mike2k
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 1,571
- 3,448
- Thread starter
- #61
Hapa sijakuelewa mtoa mada, ufafanuzi tafadhali. Hapo zinavyo onekana ndiyo ndivyo zilivyokuwa miaka 4.5billion sasa nikitaka kuona zilivyo leo hii nafanyaje au nasubiri tena miaka 4.5billion ijayo ?
Lakini jambo hili linawezekana vipi ? Kwa hiki ulichokiandika.
Hili linawezekana vipi ? Hivi mfano wewe ukitaka kujua miaka 300 hali ilivyo kuwa ni lazima utumie hiki kifaa au upate taarifa kutoka kwenye the "Primary Source" ?
Hapa akili zetu zinatakiwa zitumike vizuri. Yaani unawezaje kujua hali ya dunia kutokea au kuwepo pasi na kuwa na taarifa za walio shuhudia tukio hilo ?
Wanasayansi kuna muda wanakuwa hawaeleweki kabisa, au mimi ndiyo siwaelewi ?
Miaka 4.5 iliyopita.
According to bing bang theory
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali kuliko ya mwanga.
Ili uweze kuelewa vizuri hebu jifunze hapa
Nini kilitokea katika " Big Bang " ? | JamiiForums Nini kilitokea katika " Big Bang " ?
Ukishaelewa kuhusu bingbang theory sasa utakuwa unaelewa ni namna gani ulimwengu ulivyo na unavyofanya kazi.
Kwa sababu ulimwengu unatanuka kwa speed kubwa kuliko mwanga basi utakpokuwa umeamua kutazama katika anga hata kwa macho tu zile nyota unaziona ni vile zilivyokuwa mamilion ya miaka iliyopita kwa ziko mbali.
Kwa lugha nyingine iko hivi
Mwezi unazunguka dunia
Dunia inazunguka jua
Jua nalo linazunguka kitovu cha milk way galaxy,
Na milk way galaxy nayo inazunguka,
Yaani kila kitu katika ulimwengu kiko katika mwendo kasi,
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali sana.
Kwa maana hiyo unapoona mwanga wa jua ina maana umesafiri kutoka katika jua mpaka duniani. Umbali kutoka juani mpaka duniani ni kilometers 150 million kwa maana hiyo mwanga wa jua hutumia dakika nane kufika duniani kwani mwanga unasafiri kwa speed ya km 300000 kwa second.
Kwa maana nyingine ni kwamba jua unaloliona siyo live ila ni lilivyokuwa dakika nane zilizopita.
Mwezi unaouona mwanga wake unatumia 1.3 seconds kufika duniani kwa maana nyingine mwezi unaouona sivyo ulivyo sasa ila ni 1.3 seconds zilizopita.
Kwa sababu ulimwengu unatanuka matukio ya miaka billion iliyopita mwanga wake ndo JWST imeweza kuyanasa wakati huu.
Tunaposema mwaka mmoja wa speed ya mwanga ni 300000km x 60 second x 60 minutes x 24 hours x 30 days x 12 months =trillion 9 km jibu lake ndo km hizo.
Yaani mwanga kufika hapa duniani utachukua mwaka mmoja. Yaani ukibahatika kuona hiyo nyota 🌟 basi sivyo ilivyo sasa ila ni mwaka mmoja uliopita.
Nakupa mfano huu lets say kuna aliens yupo katika nyota ya karibu kbx na solar system inaitwa proxima Centaurus iko umbali wa 4.5 light years away akachukua telescope 🔭 akatazama duniani hapa. Basi ataiona dunia ilivyo mwaka 2018. Yaani ataiona TANZANIA YA MAGUFULI.
Macho yako ni time machine kwani utazamapo angani na ukaziona nyota basi unazipna zilivyo mamilion ya miaka iliyopita.