Hatimaye: Serikali ya Tanzania yafuta mkataba wake na Kampuni ya Kenya (Indo Power Solutions LTD) iliyojinasibu kununua Korosho kwa Bil 400

Hatimaye: Serikali ya Tanzania yafuta mkataba wake na Kampuni ya Kenya (Indo Power Solutions LTD) iliyojinasibu kununua Korosho kwa Bil 400

Walitaka kuzungusha pesa kutoka mkono wa kulia nyuma ya mgongo kwenda mkono wa kushoto waseme mkono wa kushoto umenunua kumbe ni wao mkono wa kulia lengo ni kuficha aibu ya kutonunuliwa korosho na wangenunua kwa mkono wa kulia watu wangeuliza kwanza pesa mmetoa wapi, bajeti ipi na baada ya kununua kinachofuata ni nini? Uzuri wenye uelewa na mapenzi ya nchi wakashtuka wakaanika mambo. Nadhani CAG hapa angekagua angekutana na madudu, mtu mzima kaamua kuchutuma. Hataree
Hii inafundisha:

1.Serikali haiwezi kufanya biashara, wakifanya hivyo wataingia hasara kubwa
2. Hata uwe na pesa kiasi gani, unahitaji elimu na maarifa au upate watu sahihi kwa biashara hiyo ndio ufanikiwe.
3. Ndio maana benki, hazitoi hela au mikopo kwa mtu ambaye, hajadhihirisha uwezo katika kile anachotaka apewe mkopo
4. Fedha za walipa kodi zimepotea na ni hasara kubwa
 
Naona sasa ni wakati wa kuanzisha masoko ya kuuza korosho kila mkoa, maana kwa madini wameanza, hii KOROSHOW inasumbua taifa, haaahaaaa... nchi hii!!!!!!!!!!!!
Hivi mtwara hakuna sangoma?
 
Hapo ndio ukipitia kazi za intelijensia zetu utajua ni kwa ajili ya Chadema. Tunapigwa kirahisi halafu kina Zitto, Lissu, Msigwa wakija kutoa kwenye PC wanaambiwa wanatumika na mabeberu. Nchi imetokomea kuwasikiliza baadhi ya watu Fulani tu wapiga porojo za ccm. Kina Bashiru hawawezi kusema ukweli na kutoa ushauri Bali ni kujipanga kwa uchaguzi tu
 
Rahisi sana kuwatapeli kina Sultan Mangungo, ukija kufanya deal kodisha private jet , shuhudia zoezi zima la utiaji saini na 'siasa' nyingi ktk video hapo chini :

Mfanyabishara atua na Ndege binafsi kununua tani 100,000 za Korosho

30 Jan 2019

Bodi ya Nafaka na mazao imetia saini na Kampuni ya Indo Power Solution ya kwa ajili ya Ununuzi wa Korosho Tani laki moja ambapo viongozi mbalimbali wameshuhudia mkataba huo akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi ,Waziri wa Viwanda na biashara, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mkoani Arusha.
 
Hapo ndio ukipitia kazi za intelijensia zetu utajua ni kwa ajili ya Chadema. Tunapigwa kirahisi halafu kina Zitto, Lissu, Msigwa wakija kutoa kwenye PC wanaambiwa wanatumika na mabeberu. Nchi imetokomea kuwasikiliza baadhi ya watu Fulani tu wapiga porojo za ccm. Kina Bashiru hawawezi kusema ukweli na kutoa ushauri Bali ni kujipanga kwa uchaguzi tu
Uzibeze usichokijua
 
Kuna mtu huko limemfia.
IMG-20190510-WA0020.jpeg
 
Hii ndio mikataba anayoingia Profesa Kabudi. Nikashamuona Profesa Kabudi kwenye jambo lolote huwa najua kabisa hamna jipya hapo.
Huyu waziri ni kilaza kweli kweli na mpenda kusema "Ndiyo mzee". Anaweza hata kuletewa mkataba wa kufufua wafu na akausaini! Ila namshukuru Mungu nimemjua kiundani maana nilikuwa nikimuona akitoka povu namuona wa maana.
 
Kuna zinazobanguliwa sasa hivi, viwanda vipo full capacity, Kuzibangua zote hadi ziishe itachukua miaka kama 12 hivi
Kumbe tatizo ni ubanguaji na sio soko. Maana tunaweza zitumia ndani ya East Africa tukazimaliza kabisa. What are long run strategies? TZ haina wawekezaji kwenye sector hii??
 
Nilitaka nishangae yaan upige deal na mkenya usiende fyongo??? Hahaha bora wamefuta tuu maana hata Hela yenyewe hawana kazi usumbufu tuu
 
Msimu huu nimesitisha kuendeleza shamba langu la korosho.
Wale wanunuzi kutoka nje (India & Vietnam) sijui serikali itawashawishi nini ili waje tena Tanzania.
 
Tulisikia kuwa walishaanza kubeba tani 10,000, jee walizilipia hizo, ama ndio pigo lililopangwa?
 
Lumumba tupeni tathimini hii U turn
Mimi ni mwanachama wa ccm, tena wakulipa ada, hili ni janga kubwa na kosa linalohitaji viongozi wengi kuwajibika. Serekali ya chama changu ije iwaombe radhi watanzania na wakubali makosa yao, watuwekee wazi hasara nchi na wakulima walizopata kwa mkurupuko wa zoezi hili.
 
Kwa ujumla Kabudi ni mjinga fulani, huyu Kabudi ndio alikuwa kwenye majadiliano ya na wazungu wa Barrick, alitoka kwenye ule mkutano na maelezo ya uongo, mara sijui tutalipa kishika uchumba, mara sijui wanapitia deni letu. Yaani hadithi kibao.
Huyu mparamagaga kabugi huyu!we mwache tu na mijicho yake ile
 
Kila Nikitaka Kuandika Huwa Namkumbuka Mdude Chadema Sijui Kwanini!!
Sometimes unajisikia kuwatukana hawa watu mpaka marehemu bibi zao na babu zao aka ukoo wao ila mdude mdude katuharibia spirit ,maana wamemgeuza sura hv hv mi sikumjua kabisa kwa uumukaji ule
 
Ni vichwa vigumu tu.
Watu wengi tu walitoa tahadhari ya kuingia mkataba na hiyo kampuni.
Nakumbuka hata serikali ya Kenya ilitutahadharisha kuwa hiyo kampuni haina ofisi zinazofahamika wala haijawahi kufanya biashara ya korosho. Serikali iliamua kuziba masikio, na sasa ndiyo wanashtuka wakati wamechelewa!
Awamu hii ya tano viongozi wote wa serikali ni wendawazimu kama wanavyojinasibu.
 
Huyu waziri ni kilaza kweli kweli na mpenda kusema "Ndiyo mzee". Anaweza hata kuletewa mkataba wa kufufua wafu na akausaini! Ila namshukuru Mungu nimemjua kiundani maana nilikuwa nikimuona akitoka povu namuona wa maana.
[emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom