most of the Antarctic region.19 May 2022

Hakuna wakazi wa kudumu kule, kuna kipindi baridi hufikia hadi -60
 
Ardhi ya Antarctica hailimiki. Ni jangwa la barafu... sasa hii ni mbaya zaid kwa kusupport uhai... kuna viumbe wanaoishi huko Antarctica kama jamii kadhaa za nyangumi, na muda mwingine penguins.

Lakin kiumbe kikubwa zaidi cha nchi kavu huko ni "Belgica antarctica"
 
Sio taarifa sahihi, huwezi kuurudisha muda nyuma kwa kamera iliyotengenezwa leo..hizo ni imejinasheni tu kwa kutumia viashiria vya wazi
Iko hivi... huwezi kuziona hizo nyota kwa wakati wa sasa. Na infact, kwa asilimia kubwa nyota unaziona usiku inakua ni muonekano wa mamilioni ya miaka iliyopita.

Kwanini?
Kwa sababu nyota izo ziko mabilion ya miaka mbali na dunia (light years away from earth). Kwa maana hio, nyota kama iko 1 billion light year away inamaana kwamba; kwa sipi ya mwanga, utaifikia hio nyota ndan ya miaka billion moja.

Na kama tunavojua, ili kuona kitu ni mpaka mwanga wake (au reflection) ikufikie kwenye macho. Sasa kitu kama kiko billions light years away inaamana hauto kiona mpaka baada ya huo muda.

Oh yea. Na hilo jua unavoliangalia wakat wa mchana, ujue unaliona lilivokua dakika 8 zilizopita (maana mwanga wa jua unatumia dakika 8 kufika dunian)
 
Daaah, kumbe nyie ndo mnaohisi tunaishi ndani ya Dunia? Kwamba ukitoka nje unatoboa? Daah, [emoji1]
 
"Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita."


Mkuu hayo maelezo hapo yana kiuchachu fulani hivi.
Hako kauchachu ndo ilipo logic yenyewe.
 
Nlikuwa nadhani hizi picha ndivyo zilivyo mpaka niliposoma juzi kuwa kumbe zinakuwa edited na kuwekea hizo rangi ili mtu wa kawaida aweze kuzielewa.
Kumbe kiuhalisia hizo picha hata haziko hivyo wana edit kwa kufuata color spectrum. Hivyo zimeacha kunivutia kama zilivyonivutia awali.
 
Sahihi kabisa.
 
Ulikuwa unadhani?
Endelea kudhani hivyo hivyo.

Lengo la hizi picha siyo kwa ajili ya kukuvutia ila ni kwaajili ya somo la astronomy.
Picha hizi ni msaada kwa wanafunzi wa astronomy.

Tanzania hili somo halipo so hazina umuhimu kwako wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…