Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

Shida ya Sayansi ipo katika kukufanya uujue ukweli au kukupeleka katika kuujua ukweli, hapa ndipo kuna mauza uza ya Sayansi.

Maana imewasilishwa, sijaona hata mmoja akihoji kuhusu au juu ya ukweli wa hizo habari. Lakini kwa maendeleo ya sasa katika usawirishaji wa mambo watu kutengeneza picha kama hizo wanaweza sana. Sasa tunapoletewa habari kama hizi watu wanatakiwa waumize akili na kufikiri na kuhoji, kinyume na hapo tutishi miaka yote tukiamini mambo ya uongo na uzandiki tu.
Sahii kabisa,
Wamarekanj ni.mabingwa wa kucheza na akil za Watu[emoji4]
 
Miaka 4.5 iliyopita.
According to bing bang theory
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali kuliko ya mwanga.

Ili uweze kuelewa vizuri hebu jifunze hapa
Nini kilitokea katika " Big Bang " ? | JamiiForums Nini kilitokea katika " Big Bang " ?
Ukishaelewa kuhusu bingbang theory sasa utakuwa unaelewa ni namna gani ulimwengu ulivyo na unavyofanya kazi.

Kwa sababu ulimwengu unatanuka kwa speed kubwa kuliko mwanga basi utakpokuwa umeamua kutazama katika anga hata kwa macho tu zile nyota unaziona ni vile zilivyokuwa mamilion ya miaka iliyopita kwa ziko mbali.


Kwa lugha nyingine iko hivi

Mwezi unazunguka dunia
Dunia inazunguka jua
Jua nalo linazunguka kitovu cha milk way galaxy,
Na milk way galaxy nayo inazunguka,
Yaani kila kitu katika ulimwengu kiko katika mwendo kasi,
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali sana.
Kwa maana hiyo unapoona mwanga wa jua ina maana umesafiri kutoka katika jua mpaka duniani. Umbali kutoka juani mpaka duniani ni kilometers 150 million kwa maana hiyo mwanga wa jua hutumia dakika nane kufika duniani kwani mwanga unasafiri kwa speed ya km 300000 kwa second.
Kwa maana nyingine ni kwamba jua unaloliona siyo live ila ni lilivyokuwa dakika nane zilizopita.

Mwezi unaouona mwanga wake unatumia 1.3 seconds kufika duniani kwa maana nyingine mwezi unaouona sivyo ulivyo sasa ila ni 1.3 seconds zilizopita.

Kwa sababu ulimwengu unatanuka matukio ya miaka billion iliyopita mwanga wake ndo JWST imeweza kuyanasa wakati huu.
Tunaposema mwaka mmoja wa speed ya mwanga ni 300000km x 60 second x 60 minutes x 24 hours x 30 days x 12 months =trillion 9 km jibu lake ndo km hizo.
Yaani mwanga kufika hapa duniani utachukua mwaka mmoja. Yaani ukibahatika kuona hiyo nyota 🌟 basi sivyo ilivyo sasa ila ni mwaka mmoja uliopita.

Nakupa mfano huu lets say kuna aliens yupo katika nyota ya karibu kbx na solar system inaitwa proxima Centaurus iko umbali wa 4.5 light years away akachukua telescope 🔭 akatazama duniani hapa. Basi ataiona dunia ilivyo mwaka 2018. Yaani ataiona TANZANIA YA MAGUFULI.

Macho yako ni time machine kwani utazamapo angani na ukaziona nyota basi unazipna zilivyo mamilion ya miaka iliyopita.
Mimi na nyinyi tunatofautiana sehemu moja, mimi nataka kujua kwanini hizo namba zimekuwa hivyo vilivyo, na nyinyi mnafurahia hesabu mnazowekewa.

Mimi kwanza kabisa unatakiwa uthibitishe ukweli usio na shaka juu ya "Big Bang Theory" au "Big Bang Models"

Aliens ni nani ? Na kwanini Aliens ? Kwanini usiandike chukulia wewe ndiyo upo katila hiyo Nyota fulani ?

Nachotaka mimi unipe hesabu zako pasi na kuwepo "Assumptions" yoyote katika hesabu husika, huo mwendo kasi wa mwanga umepatikana vipi ?
 
Sahii kabisa,
Wamarekanj ni.mabingwa wa kucheza na akil za Watu[emoji4]
Tayari washajua watu hawana muda wa kuhoji na wanapenda kuona mapicha picha basi mnawekewa mapicha na mnafurahi kabisa. Leo ukiingia katika Graphics Design Software mfano tu Adobe Illustrator kuna Scripts zinazokuwesesha kutengeza "Night Sky" au wewe mwenyewe unaweza kudesign from zero Night Sky kama hiyo katika hizo picha, sasa kwa maendeleo haya vipi tutajua hii siyo picha ya kutengeneza, mimi sababu nina uzoefu na haya mambo, hizo picha nilivyo ziangalia tu nikaona siyo picha halisi kabisa.

