Hatimaye Rais wa FIFA akiri, ataja sababu ya Argentina kushinda kombe la Dunia

Hatimaye Rais wa FIFA akiri, ataja sababu ya Argentina kushinda kombe la Dunia

Messi ndie mchezaji bora zaidi ulimwenguni kuwahi kutokea, tusipingane na hili.

Ndani ya Nou Camp Madrid ilokuwa na mastaa kibao iliicharaza Barca bao 3. Messi akaingia akitokea sub, kipindi hiko ana miaka 19.

Messi anaweka Hat Trick na kuinusuru Barca, humo ndani madrid kulikuwa na Zidane, Ramos, Carlos, De Lima, Raul na mastaa wengi sana.

Toka wakati huo, Barca ikavunja uteja wa Madrid. Toka Messi apewe nafasi Barca, 80% ya kombe la Ligi limetua Barca.

Alibadili kila kitu pale Spain.
Alibadiri kila kitu Spain kipi?. Kuisawazishia Barca ndio tayari kubadiri?.
 
Hakuna ubingwa wa kupewa, Argentina walipambana Sana na walistahili.
 
Kwani uongo ninyi sio team ronaldo?
Sinaga masuala ya uteam kwa kweli yaani iyo sio kwenye soka tu hata dini siasa n.k mtu awe chadema au ccm, awe mkristo au muislamu pale ambapo jambo halipo sawa nasema hapa sio sawa pale ambapo lipo sawa nasema hapa ni sawa
 
Mashabiki wa messi mnalazimisha kubadilisha upepo wa mada., mtoa mada kajenga hoja yake kwa kuoanisha maneno ya baadhi ya wachezaji na maofisa wanaohusika na uendeshaji wa hii michano kwa kuonesha kuna uwezekano kwamba ilipangwa messi achukue hili kombe ilitakiwa mtoe hoja zenu kwa kuangazia mada husika cha kushangaza mnaleta story za ushindani wa ronaldo na messi., mfano penati aliyopewa argentina kwenye fainali ilikua mbeleko kwa sababu di maria akuguswa hapo ulitakiwa kupinga kwa kusema ile ilikua penati halali kwa sababu hii hapa... sio hayo mambo mengine hayo mambo ya rekodi, ballon dor sijui messi kuchukua vijiji wote tunayajua toeni hoja zenu kwa kuangazia mada husika
Umezipitia hizo nukuu za viongozi anao wasema ama na wewe umeunga mkono kwasababu alichokiandika kinaendana na hisia zako?.
Dah!!
 
Messi ndie mchezaji bora zaidi ulimwenguni kuwahi kutokea, tusipingane na hili.
Assuming Pele na Maradona ni untouchables na hawamo kwenye list

Messi hawezi kuwa juu ya Pele.
 
Umezipitia hizo nukuu za viongozi anao wasema ama na wewe umeunga mkono kwasababu alichokiandika kinaendana na hisia zako?.
Dah!!
Uenda hao viongozi walimaanisha kitu kingine na mtoa mada akaelewa vingine lakini nilichomwelewa mtoa mada alichotaka kusema ni kwamba kulikua na mpango wa kuwezesha messi achukue world cup
 
Assuming Pele na Maradona ni untouchables na hawamo kwenye list

Messi hawezi kuwa juu ya Pele.
Huwa najiuliza kama messi angecheza zama za pele na maradona je angeweza kuwafunika? Na kama maradona na pele wangecheza zama za messi je wangeweza kumfunika.. huu mjadala ni mgumu sana maana wote wamecheza vizazi tofauti binafsi natamani sana ningewashuhudia hawa magwiji wawili wakicheza, nimeangalia video zao tatizo youtube hakuna mchezaji mbovu uko ukiangalia video za fellain unaweza kusema alikua zaidi ya zidane
 
Sasa atokee mtu abishane na Ancelotti
Screenshot_20221219-195815_Samsung%20Internet.jpg
 
Back
Top Bottom