Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma


Miaka 4.5 iliyopita.
According to bing bang theory
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali kuliko ya mwanga.

Ili uweze kuelewa vizuri hebu jifunze hapa
Nini kilitokea katika " Big Bang " ? | JamiiForums Nini kilitokea katika " Big Bang " ?
Ukishaelewa kuhusu bingbang theory sasa utakuwa unaelewa ni namna gani ulimwengu ulivyo na unavyofanya kazi.

Kwa sababu ulimwengu unatanuka kwa speed kubwa kuliko mwanga basi utakpokuwa umeamua kutazama katika anga hata kwa macho tu zile nyota unaziona ni vile zilivyokuwa mamilion ya miaka iliyopita kwa ziko mbali.


Kwa lugha nyingine iko hivi

Mwezi unazunguka dunia
Dunia inazunguka jua
Jua nalo linazunguka kitovu cha milk way galaxy,
Na milk way galaxy nayo inazunguka,
Yaani kila kitu katika ulimwengu kiko katika mwendo kasi,
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali sana.
Kwa maana hiyo unapoona mwanga wa jua ina maana umesafiri kutoka katika jua mpaka duniani. Umbali kutoka juani mpaka duniani ni kilometers 150 million kwa maana hiyo mwanga wa jua hutumia dakika nane kufika duniani kwani mwanga unasafiri kwa speed ya km 300000 kwa second.
Kwa maana nyingine ni kwamba jua unaloliona siyo live ila ni lilivyokuwa dakika nane zilizopita.

Mwezi unaouona mwanga wake unatumia 1.3 seconds kufika duniani kwa maana nyingine mwezi unaouona sivyo ulivyo sasa ila ni 1.3 seconds zilizopita.

Kwa sababu ulimwengu unatanuka matukio ya miaka billion iliyopita mwanga wake ndo JWST imeweza kuyanasa wakati huu.
Tunaposema mwaka mmoja wa speed ya mwanga ni 300000km x 60 second x 60 minutes x 24 hours x 30 days x 12 months =trillion 9 km jibu lake ndo km hizo.
Yaani mwanga kufika hapa duniani utachukua mwaka mmoja. Yaani ukibahatika kuona hiyo nyota 🌟 basi sivyo ilivyo sasa ila ni mwaka mmoja uliopita.

Nakupa mfano huu lets say kuna aliens yupo katika nyota ya karibu kbx na solar system inaitwa proxima Centaurus iko umbali wa 4.5 light years away akachukua telescope 🔭 akatazama duniani hapa. Basi ataiona dunia ilivyo mwaka 2018. Yaani ataiona TANZANIA YA MAGUFULI.

Macho yako ni time machine kwani utazamapo angani na ukaziona nyota basi unazipna zilivyo mamilion ya miaka iliyopita.
 
Kisai upo sahihi

Maswali yake yana majibu ya wazi.
Kuuliza kwake kutoa nafasi ya kuweza kufunguka zaidi kwa faida ya watu wengine.

Maswali ambayo huwa ni ya kupuuza ni pale mtu aanze kuchanganya Astronomy na dini.
Mada za dini zikiishaingia humu zinaharibu thread yooote.
 
Mkuu mbona antactica watu wapo!
 
Mkuu mbona antactica watu wapo!
 
Mkuu nilkuw makin kupitia mjadala huu mkal maana meenyew bad nlikuw sielew lkn hapa Sasa nmeelewa Asante kw elim hii...[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mkuu nilkuw makin kupitia mjadala huu mkal maana meenyew bad nlikuw sielew lkn hapa Sasa nmeelewa Asante kw elim hii...[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Nashukuru kunielewa mkuu.
 
Maana yake hakuna picha halisi juu ya haya yanayo semwa. Unaposema picha zinahaririwa kwa kupakwa rangi maana yake zinaingia katika uongo na kupoteza uhalisia.

Sasa swali la msingi kwanini wanazihariri na wanajua ya kuwa wanapoteza uhalisia. Huwezi kutokiona kitu, ukatumia sanaa ya rangi kukihuisha maana yake hukipati chenyewe. Hii ni ghishi na uongo wa wazi kabisa.
 
Shida yenu haya mambo hamuyahakiki, na mimi najua kwanini hamfanyi hivyo.

Tuanze kwanza kujua ukweli wa hiyo miaka 4.5billion.

Unaweza kunithibitishia ya kuwa ulimwengu unatanuka kwa huo mwendo mkali sana ? Nani alithibitisha hili na ushabidi uko wapi ?

Unathibitishaje ukweli ya kuwa huo mwanga ulitoka miaka hiyo ? Swali langu bado hujalijibu, bali unanipa maelezo ambayo ili ukweli wake uwe yanahitaji uthibitisho.

Unakubali kama maelezo yako hayajakaa Kisayansi kama Sayansi inavyo jinasibu bali yamekaa kifalsafa zaidi ?
 
Mimi nachoshauri ni kuwa watu wanatakiwa kuwa makini sana na haya mambo, kuna mambo hayawezekani lakini kwa uchache wetu wa akili na maarifa tunaforce mwisho wa siku tunadanganya. Mfano mtu unaambiwa uzito wa jua ni kilo kadhaa ? Sasa unajiuliza tunajua kabisa ili kitu ukipime kuna hatua ainishi fulani na zisizo badilika, sasa ukiangalia kanuni iliyo tumika kukokotoa tungamo la jua ndani kuna "Assumptions" mtu makini atajiuliza kwanini wanaweka "Assumptions" katika hesabu zao, maana yake ukweli wameukosa kwahiyo wanafanya "Assumptions" kukidhi matakwa yao, mwisho wa siku huwezi kuupata ukweli mpaka mwisho wa dunia.
 
Kwanza kabla ya ufafanuzi na kukujibu swali lako unatakiwa akili yako ui switch iwe kama ya mtoto ili uwe egoless kuweza kuruhusu ubongo wako kupokea maarifa mapya.

Hii field inahitaji akili kubwa ndo maana huwezi ikuta kwenye vijiwe vya kahawa.

Sasa narudi kwenye swali lako.

Kwanza unapaswa kufahamu kuwa binadamu anaona sehemu ndogo sana ya waves za electromagnetic spectrum inaitwa visible light.

Sasa nikufahamishe kuwa binadamu anapna sehemu ndogo sana ya kilichoko kwenye universe.
Mfano mdogo ni internet mawimbi ya radio huwa hatuyaoni ila yanasafiri from 1 point to another point.
Tukiongea kwenye simu mawimbi yanasafiri hivyo hivyo lakini macho yetu hayana uwezo wa kuyaona.

Matukio yaliyokwisha kupita hatuwezi kuyaona kwa macho coz ni mid infrared katika electromagnetic spectrum. Kwa sababu hiyo JWST hutumia camera ambayo ina uwezo wa kunasa picha katika mid infrared light na yanapotumwa duniani kuna program hutumika kuweza kuzi coloring ili ziweze kuwa visible kwa binadamu kwani binadamu ana uwezo wa ku detect rangi tatu tu ambazo ni red, green, and blue.


Je kwa faida ya wasomaji ni aina gani ya technology hutumika kuweza kufanya photo colorize?
Naomba uitazame vizuri hii video imeeleza vizuri na kwa mifano halisi!.

https://www.facebook.com/
Nasa wanaelezea hapa namna ambavyo hufanya photo colorize

 
Kuna siku Mungu baaa!! gafla wanadamu hawa hapa wamefika kwenye makazi yake , kuwachunguza wapo hai wala hawajafa[emoji3][emoji3][emoji3]
Hiyo siku ikifika atajua hajui,
Na binadamu walivo watata usishangae wakataka kumpindua[emoji38]
 
Kisai huwa hupaswi kutoa ushauri kama haujaombwa ushauri..hicho tunaita kujipendekeza. Wewe kama unaona hizi hesabu ni ngumu kwa kichwa chako achana nazo zitakuua. Ziko mada mbalimbali ambazo unaona zinawezekana unaweza kutia nguvu na akili yako huko kuna mada nzuri za michezo, kuna udaku kuna vitu vingi sana ambavyo unaweza peleka ushauri wako huko na ukafanyiwa kazi. Hii field ya astrophysics waachie walioko interested waendelew kishare knowledge zao kwani ni aina ya elimu ambayo haipo katika curriculum zetu.

Hapa hauulizi maswali ili ufahamu ila unauliza maswali ili wakati tayari kichwa chako kina majibu yake.
 
Sayansi inavozidi kukua ndipo tunajua hizi dini kumbe tumenyweshwa chai nyingi sana kutoka kwenye vile vitabu vyao wanavyoviita eti ni vitakatifu [emoji4]
 
Wee jamaa fundi Sana[emoji106]
 
Kwanini hizi tafiti hazifanywi na Waraabu au nchi za Asia kama Russis na China? Ni wao Marekani tu?
China na Russia wanafanya Sana,
Na juz Russia katuma chombo Tena anga za juu.

Ila Kwasababu tumetawaliwa na Western media, ambazo Ni mahasimu wakubwa wa China na Russia.

Basi habarnkama hizo hawawezi kukutana maana itakua Ni kuwapa kick mahasimu wake.

Kwa Sasa,
Media zinatuchagulia kipi tusikie, kipi tusisikie[emoji4]
 
Mimi huwa najiuliza hivi mnawezaje kutofautisha hizi picha na picha za kutengeneza ? Yaani mnajuaje kama hizi ni picha halisi na siyo za kutengeneza ? Au huwa mnapenda kuona kuliko kujadili ?
Una point mkuu[emoji106]
 
Mimi huwa najiuliza hivi mnawezaje kutofautisha hizi picha na picha za kutengeneza ? Yaani mnajuaje kama hizi ni picha halisi na siyo za kutengeneza ? Au huwa mnapenda kuona kuliko kujadili ?
Imenikumbusha ile picha ya NASA, jamaa Yuko mwezinj na chupa ya Coca-Cola [emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…