Hatimaye Vyombo vya Habari vya Tanzania vyajiondoa ndani ya Chungu, hebu Someni hili gazeti

Vyombo vya habari haviko huru, wanaripoti habari za maandamano kwasababu Serikali imeyaruhusu na hivyo haina madhara kwao wakiripoti.

Ila ingekuwa tofauti kama Serikali ingekataa yasiwepo. Unafiki ni mwingi sana.
 
Hakukuwa na gwanda hata moja.

Yale magwanda yaliyokuwa yakiuzwa hapa JF.

None zero Kalas.
 
Kwa sababu limeandika uongo unaokufurahisha?
 
Yet mnatoa lugha chafu Kwa Dr Samia, mnadhani haya mambo yanatokana na katiba la hasha kwani miaka yote mabomu yalipokuwa yanatumika kutawanya waandamanaji hakukuwa na viongozi!? Kongole Kwa Dr Samia
 
Huenda tukaaza kununua magazeti kwani tuliacha kabisa kununua upuuzi wa kupangiwa vya kuandika!
 
Hivi mnaongea demokrasia mnaijua nyie lakini, umaskini wa afrika unaletwa na huu ujinga unaitwa demokrasia, ukiona mzungu anafosi jambo lifanyike africa jua ni kwa ajili ya manufaa yake na sio ya waafrica sijui huu umbumbumbu africa utatoka lini
Kama hutaki demokrasia unataka nini?.Kwasababu nikama ata haujui demokrasia ni nini.
 
Najiona kama vile nashawishika kununua magazeti
Nakumbuka zamani nilikuwa mapita banda la magazeti makusanya karibia gazeti tano, alafu natamani nifike home nitulie nasoma moja. Baada ya moja
Nilikuwa nainjoy kiukweli
 

Jana Tanzania nzima imeona na kuamini kwamba wanaopenda na kuleta fujo sio wanaoitisha maandamano bali wale wanaoyapiga marufuku.

Hekima za Rais Samia zimetusaidia kujua tatizo lipo wapi.
 

Jana Tanzania nzima imeona na kuamini kwamba wanaopenda na kuleta fujo sio wanaoitisha maandamano bali wale wanaoyapiga marufuku.

Hekima za Rais Samia zimetusaidia kujua tatizo lipo wapi.
Si Hekima za Samia , shukuruni Wazungu
 

Mkuu, mimi sifanyi siasa hapa. Wakati wa Magufuli hao wazungu hawakuwepo?

Lazima tukubali ukweli, maandamano ya jana yamewezekana kwa hekima za Rais Samia. Hata hivyo pia sio sawa haki za watu kutegemea hekima ya mtu mmoja.
Washauri wa Samia ndio akina Makonda , unadhani hawa wanataka maandamano ?

Ndio maana tunakuambia Washukuru Wazungu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…