Mimi katika Sayansi ambayo niliacha kuiamini ni hii Cosmology na Astronomy, yaani kama mtu unatumia akili yako japo kidogo lazima utaona uongo wa hawa watu. Mimi naishi katika mambo ya Sayansi ila Sayansi hii ya anga na umbile la dunia hawajawahi kupatia.
 
Kwa lugha nyingine iko hivi

Mwezi unazunguka dunia
Dunia inazunguka jua
Jua nalo linazunguka kitovu cha milk way galaxy,
Una kubali kwamba Sayansi haijawahi kuthibitisha juu ya hizi nadharia ulizo ziandika hapa ? Mfano wewe unaweza kunithibitishia ya kuwa Dunia inazunguka ?

Jua linazunguka au linatembea ?
 
Kwanza kabla ya ufafanuzi na kukujibu swali lako unatakiwa akili yako ui switch iwe kama ya mtoto ili uwe egoless kuweza kuruhusu ubongo wako kupokea maarifa mapya.

Hii field inahitaji akili kubwa ndo maana huwezi ikuta kwenye vijiwe vya kahawa.

Sasa narudi kwenye swali lako.

Kwanza unapaswa kufahamu kuwa binadamu anaona sehemu ndogo sana ya waves za electromagnetic spectrum inaitwa visible light.

Sasa nikufahamishe kuwa binadamu anapna sehemu ndogo sana ya kilichoko kwenye universe.
Mfano mdogo ni internet mawimbi ya radio huwa hatuyaoni ila yanasafiri from 1 point to another point.
Tukiongea kwenye simu mawimbi yanasafiri hivyo hivyo lakini macho yetu hayana uwezo wa kuyaona.

Matukio yaliyokwisha kupita hatuwezi kuyaona kwa macho coz ni mid infrared katika electromagnetic spectrum. Kwa sababu hiyo JWST hutumia camera ambayo ina uwezo wa kunasa picha katika mid infrared light na yanapotumwa duniani kuna program hutumika kuweza kuzi coloring ili ziweze kuwa visible kwa binadamu kwani binadamu ana uwezo wa ku detect rangi tatu tu ambazo ni red, green, and blue.


Je kwa faida ya wasomaji ni aina gani ya technology hutumika kuweza kufanya photo colorize?
Naomba uitazame vizuri hii video imeeleza vizuri na kwa mifano halisi!.



Nasa wanaelezea hapa namna ambavyo hufanya photo colorize


Sasa kijana hiki kinachofanywa hapa watu wana kifanya sana majumbani mwao na maofisini kwa kutumia hizi "Adobe Products" haya mambo ya Color Grading, yaani hapo bado hujaonyesha ukweli wa hiki unachokiandika hapa.
 
Kisai huwa hupaswi kutoa ushauri kama haujaombwa ushauri..
Hakuna sharti popote pale linalosema ya kuwa kutoa ushauri mpaka uombwe, bali unaweza kutoa ushauri kwa mtu ambaye haoni haja ya kupewa ushauri, sisi tunasema unamsaidia yule aliye ghafilika tena tunaita "SADAKA".
Wewe kama unaona hizi hesabu ni ngumu kwa kichwa chako achana nazo zitakuua.
Kwangu somo la hesabu halijawahi kuwa gumu, na ninacho kiandika hata wakubwa zako walikiona ndiyo maana wakakificha katika msitu wa "Assumptions" kwangu sijawahi kuona hesabu ngumu, kuzidi kuing'amua kesho yangu inakuwaje.

Huenda nina zijua hesabu za kukukokotoa kukuzidi wewe. Sababu sipo hapa kujifaragua na ujuzi fulani au kujua kitu fulani, bali nipo hapa kuwaamsha usingizini. Vijana mmelala fofo, tena mmelala usingizi wa pono.

Nikashangaa leo hii mtu anajadili kuhusu "Big Bang Theory" nadharia mfu ambayo baadhi ya Wanasayansi wanashauri itizamwe upya, mko wapi na elimu na kuihakiki ?

Ziko mada mbalimbali ambazo unaona zinawezekana unaweza kutia nguvu na akili yako huko kuna mada nzuri za michezo, kuna udaku kuna vitu vingi sana ambavyo unaweza peleka ushauri wako huko na ukafanyiwa kazi.
Naona hizi ni dalili za kushindwa kukosoa hoja zangu kielimu. Hizo siyo mada zangu ndiyo maana niko hapa muda huu, hii mijadala sijaanza leo humu jamii forum. Katika mada nyepesi kwangu mimi ni hizi, ambazo nyinyi mnaziona zinahitaji akili kubwa. Sasa sijui akili gani kubwa unaitaja wewe ambayo imekushinda kuujua ukweli uliofichwa kwenye "Assumptions".
Hii field ya astrophysics waachie walioko interested waendelew kishare knowledge zao kwani ni aina ya elimu ambayo haipo katika curriculum zetu.
Hii field si halisi zaidi ya nadharia za kifalsafa. Vingi tu havipo katika mitaala ni vya uongo mfano wa hivi, jiulize huenda walijua ya kuwa wakiweka haya uongo wao utabainika kiurahisi sana.
Hapa hauulizi maswali ili ufahamu ila unauliza maswali ili wakati tayari kichwa chako kina majibu yake.
Sasa si ndiyo ujibu maswali yangu kwa ufasaha, ili uonyeshe ukweli wa hiki unachokijadili ?
 
"Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita."


Mkuu hayo maelezo hapo yana kiuchachu fulani hivi.
Sasa uchachu gani wakati ndio ukweli
 
Mkuu hii dunia tumegawana majukumu, hayo makubwa tumewaachia wao wakubwa, sisi waafrika ni soko, pamoja na kuzalisha raslimali mfano gold, ukienda M.East wao wanazalisha mafuta.
Ni simple idea lkn ndo balance of nature mzee.
Justification tu. Kwani iliandikwa wapi ama una uhakika kuwa umeumbwa ivyo kweli mkuu Ila bana brains kwa kukwepa ukweli tu haijambo ujue.
 
Hivi hii speed ilipimwaje mpaka ikapatikana hii thamani ?

Hii miaka billion 4.5 waliijuaje ? Naomba ufafanuzi kidogo nipate kuelewa.
Kasome history mkuu. Kuna kitu kinaitwa one light year. Dunia unachukua muda gani kulizunguka Sasa huo umbali ndio unaitwa one light year ndio so unit ya distance huko angani, ulisoma zile si unit of length,mass n.k
 
Kasome history mkuu. Kuna kitu kinaitwa one light year. Dunia unachukua muda gani kulizunguka Sasa huo umbali ndio unaitwa one light year ndio so unit ya distance huko angani, ulisoma zile si unit of length,mass n.k
Nithibitishie kwanza ya kuwa dunia inazunguka ?
 
Jua nalo linazunguka kitovu cha milk way galaxy,
Milk way galaxy mkuu Ni mkusanyiko wa hizi sayari zetu Tisa ama kumi,Sasa hizi sayari zote zinazunguka jua ama Zina mfumo wao wa jua hili hili linalotumulika,Sasa vile vile Kuna galaxy kibao huko angani zikiwa na sayari Kama hizi za mfumo wetu. Galaxy Ni jina la mkusanyiko wa sayari zikiwa na jua lake ama tochi. Galaxy inazunguka inaenda wapi.
Ila unaambiwa beyond our solar system ambayo ndio hii milk way galaxy ya kwetu is the endless space extending in all space.
Hii sentence ya mwisho ilinifanya nikiri Kuwa Mungu yupo mkuu. Yaani iyo endless space mpaka niliogopa na sie hapa tupo angani tunaelea elea tu Ila hatuanguki
 
Nithibitishie kwanza ya kuwa dunia inazunguka ?
Hii mbona jiografia fomu wani mkuu. So hauna uhakika kuwa dunia inazunguka. Why do we've four year seasons,toka katika anga la dunia uone kwa mbali tokea juu utaiona unavyozunguka kwa orbit yake na kulizunguka jua mkuu.
 
Time travel.
Relativity theory I loved those shit from University physics na sio Belkin vile vitabu vya kitoto vya physics vile like Roger muncaster, Bannet,
 
Hii mbona jiografia fomu wani mkuu. So hauna uhakika kuwa dunia inazunguka. Why do we've four year seasons,toka katika anga la dunia uone kwa mbali tokea juu utaiona unavyozunguka kwa orbit yake na kulizunguka jua mkuu.
Four Years season ina uhusiano gani na dunia kuzunguka ?

Mimi sijawahi kuona hilo, wala sijwahi kusikia kwamba ukitoka nje ya dunia kwa maana ukiwa angani unaiona dunia inazunguka ? Kwanza naona kwako hili. Wewe tuambia ushawahi kutoka nje ya dunia au ukiwa angani ushawahi kuiona dunia ikizunguka ?

Kingine nitajie majaribio mawili tu ya Kisayansi yaliyo fanyika kuonyesha au kuthibitisha ya kuwa Dunia inazunguka na yakawa ni majaribio ya kweli.
 
Daah mwenzenu nawaza sana kama JWST itatoboa miaka 20 ambayo inatakiwa kuwa operational. Kwani imeshatobolewa na microkimondo huko anga za majuu na leo NASA wametoa picha ya assessment of impact. Daa sijui niwapatie ushauri gani kuzuia tukio kama hili kujirudia, maana katika hesabu zao hawakupigia kukutana na that size ya microkimondo. Ni changamoto sana 10 billion USD.

Hii picha kushoto is new and right is damaged mirror segment.
Unajua kuna Probe imeshavuka solar gravitational influence... Imeondoka duniani 1971
 
Nimesoma mwanzo mwisho, very very interesting. Hii dunia kuna watu wanafanya kazi za maana kwa ajili ya ulimwengu mzima, ninaimagine watanzania na wa afrika kwa ujumla project kama hizi sijui tutufanya lini!
Zinakusaidia nini picha za anga wewe kama wewe. Kumbuka hiyo project ni mabilioni ya dollar, ambapo wewe pia una contribute dollar bila kujua

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom