Hatimaye Rais wa FIFA akiri, ataja sababu ya Argentina kushinda kombe la Dunia

Hatimaye Rais wa FIFA akiri, ataja sababu ya Argentina kushinda kombe la Dunia

Tililika tu hoja yako tueleweshane mkuu wala hauna haja ya kufanya utoto
messi-dribble-goal-champions-messi-vs-all-real-madrid-players.gif
 
Ishu sio kupewa penati ishu ni izo penati unapewa katika namna ipi? Penati za ufaransa zote zilikua halali ila ile ya argentina ukiangalia vizuri replay utaona di maria hakuguswa
Penalty ya pili ya Ufaransa haikua halali, alie peleka mpira kwa mbape alitumia mkono , haikupaswa kuwa Penalty
 
Statistical gaucho hamgusi ata Neymar
Tatizo mchezaji siku hizi anapimwa kwa magoli na assists pekee, kitu ambacho kimepelekea wanaocheza nafasi za nyuma kutoonekana kama wachezaji bora..

Unakuta mtu kama Lewandowsk anatajwa kama mcheza bora kisa tu anafunga sana magoli, lakini nje ya hapo hana tofauti na Bocco.

Mpira sio takwimu tu maana kuna siku hayo magoli hayapatikani, sasa mtu anayeangalia huo mpira anafurahia kipi?, ukipata majibu ndo utajua Gaucho, Zidane, Delima na wanaofanana na hao ndo wachezaji bora ila hao wengine ni wafungaji bora.

Mchezaji kama Maradona kitakwimu hata Giroud anamzidi mbali sana ila ukitaja wachezaji bora watano kuwahi kutokea lazima awepo tena ndani ya nafasi tatu za mwanzo.
 
Tukizungumzia mpira kama talent, ni kuukosea heshima mpira kumuweka ronaldo hapo, unless umaanishe De Lima.

Ronaldo alipambana kwa jasho zito ili apambane na Messi na sio kwamba alikuwa na kipaji. Vipaji tunazungumzia akina Messi, Mbappe, Vinicious, Neymar, Iniesta n.k
yani unasema cr7 hana kipaji halafu unasema mbappe anakipaji? fuc*n.
 
Messi kacheza mpira kipindi ambacho mpira umeadvance mno, maradona mpaka magoli ya mkono amefunga. Huyo pele hata idadi ya mechi alizocheza na magoli havina uwiano.

Wamecheza mpira kipindi ambacho mpira ni kama sehemu ya burudani, soka halikuwa na pesa kama sasa kwamba mtu anaingia uwanjani kikazi zaidi.

Mazingira alocheza soka Messi ni magumu kulinganisha na hao wengine. Messi ni bora zaidi, hakuna kama Messi.
Kwan messi hajafunga goli la mkono?
 
Napenda mpira lakini huwa sitaki kuwa kwenye kiwango cha ushabiki ambacho kitanifanya nionekane kama mtu aliyepagawa. Ndiyo maana hata hili kombe la dunia sijaangalia hata mechi moja zaidi, ya kupewa matokeo.....
 
Acha uongo mzee baba messi anaingia kikosi cha kwanza tayari timu ilikua nzuri na inafanya vizuri kabisa kumbuka aliwakuta dinho, etoo, deco wapo kwenye form.. mchezaji ambae alikuja kufanya transformation ya barca ni dinho kipindi jamaa anafika barca ilikua na jina kubwa lakini bado inajitafuta yaani kama man u pale uingereza sasa hivi.. dinho aliibeba timu ikaja kuwa tishio ulaya messi alikuja kuwa star wa barca tayari timu ikiwa ni nzuri sana
Kweli Kabisa Ndugu Yangu Messi Ameikuta Barca Ya Moto , 2006 Unaikumbuka Fainali Vs Arsenal
 
Tuacheni unazi. Kama wanabebwa kwanini awamu zote za penati wasingewatoa Argentina? Zile penat kipa alizokuwa akicheza nazo ni hujuma?
Penat walikuwa wanapiga FIFA ndio maana wakawa wanakosa makusudi.
 
Pole sana mleta uzi kwa kuumizwa na ushindi wa Argentina. Miaka minne ijayo mtoe ushauri kwa Ronaldo naye ashinde muweze ushangilia. Sis wengine tunafurahia tu kuangalia mpira
 
Kama sikosei ilikuwa 2010.

Mashabiki wa Man U, team ronaldo, ambao kwa sasa wanafahamika kama team mbappe walikuwa na ujasiri sana na viungo wao, hasa paul shcoles na park ji sung, wakiamino pia kijana wao fletcher atawitia kwapano akina Iniesta na Xavi. Wakadai Scholes pasi zake hakuna wa kuzizuia pale Barca.

Unajua mkuu mashabiki wa ronaldo uwendawazimu haujawaanza leo wala jana, wamewehuka toka kitambo. Ule utatu wa Sergio Busquets, Xavi na Iniesta ulikuwa unacheza kimfumo na sio uwezo binafsi hata useme uje unawakaba wao.

Kilichotokea wote hawaamini ktk ile game, mtoto mdogo pedro akamtengua kiuno beki wao bora fabio, akashikilia bomba ili aweke kiuno sawa, jamaa akazidiwa, jopo la madaktari wakaja kumtoa nje ili kumtibu.

Shinji kagawa akapewa asimame na Erick Abidal, mipora yoote ilikuwa inatua kwa Erick Abidal, Fletcher, Pak Ji Sung wote wakapoteana ndani ya Game. Fergason hakuamini kama ile ndo Man U aloisuka kuingia fainal, alipata mtetemo mzito, kwa mtetemo ule akaona heri astaafu ili kuepuka mauti kwa presha uko mbeleni.

Messi alikuwa anamuokota Ryan Gigs, chukua Pak Sung, sijui Ferdinand na tumbili wengine kisha anatembea na mpira mbele
Ila barca hyo hyo ya Messi ilitolewa na united mwaka 2009 Kwa Bao maridadi la Paul Scholes. Mmekazana tu fainali.
 
Achaneni na Messi jamani, tena mkae kimya kabisa.

Licha ya kuundoa ufalme wa Madrid pale Spain ambao Gaucho, Romario, Rivaldo walishindwa, Messi aliweza.

Messi akavunja utawala wa Brazil kule America. Tafuta head to head za Brazil na Argentina, kaone huko balaa la Messi. Za Madrid na Barca achana nazo maana utalia.

Messi ndio mfungaji bora wa muda wote Argentina, Barca, La Liga kwa Ujumla, UEFA sijui alifikiaga wapi ila kuna muda aliweka rekod.

Messi kachafua saaana timu za England, kumbuka Messi alimfanya Sir Alex atetemeke pale Wembley.
We jamaa acha kuota lini Madrid kaondolewa ufalme na uyo Messi akiwepo Barcelona watu wame win la Liga Title mara 35 watu Wana champions league 14 Huku nyingine wabeba wakati Messi anacheza Barcelona 2014,2016,2017,2018 kuwa na adabu na Real Madrid
 
Messi kacheza mpira kipindi ambacho mpira umeadvance mno, maradona mpaka magoli ya mkono amefunga. Huyo pele hata idadi ya mechi alizocheza na magoli havina uwiano.

Wamecheza mpira kipindi ambacho mpira ni kama sehemu ya burudani, soka halikuwa na pesa kama sasa kwamba mtu anaingia uwanjani kikazi zaidi.

Mazingira alocheza soka Messi ni magumu kulinganisha na hao wengine. Messi ni bora zaidi, hakuna kama Messi.

kwani Messi hajawahi kufunga goli la mkono?
 
We jamaa acha kuota lini Madrid kaondolewa ufalme na uyo Messi akiwepo Barcelona watu wame win la Liga Title mara 35 watu Wana champions league 14 Huku nyingine wabeba wakati Messi anacheza Barcelona 2014,2016,2017,2018 kuwa na adabu na Real Madrid

Uefa wamebeba mangapi wakati wa mfalme?

La liga wamebeba mangapi wakati wa mfalme?

Copa del Rey?

Super copa?

Ballon d'Or?

Anzia mwaka ambao messi ameingia rasmi fc barca
 
Messi apewe kila kitu mpaka UGOAT ila gaucho aachwe na abaki kuwa Gaucho wala asitajwe tajwe. Kipindi chake kilikuwa kifupi cha burudani sana sana.
 
Back
Top Bottom